Spidi ya wakinga kwenye biashara inatisha, tuna lipi la kujifunza?

Spidi ya wakinga kwenye biashara inatisha, tuna lipi la kujifunza?

Kwa hiyo wewe nawe ni great thinker🤣
Ok twende hivyo hivyo bwana great thinker, nilichoomanisha mimi si viazi, isipokuwa viazi ni mfano tu wa kuwa,, mtu una kila lkn unajidhiki mpaka kula yako, mtu una kila kitu mpaka magari pia unayo lkn hapo hapo unapanda daladala na haya mambo pia yapo na tunajionea,,, na hasa wale wanaojiita magreat thinkers wengi wachawi tu,,,
vunja bei anapanda dala dala zipi??

tatizo lako unafanya generalization
 
vunja bei anapanda dala dala zipi??

tatizo lako unafanya generalization
Haaa haa haa bwana great thinker unaniangusha
Wapi nimesema vunja bei anapanda daladala?
tunavyosema wachaga matapeli hatuna maana basi kila mchaga ni tapeli
 
Gussie Mkinga Nipo hapa,

Kama una swali karibu sana sana, Wale wazee wa kununua Fuzo karibuni sana

Wale wote wanaoona biashara rahisi nawapongeza sana

Kwa sisi wakinga tatizo sio mtaji ni kiasi gani? Tatizo ni matumizi na mipango

Mipango.

Kuwa mwana ccm kama mimi ni maamuzi magumu sana kuliko kuuza Pipi
Naomba km una dadako aniambukize upako atakuwa mtunza fedha sitamlimisha yaani yeye kuwa mkinga tu inatosha kumlipa!! alafu Doni Mtwara MATC wee unamjua kweli? Yule jamaaa ana mjighorofa 30 KWENDA JUU!!! mkewe mwalimu alimuacha sijui mwanae neema yuko wapi yule dogo
 
Kina mangi wa miaka ya zamani naona walikuwa moto sana kwenye biashara kuliko hawa wa siku hizi, sijui ni mimi tu naliona hili??
Ushindani umekuwa mkubwa.Miaka ya 90's niliona wachaga tu wakibeba mavyombo na kutembeza leo kila kabila wamekuwa machinga.
Huko shinyanga nilipokulia maduka yalikuwa ya wachaga baadae wakajaa waha wakamtoa mchaga kwenye leri kisa mchaga hakutaka kupunguza bei ya vitu, bucha nyingi zilikuwa za wachaga, waha hawakuweza biashara ya bucha bali walijaa masokoni kuuza mahitaji mchaga akapisha taratibu.
Sijui miaka ya sasa kuna mabadiriko gani ya kibiashara ila hivyo ndivyo mchaga alipata upinzani kanda ya ziwa.
 
mkoa wa njombe kuna makabila y wahehe, wabena na wakinga.......Wainga wengi wapo wilaya ya Makete

Kiukweli kwenye elimu bado wapo chini sana kwa sababu miundo mbinu ya elimu ipo cini sana huko makete, shule ni chache sana , hali ya hewa so nzuri kuna baridi kali sana na mwamko wa elimu ni mdogo wengi wanakimbilia biashara au kilimo
Bora walikimbilia biashara, siku hizi elimu kumtoa mtu ni bahati nasibu.
Waombe mungu mazingira ya elimu yazidi kuwa magumu maana watapotoka na kuwaza mavyeti.
 
Wanabebana Sana pia..Kuna mmoja Yuko pale kariakoo alikuwa mtu wa mwanzo mwanzo kufanya biashara enzio hizo Hakuna wafanya biashara wengi alimake Sana pesa baadae akaja wasupport wadogo zake zaidi ya watano kila mtu duka lake la bidhaa zile zile ,saiv hawakamatiki .wanashikana Sana mkono na wanapeana Sana mizigo ambapo inakuwa rahisi mtu kunyenyuka ...makabila mengine familia moja ushirikiano sifuri kwa Hali hiyo usitegemee kuona impact

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Haaa haa haa bwana great thinker unaniangusha
Wapi nimesema vunja bei anapanda daladala?
tunavyosema wachaga matapeli hatuna maana basi kila mchaga ni tapeli
Wewe huna hoja,acha ubishani wa JF ingia mzigoni ukafanye research hata hapo kariakoo, wakinga wana nidhamu kubwa sana ya matumizi, nidhamu hyo inawafanya waonekane kama wendawazimu au wachawi wanaofuata masharti. Mtu anaweza kua na milioni 700 kwenye account ila hanunui hata chips yai achilia mbali kwenda kiwanja kujirusha.

Hakuna uchawi kwenye pesa, ingekua hivyo sumbawanga na Tanga watu wangekua matajiri, hakuna anayetaka kua masikini, siri kubwa ya pesa ipo kwenye matumizi maana hakuna asiyepata pesa.
 
Hahah wakinga pekee wanaopinga uchawi ni hawa wasomi ila ukija hawa wa kitaa wanakubali hilo!

Naishi Mbeya sehemu yenye wakinga kuliko miji mingi Tz, mbali na nidhamu ye fedha hawa watu utajiri wao ni wa short cut sana!

Naappreciate ni kwamba hawajaacha asili yao, ni watu wa matambiko sana, ukibisha niambie ni kwanini haupiti mwezi/miezi ni lazima wataenda Ukinga.
 
Nilikuwa kanda za ludewa na makete miezi miwili iliyopita, ukweli ni kuwa vijana wanajituma sana.

Kijana mwenyeji wa kule kupanga nyumba ni kitu cha aibu, unakuwa mtu wa ajabu. Itakulazimu ujenge hata kama ni kajumba kadogo.

Kula bata kupindukia au kushinda kijiweni bila kazi nayo ni aibu.

Asilimia kubwa wanamiliki mashamba ya miti au kujihusisha na kilimo cha viazi, vitunguu nk.
Hela inayotafutwa ni rahisi kuihifadhi kwa sababu maisha hayana gharama tofauti na mijini.
 
Hahah wakinga pekee wanaopinga uchawi ni hawa wasomi ila ukija hawa wa kitaa wanakubali hilo!

Naishi Mbeya sehemu yenye wakinga kuliko miji mingi Tz, mbali na nidhamu ye fedha hawa watu utajiri wao ni wa short cut sana!

Naappreciate ni kwamba hawajaacha asili yao, ni watu wa matambiko sana, ukibisha niambie ni kwanini haupiti mwezi/miezi ni lazima wataenda Ukinga.
Hakuna uchawi. Mbeya wakinga wameshika biashara zote. Kuanzia kubwa, za maduka, za mazao na umachinga. Nidhamu ya fedha ndiyo siri.
 
Wewe huna hoja,acha ubishani wa JF ingia mzigoni ukafanye research hata hapo kariakoo, wakinga wana nidhamu kubwa sana ya matumizi, nidhamu hyo inawafanya waonekane kama wendawazimu au wachawi wanaofuata masharti. Mtu anaweza kua na milioni 700 kwenye account ila hanunui hata chips yai achilia mbali kwenda kiwanja kujirusha.

Hakuna uchawi kwenye pesa, ingekua hivyo sumbawanga na Tanga watu wangekua matajiri, hakuna anayetaka kua masikini, siri kubwa ya pesa ipo kwenye matumizi maana hakuna asiyepata pesa.
Sawa nimekubali mie sina hoja,, ila wewe mwenzangu hoja unayo hiyo ya mkinga kuwa na milioni mia saba lkn akashindwa hata kununua chipsi yai,, sasa hizo hela sijui anataka akatumie kaburini!,, kama sio mashart ya mganga
 
Wanabebana Sana pia..Kuna mmoja Yuko pale kariakoo alikuwa mtu wa mwanzo mwanzo kufanya biashara enzio hizo Hakuna wafanya biashara wengi alimake Sana pesa baadae akaja wasupport wadogo zake zaidi ya watano kila mtu duka lake la bidhaa zile zile ,saiv hawakamatiki .wanashikana Sana mkono na wanapeana Sana mizigo ambapo inakuwa rahisi mtu kunyenyuka ...makabila mengine familia moja ushirikiano sifuri kwa Hali hiyo usitegemee kuona impact

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hii ni point, wakinga wanabebana, wanapeana connections na kusaidiana! Na huo ndo mwanzo wa mafanikio, Makabila mengine unakuta ndugu ndio anakudhurumu, au anakuwa yupo tayari kumsaidia mtu baki, lakini sio ndugu yake...tena unakuta msaada wenyewe sio wa kipesa, just connections tuu za kupata mzigo, au kuagiza mzigo.
 
Sawa nimekubali mie sina hoja,, ila wewe mwenzangu hoja unayo hiyo ya mkinga kuwa na milioni mia saba lkn akashindwa hata kununua chipsi yai,, sasa hizo hela sijui anataka akatumie kaburini!,, kama sio mashart ya mganga
Aya sawa, tufanye ni masharti ya mganga kama unavyoamini nipeleke na mimi kwa hao waganga maana utajiri huo wa fasta nahitaji.
 
Back
Top Bottom