Spika Makinda ‘abariki’ kodi ya simu

Spika Makinda ‘abariki’ kodi ya simu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
makinda.jpg

''Vitu vingine ni too cheap (rahisi sana) , hii kodi ni sheria, jaribuni kufikiria kuwa fedha hii kwa mwezi ni kwa ajili ya kupata maji, barabara na mawasi liano’. Makinda


KWA UFUPI

  • Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti, Spika Makinda alisema, “Haya maendeleo

  • tunayoyataka sisi kama Watanzania yatapatikana kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima achangie,”alisema.


Asema fedha hiyo ni ndogo na kwamba kila Mtanzania ana uwezo wa kuilipa.

Bagamoyo. Wakati sakata la kodi ya simu ya Sh1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayotakiwa kulipwa na watumiaji wa simu likiwa limerejeshwa bungeni na Serikali, Spika wa Bunge, Anne Makinda ameibuka na kusema fedha hiyo ni ndogo na kila Mtanzania ataweza kuilipa.

Spika Makinda alishangazwa na Mtanzania anayeshindwa kupata Sh1,000 kwa mwezi, kufafanua kuwa kama wananchi wataifanya nchi yao kuwa rahisi, watalalamika na umaskini mpaka siku watakayokufa. Julai 30 mwaka huu, Waziri wa Fedha, William Mgimwa alikaririwa akisema suala hilo litamalizwa bungeni kisheria na kwamba wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala na kodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti, Spika Makinda alisema, “Haya maendeleo tunayoyataka sisi kama Watanzania yatapatikana kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima achangie,”alisema.

Alisema bila kukusanya kodi nchi itashindwa kujiendesha na kusisitiza kuwa kama angeulizwa kuhusu masuala ya ulipaji kodi angesema uanzishwe hata mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana.

Alisema kwa kuwa suala hilo la kodi hivi sasa ni sheria, mabadiliko yake ni lazima yarudi bungeni na kwamba haamini katika kushindwa kulipa fedha hiyo.

“Tunataka kufanya vitu vingi na hatuwezi kuitegemea Serikali katika kila kitu sasa yenyewe itatoa wapi fedha. Hayo ni maoni yangu lakini hiyo ni sheria,” alisisitiza Spika Makinda.


chanzo.
Spika Makinda


SERIKALI INAWAUMIZA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI..................
 
Back
Top Bottom