Spika Ndugai akerwa na tabia ya Serikali kuchukua fedha za halmashauri bila taarifa, ataka mfumo wa " less government" utumike nchini!

Anakuaga na mtindo wa kuitisha serikali toka kitambo enzi za Mwendazake Kisha anaitwa na kueka Mambo sawa. Maza Hana iyo mimambo ye anadili nae mdogo mdogo ashamuondolea Yule katibu wa bunge Kigaigai kamueka wake. Anamnyoosha tu
Si kweli.
Lini aliwahi kuitisha serikali ya JIWE?
 
Kama nilimuelewa vizuri alikuwa anaunga mkono hoja iliyoletwa na mbunge mmoja kuhusu mchezo wa serikali kupelekea halmashauri mapesa kibao ya mradi muda mfupi kabla ya mwaka wa fedha kuisha, halafu kuzichukua tena kwa kisingizio kuwa halmashauri imeshindwa kutumia!
Kwa mfano, halmashauri imeomba bilioni 1 kwa ajili ya kujenga kituo cha afya. Wanazunguka mwaka mzima bila mafanikio lakini mwishoni mwa mwezi wa tano wana dumbukiziwa bilioni 1 kwa ajili ya mradi. Kwa maana nyingine wanatakiwa wampate mkandarasi ambae atakamilisha ujenzi ndani ya mwezi mmoja kwa sababu hamna malipo yatakayoidhinishwa baada ya tarehe 30 saa sita usiku. Amesema hiyo sio haki maana mtoaji alipaswa kujua kuwa mradi hauwezi kukamilika katika muda huo.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…