Spesho kwa ............. wa JF.

Spesho kwa ............. wa JF.

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,788
Reaction score
2,690
Leo ndama kakata kamba, aruka huku na kule. Sitaki wakunifunga, acheni niruke ruke. Siku nilipokuona nilihisi nimelogwa, uchizi ulinipanda nurusa nikate moto. Kitu gani ulikifanya nabaki najiuliza. Hivi wewe ni nani wa kurusha jiwe moyoni mwangu??

Nyuzi zako humu ndani siachi kufwatilia, mimacho nikiitoa tadhani daktari wa meno. Sijui umeniloga nahitaji lako jibu, maswali yamenishinda njoo Pm unijibu.

Lugha yako ya malikia kidogo yanitisha, tajikaza Kijamaa sabuni iliyobora, Achana na Elizabeth wa Yuropa aharibu usemi wako.

Kukupenda ni Faradhi, sioni tabu kusema, Achana na akina Bitozi, Stunter, na Nyani Ngabu. Wao maneno kwao matupu vitendo hawavijui. Wajua kucheza Kisingeli, Bongofleva na Umarekani mwingi. Takuaribia yako malengo wao kubaki kukucheka.

Njoo nikupe yako ndizi, tunda lisilo ajizi, mbegu zake zizondani, ndogo zafaa kwa kumeza, kumung'unya sitakukataza, ukipenda na lake ganda. Ndizi yako ya Mshale kuchoma wajichoma mwenyewe.

Sio wale wa vibamia, ukijani uliokisiri, ndizi yako ya manjano tameza kwa haja yako, kibamia chao chadea dea tafikiri mlenda wa Giningi. Mwisho chaota miiba kikikomazwa na jua, Wangu achana na Vibamia.

Kaburi nenda kachimbe kwako nimeshakufa, rambi rambi ukusanye mahaba yako yameniua. Sitochoka kufukiwa na mchanaga wa mapenzi unipayo.

Kamwone Mzizimkavu, Mshana Jr usimsahau, wakupe lako limbwata uje unifanye Boya, nizunguke bahari ya penzi lako nipate upepo mwanana.

Usiwe kama Miss Chagga, apendaye Mti pesa, Jua wako niko taabani ya Jpm yamenichosha. Kina Lizaboni hujifanya hawayaoni, Motochini kugugumia moyoni, Mpenzi wangu nakuambia Subira kitu muhimu.

Kwa MaNabii nilienda, Nipate nguvu ya upako, Bulldozer, na mlima wa moto kumbe yote ni Kaole. Mpenzi Wang nivumilie Kwako siwezi kufa Ganzi.

Mapenzi kitu muhimu, nani asiyejua.
Yafaa kuenziwa, kwa heshima na hekima.
Wakikupa samaki uwakubalie basi mimi ntakupa Nyavu univulie.

kukutaja naogopa, humu ndani fitina nyingi. Wasijeota ndoto za Lema, kukatisha wetu uhai. Kukupenda nakupenda kidani cha moyo Wang.

Upinde ulisimama katika mtima Wang, rangi nzuri ulizoonyesha nikabaki mdomo wazi. Sauti tamu ya marejeo Malaika waona mfano. Njoo Pm tuyajenge.

Njoo Pm Mpenzi, wajua nataabika. Avatar yako nikiiona, pumzi yaniisha kama mgonjwa wa Pumu. Usifanye hinda Mtoto wewe, Mwezio sio Roboti. Ninao moyo wa Nyama, Maumivu nasikia.

Cheko lako la uchokozi, lanigeuza Mwendawazimu. Umbo lako la Magazijuto, Lagawanya na kutoa. hakika umejaliwa, Mtoto wa Kiafrika.

Namaliza kwa faraja, yamajibu matamu kama Kokoa. Tafadhali mpenzi wangu, jibu lako pumzi yangu, usije geuka mtoa roho unijibu mang'amu ng'amu. Takufa nimeachama nikilitaja jina lako.


Karibuni!!
 
Duuuu malizia hasira zako tu humu maana ajiri ndohu
 
We mwanamke plz pitia hapa nikuimbie hii vesi.!!
 
Back
Top Bottom