Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Chautundu
JamiiForums-1804317514.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamkumbuka huyu mtoto? Mwaka 2015 aliokotwa Abuja Nigeria akiwa na utapiamlo mkali. Wazazi wake walimtupa wakihisi wamezaa jini.

Raia mmoja wa Norway Anja Ringgren Lovén alimuokota, akamuogesha na kumpeleka hospitali. Akapata matibabu kisha akarudi kuishi nae. Akamlisha vyakula vyenye virutubisho ili kuondokana na utapiamlo mkali aliokua nao.

Mwaka 2017 katika ukurasa wake wa Facebok Anja aliandika maneno haya (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);

"Siku ile nilipomuona huyu Malalika aliyetelekezwa niliumia sana. Nilipombeba ktk viganja vyangu nilijua kabisa HATAPONA. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilipoteza matumaini ya uhai kwa mtu niliyeamua kumsaidia.

Alisimama kwa shida, alipumua kwa shida, alikula kwa shida. Hata alipolia sauti ilitoka kwa shida. Kila kitu kwake kilikua shida. Kwahiyo nilijua atakufa. Lakini sikutaka afe kama mnyama. Sikutaka afe bila utu. Sikutaka afe bila jina.

Nikaamua kumpa jina. Nikamuita HOPE. Neno Hope kwangu ni la pekee. Miaka mingi iliyopita nilichora "tatoo" yenye neno HOPE mikononi. Sijaifuta hadi leo. HOPE kwangu inamaanisha;
H- Help
O- One
P- Person
E- Everyday

Kwa muujiza wa Mungu Hope alipona. Picha ya kwanza kushoto ni wakati ameokotwa. Inayofuata ni 2017 akiwa ameanza shule. Picha ya 3 kushoto ni mwaka 2018, Anja alipost kuonesha maendeleo ya Hope tangu alipookotwa hadi wakati huo. Na picha ya mwisho kulia ni December 2020 Hope akiwa nyumbani kwa Anja anapolelewa.

JamiiForums583680564.jpg
 
Back
Top Bottom