Spika Ndugai amtaka Mbowe aache tabia ya kujipima ubavu na Mkuu wa nchi Rais Magufuli, aache kabisa!

Hiyo ni speaker inapaza sauti maneno yanayotoka redioni.

Na siku zote spika lazima isikike kama ina nguvu na uwezo, ila ikiwa mbovu hata alieko mita 5 hawezi kuisikia.
 
Kama huyu anayezungumza ndio Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano basi nchi hii ni zaidi ya gheto, Spika hajui azungumze nini aache nini.
Hii ni zaid ya aibu kwa Taifa huru kuwa na kiongozi wa mhimili nyeti kama Bunge. Ndugai ni laana ya Tifa hili, Spika anazungumza kama kichaa aliyepona?
 
Ndugai amezidi jujikimbakomba.... Sijui kwa vile anataka kurudi Nov....!!?

Mbowe alishapanga hotuba yake na watu walijua atakuwa anahutubia siku hiyo. Sasa hizi anazoxiita hotuba za Rais zinazoibuka bila kupangwa ndiyo zimekuwa tatizo.

Kule kuongea na waumini wa kabisa kijijini kwake Hakuqualify kudai kuwa Rais alikuwa anaongea na Taifa. Yaani kwa kuwa tu wamerusha matangazo live!?
 
Huyu mzee roho ya umasikini inamtesa sana, yeye alikwapua mabilioni kwenda India sijui India alikuwa kazini?
 
Spika Ndugai aendeshe bunge. Aachane na tabia ya kuisakama CHADEMA au Mbowe kila mara anaposimama. Mbowe hakuwa anajibu hotuba ya Rais. Alikuwa akitoa hotuba ambayo alipnaga kuitoa siku moja kabla lakini akazuiwa na Polisi.
 
Si bora Mbowe alisubiri, sisi tulimjibu muda uleule humu Jf na kwenye mitandao mingine maana hotuba yenyewe ilikuwa vurugu tupu!
 
Kwenye hotuba yake Mbowe alisema Spika anayemaliza muda wake uliobaki aombewe

Itakuwa jambo jema kama bunge lijalo hatutakuwa naye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…