Mimi nakupinga vikali sana Mkuu, ukiniambia Halotel na kifaa chako nita kuelewa. Halotel ni bora wajitoe tu kwenye maswala ya huduma za internet. Pili kifaa chako jaribu kupata simu achana na hicho kifaa utakuja ni shukuru. Natumia Voda na Airtel internet kwa level ya 3G & 4G tu speed nayo pata ina tosha kwenye upande wa simu na computer speed ya 5MBps ni standard kabisa kwa kustream mpaka 4K videos, kufanya video call, kubrowse etc.
Ila kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya internet japo sita weza kutoa statistical data ila kwa mlundikano wa internet routers zinazo uzwa mtaani una weza jipatia jibu, hili limepelekea kuwe na load kidogo kwenye mitandao kama Airtel mida flani haswa ya jioni japo kwa uwepo wa mkonga mkubwa hivi sasa wana limudu hilo bado kasi ipo vizuri kz wanao fanya streaming kwenye TV wana weza toa ushahidi buffering sio nyingi.
Kumalizia napenda kukushauri badilisha hicho kifaa tafuta simu RAM kuwa kubwa bado sio kigezo cha ubora wa kifaa chako simu zipo, narudia kuna simu ongeza mapambano yako upate simu ya kueleweka.