Spika Dkt. Tulia yuko sahihi sana, CHADEMA wajifunze kufanya vitu kwa usahihi na wafanye kiusahihi

Ka
Bunge ni taasisi, mahakama isingeweza kuingilia mamlaka ya bunge, kama ilivyotokea jana kwamba kina Halima wameshaenda mahakamani hivyo spika anasubiri maamuzi ya mahakama

Umeelewa sasa
KWELI kabisa, kama ilivyotokea wakati wa wabunge wa CUF.
 
Kama Mbowe ndo mhusika, yule aliyekuwa gerezani alimtoaje huko haraka haraka akawahi kuapishwa?
Anamaanisha Mbowe alishirikiana na serikali/vyombo vya dola (partners in crime).

Hii ni nchi ya vituko sana. Pamoja na dola kutaka kumuangamiza Mbowe kimwili, kihaiba na kiuchumi, huwa pia wanadai ni TISS - yuko CHADEMA kwa kazi maalum. Ni kizunguzungu tu.
 
Hakuna shaka katika hili la Mbowe?
 
Mkuu Chadema ni mali binafsi ya mwenyekiti, waliobaki wote ni wageni hawana ubavu wa kumfukuza mwenye mali...
Ndugu, hadithi za aina hiyo, hata watoto wa chekechea hawavutiki tena.
Mlihangaika sana kwa hali na mali ili kumtoa Mbowe ili kuweka mapandikizi yenu. Maadam Mungu wa haki yupo, hatuna wasiwasi.
Msipotubu na kuacha hila zenu, shetani atazidi kuwayumbisha nyie mlio wa kwake, katika mahangaiko yenu bila ya mafanikio. AMEN.
 
Wewe umeanza kuharibu jf, kila siku kupambana na chadema kwa malipo duni ya kujikimu
 
Mambo yakija pamba moto, hawa mawakala mmoja mmoja wataanza kudai kwenda maliwato.
 
Ww ni muongo, alafu ulituambia umeambiwa na watu wa ndani mdee na wenzake hawatafukuzwa chadema na uliapa chadema kwenye baraza kuu wakiwafukuza akina mdee unajitoa jf

MUONGO MKUBWA
 
Siku kibatala atakapo omba nakala na barua toka CHADEMA iliyowateua Hawa covid 19 , na Nusrat fomu yake ya iteuzi aliosaini saa ngapi akiwa mahabusu na alitolewa mahabusu kwa sheria ipi hapo ndipo paskali utakapo tafuta bandiko jipya ....
Nadhani hii ndio hoja kuu, kuna watu humu wako vizuri sana na wanajuwa mengi sana tusiyoyajuwa. Mimi ningeomba mpaka kina Mayalla mtu binafsi namuheshimu kwa michango yake, Mimi ukweli kabisa sina chama japo bado siamini kama Chadema wako ready siamini nadhani wanaweza kuwa wapinzani tu na kuleta changamoto lakini pia CCM na ukubwa wao wana mapungufu wakati mwingine kujimilisha hii nchi. Tuache haya turudi kwenye mada tuseme kuna ukweli wa aliyosema Mayalla, shida ni zile double standard, speaker aliwahi kutoa hukumu kabla ya hukumu kutoka mahakamani. Unaona kabisa yuko upande gani lakini ile haikuwa kazi yake yeye angesubiri hukumu angekuwa na hoja. Kuhusu yule dada aliyekuwa jela ataeleza na yeye wapi ali sign na toka lini watu wanaachiwa usiku rumande? Chadema inawezekana kuna mapungufu lakini Mayala kaongea bila kubalance na hili sio jambo zuri. Kwa mara hii tunaomba mtuambie ukweli uchama tuweke pembeni hii ni sheria za nchi, katiba ya nchi. Ni wakati hawa dada 19 kuongelea mchakato wa wao kupata uteuzi hakuna kuogopana au kumtaja mtu maana huko mahakamani kuna watu wataaibika kila kitu kitawekwa wazi hatutaki huko wakatajwa mpaka marehemu haipendezi sio tamaduni zetu.
 
Porojo uji Pascal unawaza sana ya upande huo kuna nini ki nakuumiza!??

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Huko ndiko tunataka lazima watajwe watu waliohusika lakini mimi sijawahi kusikia mtu mmoja anaamua maamuzi ya chama hapa sio kwamba kuna watu Chadema wataabika lakini pia CCM kuna wakubwa wataabika hili haliwezi kufanywa na mtu mmoja upande mmoja tu hakuna. Shida ya Chadema hata mitandandaoni hawataki kukosolewa wanakuwa wakali wanakuona adui lakini na CCM wao kila kitu wana support tu.
 
Mbona Tundu Lissu anasema na yeye alipinga kuvuliwa ubunge wake mahakamani, lakini bunge halikungojea mahakama?

Is this some selective justice system?

Kwani bunge linapata mamlaka yake wapi? Kutoka mahakamani au kutoka kwenye katiba?
 
Inafikirisha....ni kweli anasema alimbembeleza sana Mdee, swali, kwa nini?! Inaonekana Mbowe Yuko katikati ya mchezo wote
 
Naomba nikwambie kitu mdogo wangu britanicca .
Ni upumbavu na uhuni wa hali ya juu kufanya mapatano na mtu binafsi huku ukitegemea huyo mtu binafsi atakukingia kifua linapokuja swala la kitaasisi.
Taasisi ni kubwa kuliko mtu mmoja binafsi,hata kama huyo mtu ni kiongozi wa hiyo taasisi.
Mimi ni muwekezaji,ukikutana na mimi kishkaji na tukakubaliana kishkaji,usidhani kwenye makampuni yangu yatahusika na wewe.
 
Fanya yooote lakini bado utawajibika kwenye muongozo wa nchi. Ukisema katiba ya chama haiko chini ya katiba ya nchi basi mahakama isingekuwa na uamzi juu ya kesi za kisiasa. Katiba ya nchi ndyo katiba mama kwa vijikatiba vingine vyooote ndo maana mnahangaikia katiba mpya ya nchi ili mambo yenu ya kikatiba yaende sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…