Spika Mstaafu Tulia Ackson aipongeza Kamati ya Bunge la Myanmar kwa kupigania Demokrasia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kupitia ukurasa wake mtandaoni Spika Mstaafu na Mbunge wa Uyole ameandika;

"Nawapongeza wanachama wote wa Kamati inayowakilisha Bunge la Muungano wa Myanmar (CRPH) kwa mapambano yenu thabiti dhidi ya ukandamizaji na kwa kujitolea kwenu bila kuyumba kwa matarajio ya kidemokrasia ya Myanmar. CRPH inasimama kama sauti ya wananchi, ikiwakilisha matakwa yao ya kuwa na serikali inayowajibika, iliyo wazi na inayojibu mahitaji yao."

1766228567643.jpeg

===

Wakati wewe ni Spika wa Bunge, sijawahi kusikika ukilaani mauaji ya kikatili ya raia, ilhali matukio ya mauaji yameendelea kutokea hadi katika mkoa wa Mbeya, eneo lako la nyumbani. Vijana wamepoteza maisha yao kwa kupigwa risasi kichwani, nawe umeendelea kukaa kimya.

Soma: Spika Dkt. Tulia na Wabunge wa CCM wagomea hoja ya watu kutekwa na kuuawa kujadiliwa. Wananchi Tuwaambie "YOU ARE FIRED"

Inaonekana unaumizwa zaidi na kunyimwa haki kwa wananchi wa Myanmar kuliko unavyoumizwa na Watanzania kunyimwa haki yao ya msingi ya kuishi. Hali hii inaibua maswali mazito juu ya uhalisia wa msimamo wako.

Unazungumzia kwa nguvu ndoto ya demokrasia imara nchini Myanmar, lakini unaonekana kupuuza demokrasia inayodhoofishwa waziwazi mbele ya macho yako hapa Tanzania. Je, huoni yanayotokea, au umeamua kutoona?

Mara kadhaa hoja ya utekaji iliwahi kufikishwa mezani kwako ukiwa Spika, lakini hukutaka Watanzania wajue kinachoendelea kuhusu utekaji unaoendelea nchini na kudai watu watafute majibu ya hoja zao kwa kuwauliza viongozi wao na si kwenda barabarani kuandamana

Kupongeza juhudi za demokrasia ya Myanmar kunazua maswali mengi kuhusu msimamo wako katika kulinda na kusimamia demokrasia nyumbani kwetu.

Hata ukiwa kwenye mahojiano bado msimamo wako ulikuwa hii nchi watu hawatekwi bali ni hawaonekani tu, ila watu hawajui
 
View attachment 3518197

Amelisema hili kwasababu ni IPU President au kwasababu anaamini hivyo regardless ya nafasi yake?

Ningemuona wa maana zaidi kama angeanza kwa kukemea ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya home country yake!
 
Huyo hana hoja anaongea hivyo baada tu ya kupoteza uspika, huko mkoani kwake mamia kama sio maelfu ya watu wameuliwa na utawala wa kikatili lakini hasemi chochote. Ghasia kabisa huyo.
 
Itakuwa deepfake AI
Usibishe mkuu, siku hizi bi betina anajifaragua sana mitandaoni hasa baada ya kutemeshwa bungo!

Anavyoongea sasa, utadhani ni binadamu, kumbe ni shetani halisi.
 
Back
Top Bottom