R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Kutokana na taarifa za ikulu kuwa raisi atasaini mswada wa katiba mpya,
majina ya chenge na sitta ndo yanatajwa zaidi katika kinyanganyiro cha uspika.
Na kmbi rasmi bungeni ni cuf kutokana na kuwa na wabunge wa kutosha zanziba na bara
chadema bado aijatoa tamko kama itaomba kuhusiswa kutokana kuitolea nje cuf.
Lakini ni busara cuf wakichukua vijana wa chadema ambao sio wavurugaji kama mh zitto na mdee.
========
Feb 19, 2014
majina ya chenge na sitta ndo yanatajwa zaidi katika kinyanganyiro cha uspika.
Na kmbi rasmi bungeni ni cuf kutokana na kuwa na wabunge wa kutosha zanziba na bara
chadema bado aijatoa tamko kama itaomba kuhusiswa kutokana kuitolea nje cuf.
Lakini ni busara cuf wakichukua vijana wa chadema ambao sio wavurugaji kama mh zitto na mdee.
========
Feb 19, 2014
Feb 24, 2014Kama hakutakuwa na mabadiriko yeyote, basi tarehe 25 February 2014, siku ya Jumanne, mpaka kufika saa kumi na mbili jioni watanzania na Dunia itakuwa imemjua Spika wa Bunge la Katiba mpya ya nchi yetu.
Wajumbe wa Katiba mpya wameishateuliwa, na jana wameripoti Bungeni, tayari wameishamchagua Mwenyekiti wa muda ambaye atasimamia mchakato wa kumpata Spika wa Bunge ambaye ataendesha vikao vyote vya kuipata Katiba mpya.
Mpaka hivi sasa kumejitokeza majina mawili yanayotajwa tajwa sana ktk mchakato wa kuwania kiti hicho. Majina hayo ni la Mhe. Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine ni Mhe. Andrew Chenge, ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuingia ktk siasa na baadae kuteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Mhe. Chenge al maarufu kwa jina la "vijisenti" alilazimika kujiuzuru ktk wadhifa wa Uwaziri kwa kashfa ya Rada.
Mhe. Chenge na Mhe. Sitta wote ni wanasheria kitaaluma, wote wanatoka kanda ya ziwa. Ila wanatofautiana kimitizamo. Wakati Mhe. Sitta anaongoza kundi la watanzania wanaopinga ufisadi nchini, Mhe. Chenge yeye ni mhanga wa ufisadi kutokana na kashfa ya Rada. Kundi hili inasemekana linaunga mkono hoja ya mfumo wa Serikali tatu.
Taarifa kutoka viunga vya mji wa Dodoma vinadai kuwa, katika kampeni hii Mhe. Chenge anabebwa na kundi la Mhe. Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond, huku Mhe. Sitta akiungwa mkono na kundi la Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kundi hili linaunga mkono hoja ya Serikali mbili zilizopo hivi sasa, ila linataka kero za Muungano zitafutiwe dawa ya kudumu.
Sababu ya kuleta hoja hii hapa ni kutaka kutoa fursa kwa watanzania wanaoipenda nchi yao kutoa maoni yao juu ya mchakato huu wa Katiba mpya na bila kumsahau Spika atakayeliongoza Bunge litakalotuletea "KITABU" kitakacho tutawala kwa kipindi kirefu cha maisha yetu.
Kutoka na ratiba ya kwanza iliyotolewa na bunge la katiba tulidhani tarehe 26 kungekuwa na uchaguzi wa Sipka (mweyekiti?) wa bunge maalum la katiba na penginge hotuba ya ufunguzi ya Mh Rais. Hivyo bosi wangu alinikurupua na kuniagiza niwe Dodoma kufikia jpili. Nilipofika Dodoma nilipitia viwanja maarufu kwenye mitaa ya Kisasa, Nkuhungu na Kikuyu. Huko nilikutana na wajumbe wengi wanaotokana na Asasi za kiraia maana nafahamiana nao.
Kilichonitisha ni pale ambapo makundi ya Ccm walitufuata na kuanza kutushawishi kila kundi na mgombea wao, walianza kufika watu wa Sitta wakatuambia ubaya wa Chenge kwamba ni fisadi na kwamba anawakilisha kudi la mtandao wa mafisadi ambao wamekuwa wakitafuta madaraka kwa nguvu ya fedha chafu. Wakasema wana mtandao mkubwa wa mafisadi na wauza madawa ya kulevya. Wako tayari kuingiza madarakani watu wa aina yoyote ili mradi aliwasapoti katika juhudi zao. Wakatutaka tuwe makini maana usipika wa bunge hili ni jaribio tu la kuelekea katika nafasi wanayoitafuta!
Baada ya hapo wakaingia kundi linalosemekana la Chenge, wao walikuja na gia ya kwamba Sitta hakubaliki hata kidogo maana amekuwa akiisakama Ccm na serikali katika kujitafutia sifa. Wanasema wamebakiza kazi ndogo ya kuwashawishi wajumbe wasiotokana na Ccm ili kukamilisha kazi ya kumsimika mgombea wao. Wanasema linapokuja suala la kanuni hata Sitta anamkubali Chenge. Kuhusu kwamba mgombea wao ametumwa na kundi la mafisadi, walisema ni kelele za Sitta ambazo zimeshazoeleka, eti yeye mbona aliasisi CCJ hawakusema?
Eti na mimi naombwa kura! Nitasanua mengi maana hapa wajumbe wengi hawafahamiani.