Mwanafunzi wa darasa la Saba Shule ya msingi Lukobe Manispaa ya Morogoro mwenye umri wa miaka 16 anayefahamika Kwa jina la Stephen Robert amejinyonga hadi kufa Kwa kutumia kamba ya chandarua chumba kwake
Akizungunza baada ya kutokea tukio hilo baba mzazi wa Mtoto huyo anasema siku ya tukio February 21 alibaki nyumbani akidai anasumbuliwa na kichwa lakin ilipofika majira ya saa tisa alasiri akajinyonga
Anasema baada ya Muda walipoingia ndani wakakuta tayari ameshafariki baada ya kukosa msaada jambo ambalo limewasikitisha wazazi hao
Kamanda wa Polisi mkoa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea Kwa tukio Hilo ambapo amesema chanzo Cha tukio hilo Mtoto huyo alisemwa na wazazi wake kuwa abadili mwendendo wa maisha yake kuwa na tabia nzuri na Kuhudhuria masomo shuleni jambo ambalo likamkera kisha kuingia ndani na kujinyonga
RPC Mkama amewataka watoto kufika katika Kituo cha polisi dawati la jinsia au kwa viongozi wa mtaa ili waeleze changamoto zao badala ya kuchukua maamuzi magumu ya kujiua
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.