Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

Spesheli ya watoto tu. Hasi na chanya

20221015_145702.jpg
 
MAMA NA MWANA

Mbawala : shikamoo Mama, nimefukuzwa shuleni.

Mama : marhaba mwanangu Mbawala, hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzi kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.

Mbawala : Sawa mama naomba na pesa ya matumizi, nitashukuru.

Mama: Sawa mwanangu.

Mbawala: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili.

Mama : Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za palizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo.

ukafika muda wa kwenda chuo.

Mbawala : Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo nimekosa sijui nifanye nini mama.

Mama : Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje ??, nipo tayari kujaza madeni usome.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nzuri.

Mama : Mbawala siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini ??, hata simu haunipigii mwanangu !!!.

Mbawala : Yaani mama majukumu ya kazi yamekuwa mengi huwezi kuamini, juzi nilikuwa Zanzibar hivi ndiyo nimerudi majuzi hapa Dar, utanisamehe tu mama'ngu.

Mama : Kwani huko Zanzibar kuna mitandao tofauti na ya huku ??

Mbawala : Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.

Mama : Mdogo wako amefukuzwa shule kwa ajili ya ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda lakini wamemfukuza tena.

Mbawala : Mama hivi bado unatengeneza pombe ??, hivi BIBLIA inasema nini kuhusu pombe Mama, Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.

Mama : Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, na kunituma pesa kidogo za matumizi ningekuwa nimeacha.

Mbawala : Ningekutumia mama'ngu ila sasa hivi ninakimbizana na ujenzi,
hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya,
nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata,
nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.

Siku nyingine ikafuata

Mama : mwanangu nataka nije huko mjini kumsalimia mjukuu wangu mwezi huu.

Mbawala : daaahhh, yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama, mjukuu wako kwa mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.
daaahhh, na bahati mbaya zaidi likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa UINGEREZA kusherehekea birthday ya mtoto wetu, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto ???

niambie tupo akina Mbawala wangapi leo hii..?

JE, HATA KWENYE GROUP HILI PIA WAPO ??.

[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Nurdin Abdallah

Shahidi namba moja ambaye ni mtoto wa miaka 6 anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi Mchungaji Nurdin Abdallah (54) na Muinjilisti wa kanisa la waadventista wasabato Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza, amekiri mbele ya Mahakama kufanyiwa kitendo hicho kwa nyakati tofauti na baba yake huyo.

Kesi hiyo ya ubakaji namba 79 ya mwaka 2022, ilifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 12, mwaka huu.

Leo Oktoba 19, 2022 kulikuwa na mashahidi watatu waliotoa ushahidi Mahakamani hapo akiwemo mtoto ambaye ndiye mwathirika.

Imeelezwa kuwa chanzo cha kubaini tukio hilo kuna mwanachama mmoja wa Ustawi wa Jamii alipata taarifa kutoka kwa majirani, wakamtafuta mtoto ambaye alieleza anayofanyiwa na baba yake.

Mtoto akapelekwa Polisi, daktari akaeleza jinsi sehemu za siri za mtoto zilivyotanuka, ndipo taratibu za Mahakamani zikaanza.

Akiwa Mahakamani mtoto alieleza kuwa baba yake amekuwa akimfanyia vitendo hivyo usiku huku akioneshea sehemu zake za siri kwa kutumia mkono wake.

Alipoulizwa kuhusu mama yake alipo akasema hajui alipo kwa kuwa aliondoka.

Baada ya maelezo hayo, hakimu akampa nafasi baba mtu kumuuliza mtoto, kwanza akaulizwa kama anamtambua, akakiri kuwa huyo ni mwanaye kabisa wa kumzaa.

Mtuhumiwa akaanza kumuuliza maswali mtoto, akamuuliza kama kuna watu ambao wamemtuma aje azungumze hayo Mahakamani, mtoto akasema: "Hakuna aliyenituma nisema haya."

Baba mtu: Kwa hiyo wewe unasema uongo?
Mtoto: Hapana sisemi uongo kwa kuwa kanisani tuliambiwa ukisema uwongo unaenda motoni, mimi naogopa kwenda"

Baba: Unasema mimi nimekubaka, kweli wewe unajua kubaka
Mtoto: Ndio wewe ulinibaka, ulikuwa ukiniingizia dude lako huku (akionesha kwa mkono sehemu za siri)

Baba: Kwahiyo hautaki kuja nyumbani?
Mtoto: Ndio sitaki kwa kuwa wewe utanibaka

Baba: Unataka kuishi wapi?
Mtoto: Nataka kuishi na mama James (ni katika kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu) au mama

Mchungaji huyo alikuwa ni muumini wa Dini ya Kiislam, alibadili dini na kuanza kuhamia katika Ukristo lakini hakubadili dini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4, 2022 na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: EATV

Pia Soma: Mchungaji Nurdin Abdallah afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa miaka 6
JamiiForums-541549773.jpg
 
Watoto Rehema Masanga wa miaka 7 na Amos Masanga mwenye miaka 5 wamekutwa wakiwa wamekumbatiana baada kushindwa kujiokoa kutokana na kufungiwa ndani na mama yao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mafifi, Rabi Mgata amesema chanzo cha moto ni mshumaa ulioshika Godoro na kuunguza nyumba wakati mama wa watoto akidaiwa kwenda kunywa Pombe.

Kamanda wa Zimamoto Isabela Bwago amesema “Ni uzembe wa mzazi aliyendoka akiwa amewafungia watoto wake. Taarifa ya moto tulipewa kwa kuchelewa na hata ingekuja mapema gari isingeweza kufika eneo la tukio kulingana na miundombinu mibovu,”.
 
MAMA NA MWANA

Mbawala :
shikamoo Mama, nimefukuzwa shuleni.

Mama : marhaba mwanangu Mbawala, hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzi kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.

Mbawala : Sawa mama naomba na pesa ya matumizi, nitashukuru.

Mama: Sawa mwanangu.

Mbawala: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili.

Mama : Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za palizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo.

ukafika muda wa kwenda chuo.

Mbawala :
Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo nimekosa sijui nifanye nini mama.

Mama : Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje ??, nipo tayari kujaza madeni usome.

Baada ya kumaliza chuo na kupata kazi nzuri.

Mama :
Mbawala siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini ??, hata simu haunipigii mwanangu !!!.

Mbawala : Yaani mama majukumu ya kazi yamekuwa mengi huwezi kuamini, juzi nilikuwa Zanzibar hivi ndiyo nimerudi majuzi hapa Dar, utanisamehe tu mama'ngu.

Mama : Kwani huko Zanzibar kuna mitandao tofauti na ya huku ??

Mbawala : Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.

Mama : Mdogo wako amefukuzwa shule kwa ajili ya ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda lakini wamemfukuza tena.

Mbawala : Mama hivi bado unatengeneza pombe ??, hivi BIBLIA inasema nini kuhusu pombe Mama, Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.

Mama : Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, na kunituma pesa kidogo za matumizi ningekuwa nimeacha.

Mbawala : Ningekutumia mama'ngu ila sasa hivi ninakimbizana na ujenzi,
hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya,
nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata,
nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.

Siku nyingine ikafuata

Mama :
mwanangu nataka nije huko mjini kumsalimia mjukuu wangu mwezi huu.

Mbawala : daaahhh, yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama, mjukuu wako kwa mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.
daaahhh, na bahati mbaya zaidi likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa UINGEREZA kusherehekea birthday ya mtoto wetu, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto ???

niambie tupo akina Mbawala wangapi leo hii..?

JE, HATA KWENYE GROUP HILI PIA WAPO ??.

[emoji24][emoji24][emoji24]
Dah! Hii niliiona sehemu lakini imetofautiana nukta ndogo sana...

MAMA NA MWANA

Gozbert : Mama wamenifukuza shule.

Mama : Hivi ndo nimetoka kijiji cha Mkomanzila kwa rafiki yangu kuchukua pipa nikoroge pombe, nikiuza nitakutumia mwanangu, kazana kusoma.

Gozbert : Sawa mama naomba na pesa ya Matumizi, nitashukuru.

Mama: Sawa Mwanangu.

Gozbert: Mama shikamoo, nashukuru nilipata ile pesa naomba nisaidie na pesa ya mtihani mama tumeanza usajili

Mama : Mwanangu sina hela kwa sasa jana tumelalia uji na wadogo zako, Nitajitahidi niende kwa Mzee Mwaka nikakope pesa za Parizi nitaenda kupalilia shamba kwa wiki nzima, Jitahidi usome mwanagu nakuombea, akamaliza chuo ukafika muda wa kwenda chuo.

Gozbert : Mama sina pesa kabisa, nimeomba mkopo mama nimekosa sijui nifanye nini mama.

Mama : Mwanangu kama nimekusomesha kote huko chuo nitashindwaje? Nipo tayari kujaza madeni usome.

Baada ya kusoma na kupata kazi nzuri.

Mama : Gozbert siku hizi haunikumbuki mwanangu shida nini? Hata simu mwanangu!

Gozbert : Yaani mama majukumu ya kazi huwezi amini juzi nilikuwa Zanzibar ndo nimerudi majuzi hapa Dar, tanisamehe mama.

Mama : Kwani Zanzibar kuna mitandao tofauti nay! huku?

Gozbert : Hapana, halafu mkwe wako mjamzito kwa hiyo muda mwingi nakuwa na mhudumia naporudi nyumbani.

Mama : Mdogo wako amefukuzwa shule ada inasumbua, nilichukua pesa kidogo niliyouza pombe nikampa wameenda kumfukuza tena.

Gozbert : Mama hivi bado unatengeneza pombe? Hivi biblia inasema nini kuhusu pombe Mama? Hapana Mama hapo unanikwaza kwa kweli.

Mama : Mwanangu kumbuka nimekusomesha kwa kuuza pombe na laiti ungenipunguzia mzigo huu wa kusomesha, kwa kutuma pesa ningekuwa nimeacha.

Gozbert : Ningekutumia sasa hivi nakimbizana na ujenzi mama, hata nikikuahidi sasa hivi nitakudanganya, nilichukua mkopo benki kwa hiyo wananikata, nitakupigia baadae kuna simu inaita hapa.

Siku nyingine ikafuata

Mama : Nataka nije nimsalimie mjukuu wangu mwezi huu.

Gozbert : daah yaani kwa sasa hatuna pesa kabisa mama mjukuu mwezi mmoja tu zimenitoka kama Milioni mbili.

Gozbert : Daah bahati mbaya likizo hii mimi na mke wangu tutakuwa uingereza kusherehekea birthday ya mtoto huko, tukirudi tutafanya utaratibu uje kutusalimia.

Tunakwama wapi watoto wa walala hoi???

Wee! niambie tuna akina Gozbert wangapi leo hii..?
JE,HATA KWENYE GROUP HILI PIA WAPO?

Samahani Admins Ni kukumbushana tu kuwakumbuka wazazi wetu na walezi wetu

"Copy and paste"

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom