Spika Ndugai asilaumiwe mpaka sasa

Spika Ndugai asilaumiwe mpaka sasa

Malima Chacha

Member
Joined
Oct 11, 2020
Posts
9
Reaction score
17
Kufuatia matamshi ya Spika wa bunge leo bungeni wakati akiwaapisha wabunge wateule Humphrey Polepole na Bi. Riziki, ambapo Spika amewahakikisha ubunge wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na Chadema

Kumeibuka kundi la watanzania wakipinga suala hilo.
Binafsi ningependa kuwaambia ya kwamba kamati kuu ya chadema kuwavua uanachama peke yake bila kupeleka taarifa rasmi kwa spika haitoshi kuhalalisha kwamba tayari wamepoteza ubunge

Chadema wanapaswa kukamilisha utaratibu kwa kumpa taarifa rasmi spika juu ya maamuzi ya Kamati kuu, jambo ambalo anapaswa kufanya katibu mkuu wa chadema John Mnyika

Hii haina tofauti kabisa na ile scenario ambayo Tundu Lissu aliyekuwa mgombea wa chadema wakati wa kampeni aligomea wito wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba hana taarifa rasmi zaidi ya kusikia tu

Maana kinachoonekana na kilichopo kwa sasa kwenye hili suala la wabunge hawa ni mchakato kutokamilika,

Pamoja na Wafuasi wengi wa chadema wa kudai kwamba hata taarifa rasmi ikipelekwa haitasaidia, LAKINI WATAMBUE KWAMBA WAO WANAPASWA KUTIMIZA WAJIBU WAO LIBAKI JUKUMU LA SPIKA

Tofauti na kufanya hivi basi wimbo utabaki kuwa ule ule wa Ndugai Ndugai wakati wajibu haujatimizwa.
#MChacha Franco
 
Mvunja sheria hawezi kupelekewa taarifa ya sheria aliyoivunja.

Kumwandikia barua ndugai juu ya kuvuliwa uanachama kwa hao Covid 19 wa Chademab ni sawa na kuhalisha kitendo kibaya cha uvunjifu wa sheria kilichofanywa na Spika, kitendo cha kuwaapisha "wanachama wa chama" kuwa wabunge bila ridhaa ya chama.

Kitendo tu cha kumuandikia barua ni sawa na kubariki uchafu alioufanya. Hiyo ni sawa na mtu aje kumchukua binti yako kwa nguvu na kumfanya mkewe halafu wewe unamuandikia barua huyo mtu kwa heshima kumtaarifu juu suala la mwanao badala ya kumchukulia hatua za kisheria, ndugai inatakiwa apelekwe mahakamani kwa kuvunja sheria wazi kwa kiburi.
 
Boss , Ndugai alipelekewa majina ya wabunge wa viti maalum walioteuliwa na CHADEMA na tume ya uchaguzi NEC.
 
boss , Ndugai alipelekewa majina ya wabunge wa viti maalum walioteuliwa na CHADEMA na tume ya uchaguzi NEC.

Sasa yeye ni kiziwi asiyesikia sekeseke hii yote iliyotokea???, anashindwa hata kuwasiliana na NEC???---- nchi gani hii imekosa coordination!!!. Hawa akina Ndugai na NEC wanalao jambo katika suala zima la huo Ubunge, wameisha likoroga kwenye uchaguzi bado wanendelea kulikoroga tena.

Katika hali hii ni lazima, kwa busara tu, kuwepo na coordination kati ya NEC, Chadema na Spika, Spika ni mkuu wa Muhimili wa dola anaweza kwa wadhifa wake kuwasiliana moja kwa moja na NEC na Uongozi wa chadema kutatua sintofahamu hiyo, it is simple like that, lakini Yeye ndiye chanzo cha "tag of war" za kijinga utadhani ni mtu wa kijiweni.
 
boss , Ndugai alipelekewa majina ya wabunge wa viti maalum walioteuliwa na CHADEMA na tume ya uchaguzi NEC.
Kama kweli mbona NEC walikuwa wanajichanganya? Tarehe 20/11/2020 walisema hawajapokea majina (ukitaka ushahidi wa video nitakuwekea). Tarehe 27/11/2020 baada ya CHADEMA kusema majina ni fake wakaibuka wakisema walipokea majina tarehe 19/11/2020 kisha kamati ya NEC ikakaa tarehe 20/11/2020 kuchagua majina ya wabunge na madiwani kutoka kwenye majina waliopokea. Huu mbona ni mkanganyiko unaodhihirisha uongo mkubwa.
 
Una uhakika kuwa Bunge halijapelekewa hii taarifa maalumu ya kufukuzwa uanachama?

Kite do cha Spika kudai kuwa atawalinda kinatoa picha flani.
 
Nduga alisema wapinzani awatorudi bungeni wakizidi labda 3 ndoto yake imepelea mmoja wafike 3.Leo anawashwawashwa kulazimisha wapinzani kuingia bungeni.
Naona kamisi kumtimua halima bungeni.
 
Attachments

  • Screenshot_20201201_051636.jpg
    Screenshot_20201201_051636.jpg
    100.4 KB · Views: 3
  • Screenshot_20201129_095823.jpg
    Screenshot_20201129_095823.jpg
    47.9 KB · Views: 3
Sasa yeye ni kiziwi asiyesikia sekeseke hii yote iliyotokea???, anashindwa hata kuwasiliana na NEC???
Mkuu, unaargue kama mtu layman kabisa asiyeelewa mambo. Sasa unataka speaker afanyie kazi habari za kusikia kutoka kwenye press conference? Chadema wasipopeleka barua rasmi ya taarifa maana yake ni kwamba hao wamama wataendelea kutambuliwa kuwa wabunge halali. Itakula kwa chadema!
 
Lakini CDM haikuwahi kuwateua hao akina mama.Wameghushi nakala .Ni wabunge hewa

Vuta hisia wana kukamata wewe umeghushi vyeti vya form 4 wakati wao ni mabingwa wa kughushi nyaraka.
 
Ndugai aliwahi kupelekewa taarifa ya Cecil Mwambe ya aki zlijuakali kuvuliwa uanachama akasema hajaipata hiyo taarifa.
Ila ushauri waki ni mzuri, kwamba mchakato huo ni lazima ukamilike kwa kumpelekea tena taarifa no matter what.
 
Lakini CDM haikuwahi kuwateua hao akina mama.Wameghushi nakala .Ni wabunge hewa

Vuta hisia wana kukamata wewe umeghushi vyeti vya form 4 wakati wao ni mabingwa wa kughushi nyaraka.
Kana uteuzi kimaandishi sio kupitia press ambayo mtu anaweza kwambia sijaisikia...
 
Ndugai ni taahira mwenye dhamana, pesa ya beberu ni tamu ni taaamuuu!!
 
Chadema inakwenda kupotea rasmi. Ukidhalilisha kinamama malipo yake ni makubwa.
Hivi wewe unawaza kisawa sawa kweli?.Ndugai mbona amewahi kuwafukuza akina Halima Mdee na Ester Bulaya bungeni Mara kadhaa,hapo hakuwanyanyasa?,Ccm mmewahi kumfukuza Sofia Simba na wenzake,Mliona chadema inasema kitu?,CCM mliwapiga na kuwajeruhi hao alina Mdee mbona tulinyamaza?.Usiwe punguani.
 
Hatuutambui huo uchaguzi na hakuna sehemu cdm wamesema wamewafuta ubunge kilichopo cdm wamefutwa uanachama
 
Mkuu, unaargue kama mtu layman kabisa asiyeelewa mambo. Sasa unataka speaker afanyie kazi habari za kusikia kutoka kwenye press conference? Chadema wasipopeleka barua rasmi ya taarifa maana yake ni kwamba hao wamama wataendelea kutambuliwa kuwa wabunge halali. Itakula kwa chadema!
Onesha barua ya kuwateua iliyopelekwa kwanza
 
Back
Top Bottom