PreGE2025 Spika Dr.Tulia: Rais Samia anafanya vizuri kuliko wanaume

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kufanya vizuri zaidi ya baadhi ya Viongozi wa kiume akieleza kuwa mafanikio yake ni ushahidi wa uwezo mkubwa wa Wanawake katika uongozi.

Dkt. Tulia Ackson ameyasema hayo alipohutubia kongamano la Wanawake wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) lililofanyika Jijini Dar es Salaam likiwakutanisha zaidi ya Wanawake 1,000 kutoka Shirika hilo.

Katika hotuba yake amewahamasisha Wanawake walioko kwenye nafasi za maamuzi ambapo Spika Tulia amewataka kutokuwa wanyonge kwa sababu ya jinsia yao na kuendelea kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 64 kati ya Nchi 146 duniani katika ajenda ya maendeleo ya kijinsia na ipo miongoni mwa Nchi 10 bora Barani Afrika zinazofanya jitihada madhubuti za kufikia usawa wa kijinsia.

My Take
Sasa Samia ana kipya gani zaidi ya mamiradi ya JPM
 
Hakuna nchi yoyote Duniani inayoongozwa na wqnawake kwenye mihimili yote 2 ya maamzi!. Ni Tanganyika KWA wapumbavu na wajinga.... Mijanaume kama Majaliwa, WASSIRA kutwa kusifia ujinga .... Takataka Tz.
 
Mimi sikatai. Nilidhani Magufuli ni katili lakini....
 
Is this even a point ? Au ameongea ilimradi kaongea?
 
Kuna Rais wa Kike na wa Kiume awamu hii ?

Hii ndio inaitwa kupoteza muda, au kwa lugha ya kitaalamu kuongea vapour...
 
Najua una akili njema. Jitahidi ushuuzi huu uwaachie ccm wajiandikie...tuwapuuze wangese hawa
 
Raisi wa Bongo anasifa kama za Mungu

Yeye anapenda kupewa sifa na kuabudiwa

Ukimpa sifa, ukitoa sifa itapokea ulaji

Si unaona Mh Spika anavyo toa sifa, sasa hivi kila mbunge ni mwendo wa kumwaga sifa ili wapitishwe huko chamani
 
Tulia ni Speaker wa hovyo sana kuwahi kutokea kwenye historia ya Nchi hii. Bila huruma na ubabe wa ofisi ya Rais, asingepata uSpeaker

She will always be grateful kwa Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…