Keki ya kawaida tu,mana kila nikipika inakua kama ugali halafu inaungua sa sijui nakosea nini!
Keki
Vipimo
1)Mayai 6
2)Sukari robo punguza kdg
3)Unga vijiko 12 vya kulia vijae vizuri
4)Baking powder 1 teaspoon
5)Siagi robo punguza kidogo ili kupunguza mafuta
6)Arki (essence) upendayo mfano vanilla ama banana
Namna ya kutaarisha
1)Mimina katika bakuli safi siagi pamoja na sukari...changanya vizuri kwa handmixer hadi iwe laini na sukari kusagika
2)Vunja mayai then changanya katika mchanganyoko wa sukari na siagi..changanya kwa handmixer
3)Katika bakuli jengine changanya unga na baking powder vizur
4)Weka unga katika mchanganyiko wa mayai na changanya vizuri....usisage sana
5)Mimina kwenye trey...moto wa kupikia keki kwa oven ni 300F-350
6)Subiria hadi iwive vizuri hadi kuwa rangi ya brown.
Hapa nakupa trick ya jinsi ya kutizama keki kama imewiva katikati au la
Chukua toothpick safi wakati unapika keki yako kutaka kujua kama kati imewiva au la ichome kijiti then kishike kijiti kikiwa wet maanake bado haijawiva kikitoka kikavu tayari imewiva....
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums