Spika: Mazishi ya Mama Rwakatare yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10, Serikali itasimamia

Spika: Mazishi ya Mama Rwakatare yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10, Serikali itasimamia

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,982
Akifunga kīkao cha Bunge jioni ya leo, Spika Job Ndugai ametangaza kuwa mazishi ya Mama Rwakatare yatafanyika siku ya tarehe 23 Aprili na yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10, pia familia imeomba azikwe kwenye eneo la kanisa Mlima wa Moto.


Taarifa rasmi zinasema mama hajafariki kwa Corona lakini watu wengi wanajiuliza kwa nini katika eneo la kanisa hilo ambako Mama Rwakatale atazikwa na watu kumi tu, kila jumapili kuna mamia ya ya watu wanakusanyika kusali, iweje waruhusu watu kumi tukumzika kwa maelezo kuwa ni kuepusha msongamano?


Pia soma > TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) afariki dunia

​
 
R.I.P Mama. Wamesema ikiwezekana. Sasa Serikali ndo muamuzi wa mwisho. Mazishi kusimamiwa na Serikali. Merci à la Chine. Mama Rwakatare alivyokuwa msitari wa mbele kukemea Coronavirus. Leo imemwondoa. 😥😥😥💔💔💔💔
 
Hii si lazima iwe ni korona Bali inaonekana ni tahadhari dhidi ya korona. Hivi unadhani kama watu wakiruhusiwa kuhudhuria ni maelfu wangapi watahudhuria? Kwa mazingira ya sasa haiwezekani!!
Kwanini familia iiombe serikali wazike kwenye eneo la kanisa? Familia haina mamlaka ya kuamua azikwe wapi mpaka waiombe serikali?

Kwanini watu wasiozidi 10? kwanini wasiwe 100 huku wakizingatia social distance, kunawa, mask na sanitizer?
 
Back
Top Bottom