Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

MAKOSA 30 AMBAYO WATOTO WA ZAMANI WALIKUWA WAKILA BAKORA!!
WATOTO WA ZAMANI WALIISHI MAJUMBANI KAMA WAKO MAFUNZO YA KIJESHI!! WAKIKUA NI FULL ADABU KUHESHIMU WATU, UTU, BUSARA NA KUJITETEGEMEA WAKIWA NA UMRI MDOGO TU
1: Usiposalimia wakubwa asubuhi unapigwa
2: Usiposalimia wageni unapigwa
3: Ukinawa kabla ya wageni unapigwa
4: Ukilia bila sababu unapigwa
5: Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka unapigwa
6: Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni unapigwa
7: Ukikaa wakubwa wamesimama unapigwa
8: Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi unapigwa
9: Ukichelewa kurudi toka shuleni unapigwa
10. Ukiwahi kurudi shuleni unapigwa
11: Ukililia wageni wakati wanaondoka , wakitoka unapigwa
12: Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula unapigwa
13: Kujibu ovyo wakubwa unapigwa
14: Kutukana watu wazima, watoto au rika lako unapigwa
15: Ukiwa mbishi bila sababu unapigwa
16:Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze
17: Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie
18: Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa
19: Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa unapigwa
20: Ukila kwa jirani ukabainika unapigwa
21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani unapigwa
22: Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa unapigwa
23. Ukimkuta mtu nzima hujampokea unapigwa
24. Ukienda kusema kama umepigwa unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia unapigwa.
26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani unapigwa
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani unapigwa
28. Ukianza kuchaguwa chakula hiki nakula hiki sili unapigwa
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao unapigwa
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli unapigwa
31.Ukikaa na wakubwa halafu ukaanza kucheka bila sababu unapigwa.
32.Ukimwuliza Baba/ Mama umetoka wapi unapigwa.
Endapo umepigwa na Ukasusa chakula unapigwa .
33.Ukilala bila kula unapigwa.
34.Ukiitwa ukaja kimyakimya bila ya kuanza kuitika unapigwa.
Wahenga njoooni tukumbushane [emoji2]!
 
LIKIZO TIME YAKUPASAYO KUFANYA MZAZI WAKATI WA LIKIZO UKIWA NA WATOTO WAKO

(1) Mshukuru Mungu
[emoji117]Shukrani kwa Mungu kwa watoto wako kurudi salama,na kumaliza mhula wa shule salama, wako watoto wengine hawakuweza waliuugua,walifariki nk

(2)Wape muda watoto
[emoji117]Najua kweli mzazi upo bize kutafuta ridhiki ya kila siku,lakini wape muda watoto wako kipindi Cha likizo,kaa nao,angalia Kama Kuna mabadiliko yoyote ya kiroho au kimwili. Wape muda punguza ubize.

(3) Wasikilize
[emoji117]Jamani wazazi tuwe na tabia ya kusikiliza watoto wetu,wana mengi wamepitia wakiwa mbali na wewe,hebu wape muda wa kuwasikiliza basi,wanatamani kusema Ila hawana pa kusemea wape mudaa..

(4)Usiwajibu kwa ukali
[emoji117] inawezekana umengua kitu,ambacho sio kizuri,usiwakalipie,usifoke ovyooo,hata Ni kosa ongea kwa utulivu,Jifunze kutuliza hasira yako,mfano unakuta binti yako au kijana ameeanza mahusiano ya kimapenzi,so wewe unatakiwa umwambie madhara ya kufanya sex kabla ya wakati,ataelewa zaidi kuliko kumpiga...ongea na kwa upole.

(5)Watoe watoto wako outing[emoji1787]
[emoji117]
Kipindi hata sikumoja watoe watoto wako mahali wakatembeee,wacheze wafurahi,wale chakula pia nje ya nyumbani itakuwa furaha sanaa kwao.

(6)Hakikisha wanashiriki kazi za nyumbani
[emoji117] Kweli watoto walikuwa shule Sasa wamerudi,basi sio vibaya wakishiriki kazi za nyumbani ikiwa ni kupika,kuosha vyombo,kupanga sebule, vyumba vyao kuwa safi,kuosha vyombo nk wasimuachie dada wa kazi, kumbuka huu muda ndio mzuri wao kujifunza,usiwaache .

(7) Kuwa Makini kwa wanachoaangalia
[emoji117]Kweli likizo watakuwa na muda wa kuangalia sanaa tv,Ila kuwa Makini na carton,move nk wanazoangalia,zingine hazina maadili mazuri,jilizishe kwa kile wanachoaangalia.

(8)Watembelee ndugu,jamaa na marafiki
[emoji117] kipindi hiki Kama muda upo wapeleke wasalimie ndugu,Kuna familia watoto hawajui kabisa ndugu zao,hii hatari sababu hao watoto ujue wanakua na watakuwa na tabia ya kutowatembelea ndugu Wala kuwajali.

(9)Angalia mabegi yao,kabati zao.
[emoji117]Kama mzazi lazima mtoto anaporudi uangalie vizuri bag ambalo amerudi nalo,je amerudi na vitu vyake,? Wengine wanaanza tabia ya wizi au kuazimana anarudi na vitu sio vyake,Ila ktk kupekua bag Kuna vitu unaweza Kukutana navyo pia,Kuna watoto ambao wameaanza mahusiano utawakuta na vidonge vya majira, condoms nk so check up muhimu sanaa.

(10)Wahimize ibada
[emoji117]Ibada muhimu sanaa , hakikisha unaomba nao,pia kila mmoja mwambie akuandikie kwenye karatasi ombi ambalo anataka Mungu amtendeee nk omba nao wafundishe neno la Mungu nk wekeza vitu vyema kwa watoto wako...

#Watoto wetu furaha yetu
#uzao wetu mzuri
#Malezi sahihi ya watoto
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] nimejikuta nacheka nikikumbuka jinsi vile dingi alikuwa mtemi na mkorofi.. Akiletewa shitaka lolote kukuhusu kwanza ni kibano halafu ithibati baadae...hata ikithibitika huna makosa atatafuta justification ya kukuadhibu
 
Yaani kila kitu ni mikwaju tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…