Uko wapi Choice Variable uje ushuhudie jinsi yale tunayosema kila siku juu ya Ufisadi wa miradi ya Samia! Mchengerwa ni mkwe wake na Makonda ni kijana wake na ufisadi huu wa majengo unafanyika Arusha kwa mtoto wa mama!! Hapa huoni kuwa mama anapata mshiko wake kutokana na hii overinvoicing ya kwenye miradi ?Kufuatia tuhuma nzito za ufisadi alizoibua Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amewapeleka Gambo pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, baada ya mvutano mkali kuibuka wakati wa kikao cha Bunge.
Soma, Pia: Gambo aibua tuhuma za ufisadi wa mabilioni Arusha, Spika Tulia amwagiza Mchengerwa kuandaa ripoti iwasilishwe Bungeni
Gambo alitoa madai hayo, Jumatano Aprili 16, 2025, wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/26, ambapo alieleza kuwepo kwa harufu ya ubadhirifu katika ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kwa mujibu wa Gambo, vipimo na maelezo ya vifaa vya ujenzi kwenye BOQ vinatofautiana na kile kilichotekelezwa, akibainisha kuwa gharama ya jumla ya jengo hilo ni Shilingi bilioni 9—ambayo alieleza kuwa ni kubwa isivyo kawaida. Aidha, alitaja mkataba mwingine wa Shilingi bilioni 6.2 kuwa na mapungufu, huku baadhi ya kazi zikiwa hazijakamilika kulingana na makubaliano ya awali.
No wonder Makonda anaweza kuchinja ng ‘ombe 40 na kuwalisha wananchi wa Arusha!! Haiwezekani kutoka mshahara wake!
Serikali hii inanuka RUSHWA.😂😂