Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Screenshot_20211226-201514.jpg
 
BABU WADAIWA KUBAKA MJUKUU KWA ZAMU,

Na Serengeti Media Centre

Serengeti.Tembea uone mengi ndivyo unaweza kusema kuhusiana na tukio la Babu wawili katika Kijiji cha Nattambiso Wilaya ya Serengeti kukamatwa kwa tuhuma za kubaka mjukuu wa miaka 12 kwa zamu kwa madai ya tamaa ya ngono.

Watuhumiwa hao Hamisi Maganga(50) ambaye ameoa shangazi wa mama wa mtoto na Magembe Magangira (47)mme wa bibi wa mtoto huyo kabla ya kumbaka walimfunga kitambaa usoni,wakamwekea kitambaa mdomoni asipige kelele na kumlaza sakafuni wakati wanamwingilia wanadaiwa kumtishia kumuua iwapo angesema kwa bibi yake ambaye alikuwa safari.

Hata hivyo baada ya kumwingilia kwa zamu(mande)alichanika sehemu yake ya siri na kuvuja damu nyingi na alisaidiwa na majirani ambao walimkimbiza Kituo cha Afya cha Natta na kuongezewa chupa mbili za damu,kushonwa sehemu zake za siri na kupata matibabu mengine.

Kamanda Longinus Tibishubwamu aliliambia Serengeti Media Centre kuwa tukio hilo limetokea Desemba 18 majira ya usiku katika kitongoji cha Majengo nyumbani kwa Dorika Kambarage bibi wa mtoto.

"Chanzo ni ulevi wa kupindukia na tamaa ya ngono,lakini kubwa ni ukosefu wa maadili maana huyo mtoto ni mdogo wa darasa la nne,wamemwingilia huku wamemwekea kitambaa mdomoni, tunaendelea na uchunguzi ili waweze kufikishwa mahakamani,"amesema.

Kwa mjibu ya mtoto huyo kabla ya kufanyiwa unyama huo walikuwa sebuleni wakiangalia picha baadae alienda kulala na kumwacha Maganga ambaye anaishi nyumba nyingine akiwa sebuleni wakati Magembe ambaye anaishi na bibi yake kama mme hakuwepo.

"Mle ndani tulikuwa na mdogo wangu wa miaka 9 bibi alikuwa ameenda kijiji cha Mugeta,nikiwa nimelala aliingia Maganga akazima taa akachota maji ya kunywa,ghafla akanikaba na kunifunika akanishuka chini na kuniwekea vitambaa mdomoni,akanitishia nikipiga kelele ananiua,akaanza kuniingilia kwa nguvu,nilisikia maumivu makali lakini sikuwa na Utetezi,"amesema na kuongeza,

"Baadae akaingia babu Magembe naye akanitishia kuwa nikicheza atanikata kata na kuniua kisha ataondoka,naye akaniingilia kisha wakatoka na kuniacha nimefungwa kitambaa,nikajitahidi kukitoa lakini sikuweza kusimama,maana damu zikawa zinavuja sana,maumivu makali ya mwili,nililala mpaka asubuhi,"amesema.

Hata hivyo anadai asubuhi Maganga alimpelekea dawa za maumivu wakati huo akiwa anatokwa damu mabonge mabonge.

Dorika Kambarage bibi wa mtoto huyo anadai desemba 18 alipigiwa simu na Magembe kuwa mtoto anaumwa anatoka damu sehemu za siri.

"Nilistuka maana hajavunja ungo ilikuwaje ,nikamuuliza amekuwaje hakuwa tayari kunieleza,nikamwambia achukue pedi yangu moja ndani ya sanduku ampe avae ,kabla sijakaa nikapigiwa simu na jirani yangu na kunieleza mtoto kabakwa na kuumizwa.sana na kuwa amelazwa katika Kituo cha Afya cha Natta,nikapanda gari kweli niliyoyaona yalinishangaza sana,"amesema.

Amesema, mtoto alimsimulia alivyotendewa na wote wawili,alishangazwa na tabia hiyo na kuwa suala hilo wanaliachia vyombo vya dola wao wanahangaika na tiba ya mtoto.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Natta Dk Baraka Baraka amesema,"aliletwa akiwa katika hali mbaya ikabidi aongezewe damu chupa mbili,tukamshona maana alichanwachanwa sehemu za siri,tumechukua vipimo mbalimbali ,amekaa hapa siku tano hivi ametoka lakini anaendelea na dawa,"amesema.

Happiness Robert mama mzazi wa mtoto amesema baada ya kutoka Kituo cha Afya waliamua kukaa kwa mjomba wao hawakwenda kwao alikofanyiwa unyama huku akiendelea na dawa.

"Mimi naishi Mwanza na mwanangu anaishi kijiji cha Mugeta alikuja likizo kwa bibi yake ambaye ni mama yangu anayeishi na huyo Magembe baada ya baba kufariki
 
Back
Top Bottom