Spidi ya wakinga kwenye biashara inatisha, tuna lipi la kujifunza?

Nimeyaamini maneno ya Nyerere kuwa baada ya kuuvunja muungano watanganyika watagundua hakuna kitu kimoja kinachoitwa Tanganyika

Nje ya muungano kuna wahaya,wakinga,wajaluo,wasukuma nk
 
Ndg yangu weee! unasema tu! kwa sababu hujui! nini unasema!! kuvaa kustarehe inategemea na hobby ya mtu ndg yangu weyeee!
Kwa mfano mie tajiri sana!! siwezi kufakamia, Nyama choma, vinono, kutembelea gari masaa 24, mazoezi ni muhimu mnoo!

Mademu, sijui Pombe kwa sana, sababu najua hii itaniletea pressure!!! Kisukari,! Obesenk! nk na matokeo ya haya yoote ni nini??? ... Kifo cha ghafla! ukiona tajiri yuko km wewe atakufa mapema mnoo! utajiri unahitaji nidhamu! umaskini unahitaji nidhamu!

Hayo unayoosema masharti!! basi ni nidhamu ya utajiri!.....hkn cha masharti ya kichawi km ni ivo Mbagalla kote huko wangekuwa matajiri shida zoote zile unadhani wanapenda kuwa hivo??

Na pia jua kuwa mchawi ni ndugu hasa!! au kikulacho ki nguoni mwako!! haya yoote wakinga wanaya jua sasa ogopa sana Mtu ndgu, Yusuf aliuzwa na nduguze, Daudi alitaka kuuawa na mwane Abosalom ili arithi ufalme wa Babae!!

Abel aliuawa na nduguye!! sababu ya wivu tu!! weye ni nani umpe nduguyo, mwanao, jasho lako na akupende daima?

hii yoote ni Mungu katupatia ilimu au funzo tuelewe!! ajabu sasa km huelewi hapa yeye Mungu hayumo tena! atakuacha ufe tu! na mbinguni hupokelewi maana utaangamia kwa kukosa maarifa!

Sawa ni ufahari si Mungu kakupa!! kosa lake ni nini? ujue kwamba hayo unayo yaona eti ni ufahari kuna Tairi mwingine anaona ni u chochoro tu! yaani unahangaika tu! huna kitu! wala si kitu!

Mwingine kumiliki Mbuzi, Punda ving'ombe tu kwake ni ufahari mpaka wana kijiji wanamjalia kwake! wkt huo huo kuna familia wana utajiri wa karne kumi na tano huko nyuma lkn wala hawa tetemeki! tena wakula vyakula vya hovyoooo!

shida kubwa kwao ni uhai kabisaaa! teantajiri hswa hanywi chai! yeye ni uji waulezi tu, na viazi vya kuchemsha, sasa kwa akili zako utasema Bahiri! Kikwete wakt wa sherehe nyumbani kwake watakula vijana. yeye na matajiri ni kunywa maji maji tu!
 
Wewee, tema mate chini! Unatamani biashara na utajiri wa Wakinga? Kama wewe ni mcha Mungu wa ukweli, waombee tu ndugu hawa.
 
Hao wakinga ni wote wana hela au..mana mnakuza mambo watu wenyewe hata buku hawafiki kabila zima.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni kweli unachosema ila tatizo wanakumbwa mno na vifo vya utatanishi wakiwa wadogo na miaka michache tu baada ya kupata utajiri. Ukienda Njombe na Makambako kuna wajane hadi utasikitika
Baelezee! Kwa kifupi ni kwamba, Ni ngumu mno mno kufanya biashara za Bongo ukafanikiwa bila kuhusisha nguvu za giza. Nasema hivyo kwa sababu nimekuwemo humo. Mifumo ya biashara Nchi hii siyo rafiki kwa biashara. Lazima utumie rough. Uloge, uzindike, uibe, udhulumu, ukwepe kodi, utoe rushwa, uuze bidhaa counterfeit, na kadhalika. Ukimwona mtu ni tajiri Nchi hii, mwogope sana. Na umheshimu pia.
Aidha, haya mambo hayatushangazi wakristo tuliookoka; tena tuliookoka kwelikweli. Shetani-ibilisi alimshawishi Bwana Yesu Kristo amsujudie ili ampatie mali na utajiri kwani rasilmali zote za Dunia hii zipo chini ya udhibiti wake, na kuwa humpa yeyote kama apendavyo. Bwana Yesu alikataa ujinga huo. Akina Dangote hawa. Si rahisi. Wengine yalitushinda ya Wakinga. Wewe ingia kwenye biashara hata na mtaji mkubwa namna gani na usiwaone "wazee", utakosana na mke au mume kuwa anakuibia pesa. Mtaji badala ya kukua, Unapungua siku baada ya siku. Waulize wastaafu serikalini. Utasema ni uzoefu wa biashara; Uzoefu?! Dunia hii ina Mambo ndugu. Anyway, nawakumbusha ndugu zangu Wakinga kuwa hapa Duniani tulikuja uchi, na tutaondoka uchi hali kadhalika. Ndugu zangu Wachagga nao wameingizwa kwenye kamchezo ka Wakinga. Nenda Kilimanjaro na utulie, utakutana na story za ajabu za ushirikina. Wanatoana ndagu kwa kwenda mbele. Milango ya wizi serikalini si imedhibitiwa! Ndiyo hivyo.
 
Hongera dada wa kikinga ila wambie nduguzo waache kuwekana mazombi
 
Siri ya ukwasi kwenye shughuli yoyote inatokana na mambo makuu matatu:-

1. Bidii katika kutafuta na kuwekeza pesa(thrifty and investment)

2. Nidhamu katika matumizi ya pesa(frugality).

3. Kuweka akiba(savings)

Huo ndio utamaduni wa pesa ambao makundi makubwa ya watu wenye asili ya kufanya biashara(mf. wahindi) wameujua na kuutekeleza kwa vizazi vingi.

Lakini huu utamaduni sio attribute ya kabila fulani kama ambavyo ujinga unawatuma wengine kufikiria. Mtu yoyote anayeingia kwenye utafutaji akiwa na akili timamu anaweza kufikia kiwango kikubwa cha ukwasi kama akifuata utamaduni huu na mambo mengine kama kuvutia wateja kwenye biashara yake, kushirikiana na wengine katika kuibua mitaji, kufanya biashara sahihi kwenye mazingira na wakati sahihi n. k.

Hapana shaka hao wafanyabiashara wakinga wanaokuja juu wamegundua huu utamaduni wa pesa na wanaufanyia kazi. Mganga anapokuambia usijenge nyumba ya fahari ya kuishi itakayokata mtaji wako, au uvae yeboyebo na sio moccasin anakufundisha kuwa frugal.
Na ni siri iliyopaswa kuwa wazi kuwa sehemu kubwa ya utajiri inatokana na matumizi ya mali kwa nidhamu ya hali ya juu.

Hizo habari nyingine za ushirikina na mazindiko(wahindi huwa wanasemwa sana pia kwa haya) na kwamba kabila la mtu lina uhusiano na business acumen yake ni ujinga tu ambao umekataa kuondoka kwenye vichwa vya waafrika walio wengi na hivyo kuendeleza umasikini.
 
Wakinga Siri yao ya mafanikio ni moja tu, WABAHILI.

HAWAHONGI, HAWAVAI VIZURI, HAWALI VIZURI HADI KIELEWEKE.

kitu ambacho wengi kinatushinda, tukipata faida kidogo tu lazima jamii itufahamu sisi ni nani, ila mkinga unaweza pishana nae kavaa ndala na Rambo yake mkononi ukamchulia poa, kumbe anaenda zake benki kuweka mamilioni ya MAUZO, alitoka hapo anapiga viazi vitamu vya kuchemsha na maji....

Sisi wengine sasa.....sisiiiiiiii.......hehehehe tutazungukwa walinzi kisa kafaida kaduchu tu
 

Huo sio ubahili(misery) bali ni matumizi yenye nidhamu na kipimo(frugality).
 
Unachekesha [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hawa jamaa ni wachapa kazi,wavumilivu,hawana makuu,waaminifu ndio siri ya mafanikio yao
 
Wakinga ndugu zako kama ujuavyo wanapuliza vibaya na utaona tu jinsi wanavyofekana na hawatafika mbali sana.
 
Nime ipenda Spirit ya Wakinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…