Spika aahirisha safari ya Marekani

kwa vile Rais bado ana nafasi mbili za kuteua wabunge, miye naomba hako kanafasi kamoja. Hiyo inaweza kuninyamazisha hapa JF na kunifungulia Bungeni.

Mkjj, wajanja hao wataku-balali au wataku-kolimba kabisa kwanza kabla ya kukupa hiyo nafasi ya kuji-fisadi! Hawawezi kuku-dito kwani itaibua kelele nyingi!
 
Hiyo picha sio muhindi huo bali ni "mjani" fulani...

Masatu unanitibulia bwana.. Hivi majuzi Kamanda Tossi alikuja kijijini kwetu na kukatakata "mahindi" Ati "mahindi yetu ni haramu". Well, tutakula wapi wengine?
 

Mwanakijiji,

Katika haya hizo nilizobold, hakuna hata moja Lowasa analoweza kulifanya kumtishia Kikwete. Kwanza ameshapoteza imani ya Watanzania wengi sana kwani ufisadi wake na mizengwe yake ni kero kwa wanaccm wengi pamoja na wananchi wa kawaida. Pili PM hana ukaribu na wanachama wengi wa kawaida na hasa wenye credibility ambao wanaweza kuwa msaada kwake pindi atakapotoka kwenye u-PM. Lakini kubwa katika yote, kama atawajibishwa na akafungua domo lake "kuichachafya" serikali EL sio Butiku. Watamfilisi kila kitu kufidia hela za mafuriko ya Lindi na Mtwara, Richmond, EPA, Deep Green na Meremeta; ambazo sio tu ameshiriki kwa karibu sana, lakini yeye ni mmoja wa maengeneer wa issue nzima na Kanjibhai wake.
 
This time Lowassa akiacha uwaziri mkuu kwa sababu yoyote itakuwa ndiio mwisho wa his political career, lakini atakachofanya ni kuendelea behind the curtain.
Huyu jamaa ameonesha true colors zake, za kuwa na politics of intimidation, politics of corruption and bribing, deception and mengine mengi tu.
Ni ajabu sana, nasikia wabunge wengine madokta na hata maprofesa wanamuogpa sana huyu jamaa, amekuwa kama ni mwalimu mkuu mkali ambaye hata walimu wenzie wanamuogopa, kwa jinsi anavyofanya fyongo inaonekana hata rais anaogopa kumwajibisha! Sio mtu mzuri kwa nchi yetu
 
Naanza kuwakumbuka wabunge kama Mutungiriheri na Njelu Kasaka kuwa wangetufaa sana kipindi hichi!
 
Kabla ya kuisoma hiyo ripoti naona kumekuwa na kelele nyingi sana, kama walivyosema wengine unaweza kuta KUNA DANGANYA TOTO. Sasa hivi sisiem na serikalini hali ni ngumu, si wakati wa kuanza kutosana, tena kwa mtu ambaye ni mwanasiasa kama PM, itaondoa imani ya wananchi kwa JK, kwamba chaguo lake lilikuwa bomu. Balali maybe was easy, he is not a political partner, hajatafuta popote public trust ili apewe ofisi, by the way si chaguo la awamu hii....
Kulingana na hilo, ninajiuliza maswali mengi sana, acha niyaweke kwenye ubao....
Je kama hiyo kamati imewasafisha EL na wenzake ambao watu wanataka wawaone wakiaibika?? Je kama haitakuwa wazi to implicate anyone, na kuishia na zile story tulizozizoea, mfano kulikuwa na shinikizo kutoka juu but mtu huyo hakujitaja jina etc???

Maswali mengine.....
Kamati ya bunge ina uwezo gani wa kufanya uchunguzi??? Watawezaje kuthibitisha habari ambazo zimejikanganya?? ni walipata access ya watu wote waliohitaji kuwahoji???Je beyond kuhoji watu, wametafuta evidence gani nyingine??
Swali jingine, kama kamati imefanya kazi nzuri kabisa, na tunaowataka waabike hawapo, mfano kiukweli hawajahusika, Je watanzania tuko tayari kuipokea?? usikute watu tushahukumu tayari mioyoni mwetu...
 
Mimi mbona simuoni bwana Sitta ? Anaumwa tena ama ameamua kuondoka Marekani ama vipi ?
 
Mimi mbona simuoni bwana Sitta ? Anaumwa tena ama ameamua kuondoka Marekani ama vipi ?

Kwanini aje bungeni kupoteza muda???si unajua kama ukiwa na pepa vile, halafu unahitaji kuzima moto???!!!!

coz jamaa alitaka wiki ya kujiandaa....amerika ambako asingepata bughudha, jamaa wakamkomalia akabaki, so days zimepungua, n he needs to be prepared kukabiliana na maswali...Ndo kitu nachoshangaa bunge letu, spika badala ya kufacilitate discussions, yeye anadictate discussions.... Bila shaka saivi yuko anaipitia ripoti vizuri na wasanii wengine, trying to brainstorm maswali n the way to dictate the discussions...
Bungeni mtamwona akiwa tayari......asije 'akakurupuka'
 
Masatu unanitibulia bwana.. Hivi majuzi Kamanda Tossi alikuja kijijini kwetu na kukatakata "mahindi" Ati "mahindi yetu ni haramu". Well, tutakula wapi wengine?

I see, kumbe Mzee MwanaKijiji ni rire rimzee tunayeritafuta... kama rikirudi Tanzania tutarikamata pale airport...
 
Kwenye hiyo issue ya RichMond,,, nahisi jambo zito sana... anyway tusubiri likitokea nitawaambia!!!
 
Naanza kuwakumbuka wabunge kama Mutungiriheri na Njelu Kasaka kuwa wangetufaa sana kipindi hichi!

Uko sahihi, ila umechelewa sana, hawa watu hawakuwa na rushwa za kuwapa wanachama wao ndio maana wakapigwa chini.
Machozi ya mamba haya ambayo Wadanganyika tunalia!
 
•
...Spika: Sijashinikizwa kutokwenda Marekani

Na Hassan Abbas

SPIKA wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, amesisitiza kuwa kuahirisha safari yake ya Marekani hakukutokana na shinikizo la uongozi wa juu serikalini, bali alisikiliza kilio cha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana akiwa njiani kurejea Dodoma mara baada ya kuahirisha safari hiyo na kuwa tayari kuanza kuendesha vikao vya Bunge leo, Bw. Sitta pia alikiri kuwa mjadala huo una maslahi ya kitaifa.

"Sijashinikizwa na kiongozi yeyote. Nashangaa wanaohusisha taarifa hizo, watu wanakwenda mbali hadi kumtaja Rais. Haya ni mashambulizi dhidi ya heshima yangu binafsi. Niliposema nakwenda Marekani na kuahirisha kuijadili ripoti hiyo watu walinielewa vibaya, naelewa ni kutokuelewa kanuni tu na watu hawataki kujishughulisha kujua.

"Kwa mujibu wa Kamati ya Uongozi, awali tulipanga mjadala huo uwe mwishoni mwa Bunge, kwa hiyo nikaona naweza kusafiri kwa siku mbili tatu hizi na kurejea kuwahi kuuendesha. Nimeshafafanua kuwa kanuni zinamtaka Spika mwenyewe awepo pindi kunapokuwa na mijadala muhimu bungeni," alisema na kuongeza:

"Safari yangu ya Marekani ilikuwa ya manufaa kwa Bunge. Unajua Bunge hivi sasa lina mfuko maalumu wa kujiendesha. Kule kulikuwa na kikao cha viongozi katika jitihada zetu za kupata nguvu ya kujiendesha. Sasa unapoitwa tena kwa wadhifa wako unapaswa kuheshimu, hii si kumdharau mtu mwingine."

Akizungumzia zaidi sababu za kufikia hatua ya kuamua kubaki nchini, Bw. Sitta aliiambia Majira kuwa alizingatia matakwa ya wabunge.

"Jumapili baada ya wabunge kutoa tamko kwenye semina na kukataa kujadili muswada (wa sheria mpya ya umeme), nilipigiwa simu na kuelezwa hoja hiyo kuwa wengi walikuwa wakitaka kwanza ijadiliwe ripoti ya Richmond.

"Kwa kuona suala hili sasa limeletwa na wawakilishi wa wananchi wakitaka mjadala huu uje mapema kuliko tulivyopanga awali, ndipo nikaona kuna haja ya kubaki kusimamia suala hilo," alisema.

Alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge, yeye si anayeamua na kuidhinisha kila jambo. "Hapa ndipo wengi wanapokosea, watu wanadhani mimi ndiye naweza kukaa tu na kuamua hiki kifanyike ninavyoona, nasimamia kanuni na sheria.

"Ili mjadala wa Richmond ufanyike mapema zaidi, ni lazima Kamati ya Uongozi ambayo mimi ni Mwenyekiti wake, ikae tena na kupitia tena ratiba.

"Hilo ndilo ambalo limenibakiza nchini ili tukutane na kuusogeza mjadala huo ujadiliwe mapema zaidi. Hivi ninavyozungumza na wewe leo (jana) jioni, Kamati ya Uongozi inakutaka kupanga siku ya kuijadili ripoti hiyo. Kila kitu kiko wazi," alisema.

Akizungumzia tuhuma kuwa amekuwa akishiriki katika kile kinachoelezwa kuwa mkakati wa chini kwa chini wa 'kupoteza muda,' juu ya kujadiliwa ripoti hiyo, Spika Sitta alisema:

"Mimi ndiye nilisimamia mjadala wa kuundwa Kamati ya kuichunguza Richmond. Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, ambayo iliipanga ripoti hiyo kujadiliwa kwa mujibu wa kanuni ambazo kwanza zinataka miswada ya Serikali ndiyo ijadiliwe. Ningekuwa na upande, mjadala huo usingefika hata bungeni. Kwa hiyo madai hayo hayaeleweki."
 
hivi haya maneno ya..............mimi.....mimi........mimi and mimi....hivi wewe Sita unataka kutuambia kwa kuwa wewe ni mwenyelketi basi ni wewe tu ndiye mwenye uwezo wa ku-handle issues.........mbona unazidi kudharau wanakamati wenzio wewe.

yaani ulianza kumdharau Bi Makinda na sasa umehamia kuwadharau wajumbe wa kamati ya Uongozi.

Kujiona kwamba wewe ni bora wakti unaongea pumba kuwadharau wenzio......shows how WEAK you are katika uongozi
 
"Mimi ndiye nilisimamia mjadala wa kuundwa Kamati ya kuichunguza Richmond. Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, ambayo iliipanga ripoti hiyo kujadiliwa kwa mujibu wa kanuni ambazo kwanza zinataka miswada ya Serikali ndiyo ijadiliwe. Ningekuwa na upande, mjadala huo usingefika hata bungeni. Kwa hiyo madai hayo hayaeleweki."[/QUOTE]


Kumbe akiwa na upande mjadala haufiki bungeni? Afadhali ametufumbua macho. Na kwa kweli huyu mzee nimegundua ni dikteta la kutupa na ndio anayeamua nini cha kupeleka bungeni na nini kisipelekwe. Sasa kwa nini alikuwa anabisha kuwa hoja ya Slaa hakuizuia yeye? Leo kajisema mwenyewe. Shame on you Sitta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…