Mahesabu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2008
- 6,658
- 6,700
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani kama vile upo kwenye fikra zangu.Marekani Kwa ushirikiano na uingereza na kwa kuwashirikisha marafiki zao wa west na kwa kuitumia Ukraine wamefanikiwa kwa kiasi kupunguza silaha muhimu za Urusi,kwa kuipa Ukraine silaha za kupiga melivita, ndegevita ,Mifumo ya ulinzi na baadhi ya silaha muhimu za Urusi.
Hii kwa upande wa USA na marafiki zake inaweza kua ni faida kwao.
Imekua ni rahisi kwa Ukraine Kwa msaada wa west kupiga baadhi ya silaha za Urusi hata zile ambazo zilikua zimepaki TU wala hazikua kwenye uwanja wa vita,lengo ni kuitia hasara na kuidhoofisha urusi.
Urusi imepoteza ndege na hata meli muhimu.
Ingawa Magharibi wao hawajapoteza meli wala ndege zaidi ya meli na ndege za Ukraine,hii ni faida kwa USA na marafiki zake.
Lakini ukweli ni kwamba hata hao USA na NATO wangekua wanaingiza meli zao na ndege zao vitani, nao pia wangepoteza kwa wingi sana,kwa sababu nao Russia Wana uwezo mkubwa sana wa kupiga meli na ndege za USA ,UK,FR na wengineo.
Salama Yao ni kwamba za kwao hazitumiki katika vita hii au ndio maana wakaogopa kuweka No fly zone kwa sababu wanajua uwezo wa Urusi.
Hii pia ndio sababu ya USA kusita kupeleka. F16.
Hata hivyo bado Urusi nae ameendelea kuwatia hasara kama vile wanavyomtia wao.
Mfano hapa juzi kateketeza treni yenye malundo ya silaha kutoka NATO nyingi zikiwa ni kutoka USA zilizokua zinaenda mstari wa mbele zikitokea Romania zikiwa ni msaada kwa ukraine.
Sio hizo TU,Bali tokea smo hii ianze Urusi amekua akiangamiza maelfu ya silaha kutoka west kwenda Ukraine katika maeneo mbalimbali,nyingine zikiwa kwenye maghala,melini,ama barabarani ama uwanjani.
Kwa kifupi Urusi kateketeza silaha zao nyingi Hadi wakaanza kulalamika kua wameishiwa akiba ya silaha Kwa ajili ya ulinzi wa Mataifa Yao.
Hata hivyo,Kwa jinsi USA anavyoipa silaha,ushauri na misaada Ukraine ili kuidhoofisha urusi,tutegemee kabisa kuanzia Sasa kua USA haitathubutu Tena kuvamia nchi nyingine,kwa sababu anachokifanya kwa Urusi kupitia Ukraine,atafanyiwa mara mbili na Urusi na washirika wao.
Na huenda hii ndio ilikua na ni sababu ya USA kuepuka kuishambulia au kuivamia au kupigana na Iran,kwani anajua Urusi,Korea kaskazini na hata china watamfanyia anachokifanya huko ukraine.yaani nao watampa Kila aina ya misaada Iran ili amtoe nishai USA.
Kwa muktadha huu naamini USA haitafanya uvamizi kwa nchi nyingine kama ilivyozoea.
Nina wasiwasi hata huenda Iran ilipewa go ahead na Urusi china na north Korea kujibu mapigo ya Israel ili Israel ikiingia kwa nguvu zake zote kuishambulia Iran,Iran nayo ijibu kisha wazipige ili,USA akiingilia kuipiga Iran, Russia na kundi lake nao waiadhibu USA kwa staili ileile USA anayoitumia kumdhiofisha Urusi.
Nahisi USA alishitukia,nae akasanda na kumtaka Israel asijbu kwa nguvu.
Kuna kauli nyingi humu kwenye nyuzi za Israel na iran zilikua zinasema kua Iran katafutwa mda mrefu Sasa ameingia mwenyewe mtegoni kwamba atapigwa na USA ,lakini kibao kimechenji ni kwamba Sasa USA ndio anatafutwa na genge la Urusi ambalo wahuni houthi wamo,na wemchokoza USA kishenzi lakini wapi USA kachomoa kuingia mtegoni pia Hadi kaamua kuondoa meli zake maeneo katika maeneo ambayo houthi wanaweza kumfanyia kitu mbaya.
Naamini kama USA angeingia vitani na Iran kama wengi walivyokua wanadhani humu,huenda miongoni mwa ambao wangepewa vifaa muhimu na Urusi,china na Korea kaskazini ili kumdhiofisha USA, Houthi wanengekua katika orodha hiyo kwa sababu wameonesha uwezo mkubwa sana wa kumdhibiti USA kibabe.
Ndugu zangu Dunia Sasa imeshabadilika kutokana na vita vya Ukraine,Kwa Sasa USA nae anatafutwa kwa udi na uvumba,akijichanganya TU kuvamia kiji nchi Fulani atajuta,na Sasa naamini hatafanya kosa kama hilo Tena.
Hebu fikiria USA amekua wa kukimbizwa na WA Houthi?
Ama Leo USA amekua wa kufukuzwa na vijinchi vya Kiafrika?
Dunia imebadilika kwa Kasi sana.
Nidhamu imeanza kuja mdogomdogo.
Haya ni mawazo yangu TU,sio lazima iwe sahihi.
Dah kweli kama unavyosema,inaonekana kweli urusi alishaisoma USA kitabia nje ndani,yaani alijua kabisa kua,wataniwekea vikwazo,watampatia Ukraine silaha za Kila aina,watajaribu kuzishawishi Dunia imtenge,watahodhi Mali zake na Kila aina ya fitina ni kama Urusi walijua,maana Kila kilichofanywa na west kuibana Urusi,ukweli kimedunda,na kibaya zaidi imetokea vingine vimewaathiri wao wenyewe.Yani kama vile upo kwenye fikra zangu.
Sema tuendako lazima USA atatumiwa katoto ka kumchokonoa ili atoe makucha kisha wayakate... Kwa upande wa Urusi alijiandaa sana na akawa haweki silaha zake za nyuklia hovyohovyo la sivyo zingelipuliwa ndani kwake kwa namna itakayoonekana kuwa ni ajali ya bahati mbaya.
Si unaona Ukrine na washirika wake wanavyorusha mabomu hovyohovyo kwenye kinu cha zaporizhzhia kilichopo Jimbo lililotekwa na Urusi? Warusi hawakuwa wajinga kukiwahi hicho kinu na kuweka ulinzi wao ili kuepusha ajali zinazoweza kusababishwa na wendawazim/NATO.
Na ikitokea bahati mbaya Ukraine wakafanikiwa kubutua kinu hicho cha zaporizhzhia ambacho ni cha pili kwa nguvu ulaya nzima basi ujue opareshen ya Urusi itabadilika kuwa vita ambayo hata marekani na washirika wake watakaa mbali sana huku Ukraine ikikaangwa mbele ya macho yao.
Alafu cha kuongezea, siri nyingi za intelligence za USA zimefichuka kama kuna post moja humu kuna jamaa anaelezea CIA inavyofanya kazi kwa kuvuruga usalama nchi zingine kwa kufadhili makundi na kutrain pamoja na kuharibu mahusianobya nchi zingine kama ile ya Nordstream pipelineDah kweli kama unavyosema,inaonekana kweli urusi alishaisoma USA kitabia nje ndani,yaani alijua kabisa kua,wataniwekea vikwazo,watampatia Ukraine silaha za Kila aina,watajaribu kuzishawishi Dunia imtenge,watahodhi Mali zake na Kila aina ya fitina ni kama Urusi walijua,maana Kila kilichofanywa na west kuibana Urusi,ukweli kimedunda,na kibaya zaidi imetokea vingine vimewaathiri wao wenyewe.
Ukweli kwa wanaotafiti kwa kina,wataona kama vita hii imeiheshimisha sana Urusi kuliko hata kabla,yaani watu wengi wameujua uwezo wa Urusi kijeshi,kiuchumi na kidiplomasia,
Wamewajua wamagharibi na kuwaona kama ni waoga TU,wanaiona Urusi kama mbabe anaepigana na wababe wengi yeye peke yake wao wakiwa wengi.
Hii ni kama movie vile,yaani ni ugomvi baina ya mtu mmoja dhidi ya kundi la majambazi.
Kwa kifupi Urusi ameushangaza ulimwengu.