Spidi ya wakinga kwenye biashara inatisha, tuna lipi la kujifunza?

Hii mada ni ya ajabu - mbona hushangai kwanini wachagga wanafanya vizuri kwenye biashara, je nao wanatumia waganga? Hii inaweza kutumika kuchafua au kubeza mafanikio ya watu wanaojituma sana kufanya kazi na kujiwekea akiba ili wafanikiwe.
 
Hii mada ni ya ajabu - mbona hushangai kwanini wachagga wanafanya vizuri kwenye biashara, je nao wanatumia waganga? Hii inaweza kutumika kuchafua au kubeza mafanikio ya watu wanaojituma sana kufanya kazi na kujiwekea akiba ili wafanikiwe.
Hilo kundi ulilolitaja limeshapinduliwa hapo kariakoo, ukifika kariako sikuhizi wakinga wamejaa mno, Usianze kuibua vitu ambavyo havuhusiani na maada, wapi nimeandika kuhusu kutumia uganga?? nilichoandika ni kwamba watu wengi wanawatuhumu kutumia uganga, hivyo na wenyewe watumie huo uganga watoboe
 
Hata Hawa kina mangi
 
Wapare wengi ni bahili lakini hawana biashara, hapo ndipo penye utofauti
Utajiri wa masharti huo sio utajiri ni laana tu.
Yaani pesa ninayo lakini naogopa kula na kuvaa vizuri kisa nitafilisika huo ni upumbavu.
Mtu anayeonea ubahili hata tumbo lake anaweza kumsaidia maskini mwenye njaa kweli?
Kwangu mimi utajiri ni kua na uwezo wa kuihudumia familia yangu vizuri (kukidhi mahitaji yooote ya familia) pamoja na kuwasaidia watu wangu wa karibu ndugu, jamaa, marafiki na wote wasiojiweza wanaonizunguka katika jamii.
Mambo ya kufungia mabilioni ya pesa bank huku kuna watu walionizunguka wanakufa kwa njaa au wanapoteza maisha kwa kukosa huduma ya matibabu huo kwangu sio utajiri ni ufahari usio na faida yoyote kwangu.
 
Utajiri wa masharti huo sio utajiri ni laana tu.
hata wanyakyusa wa mbeya, wafipa wa rukwa, waha wa kigoma, wahaya wa kagera, wasukuma wa mwanza, wakurya wa mara, wapare wa kilimanjaro, wasambaa wa tanga, wazaramo wa dar, wamakonde wa mtwara, wangoni wa ruvuma, wahehe wa iringa, n.k wapo wanaoenda kwa waganga lakini haimaanishi ni wote, sio kwenye biashara tu bali hata makazini na maisha ya kawaida.
Yaani pesa ninayo lakini naogopa kula na kuvaa vizuri kisa nitafilisika huo ni upumbavu.
Sawa mkuu


Mtu anayeonea ubahili hata tumbo lake anaweza kumsaidia maskini mwenye njaa kweli?
Mkuu hawa jamaa wanasaidiana vizuri tu, Nenda pale kariakoo ujionee, wameikamata kariakoo kisawa sawa na hii ni kwa kusaidiana
Kwangu mimi utajiri ni kua na uwezo wa kuihudumia familia yangu vizuri (kukidhi mahitaji yooote ya familia)
Wenzako wanawaza mbali zaidi ya hapo, saizi wana kampuni hhadi za kusafirisha mizigo kutoka china
pamoja na kuwasaidia watu wangu wa karibu ndugu, jamaa, marafiki na wote wasiojiweza wanaonizunguka katika jamii.
Inapendeza lakini kwa makabila mengi ya Tanzania hayapendi kusaidiana ndio maana hayaendelei
Mambo ya kufungia mabilioni ya pesa bank
Fikisha kwanza hayo mabilioni, ndio uongelee mabilioni,

hio pesa uliyonunulia bando ingependeza uwanunulie chakula wasiojiweza.
 

[emoji28]
 
Watu wanaotokea mkoa wa njombe usiwa underestimate kabisa ki intelligence wako vizuri sana

Ukisikia mtu anatoka njombe fatilia hata rekodi zake za darasani utakuta yuko smart sana .

Tatizo wako humble saa hawana makelele Kama wale wengine wa kule

Biashara zinawatoa sana

Japo wapo wazee wa ndagu je huko kwengine hawako!?
 

mkoa wa njombe kuna makabila y wahehe, wabena na wakinga.......Wainga wengi wapo wilaya ya Makete

Kiukweli kwenye elimu bado wapo chini sana kwa sababu miundo mbinu ya elimu ipo cini sana huko makete, shule ni chache sana , hali ya hewa so nzuri kuna baridi kali sana na mwamko wa elimu ni mdogo wengi wanakimbilia biashara au kilimo
 
Ni kweli unachosema ila tatizo wanakumbwa mno na vifo vya utatanishi wakiwa wadogo na miaka michache tu baada ya kupata utajiri. Ukienda Njombe na Makambako kuna wajane hadi utasikitika
Mkoa na wilaya yao inaongoza kwa maambukizi ya UKIMWI.
 
i kweli unachosema ila tatizo wanakumbwa mno na vifo vya utatanishi wakiwa wadogo na miaka michache tu baada ya kupata utajiri.
Tatizo huishi na wakinga, unasikiliza stori zao vijiweni.

Mimi nipo Mbeya huku nawajua wakinga wengi tu wazee wenye biashara zao.

Kuna utofauti wa mkinga anaezungumziwa vijiweni na mkinga wa kwenye uhalisia
 
Kwa hiyo wewe nawe ni great thinker🤣
Ok twende hivyo hivyo bwana great thinker, nilichoomanisha mimi si viazi, isipokuwa viazi ni mfano tu wa kuwa,, mtu una kila lkn unajidhiki mpaka kula yako, mtu una kila kitu mpaka magari pia unayo lkn hapo hapo unapanda daladala na haya mambo pia yapo na tunajionea,,, na hasa wale wanaojiita magreat thinkers wengi wachawi tu,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…