JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Kiukweli huwa nasikitika sana nikikuta mtu anasema speed ya gari kubwa mathalani mabasi huwa ni kubwa kuliko speed ya gari ndogo. Unaweza kupitia comments za post niliyoiweka hapo juu.
Hoja yao kubwa huwa tairi ya gari kubwa ni kubwa kuliko ya gari ndogo hivyo hivyo tairi ya gari kubwa itafanya mizunguko mingi kuliko ya gari ndogo. Hii si sawa.
Uhalisia upo hivi. Katika speed fulani mfano 50kph. Tairi ndogo itafanya mizunguko mingi kuliko tairi kubwa ili kumaintain distance iliyokuwa covered.
Kiuhalisia speed ni speed. Hivyo ikiwa 50kph kwa basi hata kwa gari ndogo itakuwa ni 50kph.
Kwenye gari whether speed wamechukulia kwenye mzunguko wa tairi au kwenye gearbox, lazima calculation zifanyike na lazima zihusishe mzunguko wa tairi.
Ukitaka kuprove kwamba speed 200kph ni sawa kwa gari ndogo na kubwa. Siku ukisafiri na basi kaa mbele eneo ambalo unaweza kuiona speedometer ya dereva.
Set navigation kwenye google map ya simu yako [Hii huwa inaonesha speed]. Gari ikianza kutembea linganisha speed kwenye simu na kwenye gari. Huwa zipo sawa.
Siku nyingine jaribu pia hivyo kwa gari ndogo.
Utarealize speed ni speed no matter what.