Spika Ndugai ateua Wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
UCHAGUZI wa Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge 14 utafanyika leo, baada ya vikao vya kamati hizo kuanza, jijini hapa.

Huu ni mchuano mwingine bungeni kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wa upinzani ambao wanatarajiwa kupambana kuwania kuongoza kamati za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambazo kwa mujibu wa kanuni za Bunge lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani.

Ratiba ya kuanza vikao hivyo iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana, ilionyesha kuwapo kwa uchaguzi wa viongozi hao wa kamati 14.

Kamati zingine ambazo zitafanya uchaguzi huo mbali na PAC na LAAC, ni pamoja na Viwanda, Biashara na Mazingira, Katiba na Sheria, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Nyingine ni ya Utawala na Serikali za Mitaa, Huduma na Maendeleo ya jamii, Ardhi, Maliasili na Utalii, Kilimo, Mifugo na Maji, Miundombinu, Nishati na Madini, Sheria ndogo, Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) na kamati ya Bajeti.

Wiki iliyopita taarifa iliyotolewa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, ilisema kamati hizo zitakutana kutekeleza majukumu ya kibunge kuanzia leo hadi Januari 31, mwaka huu, kabla ya kuanza mkutano wa pili wa Bunge Februari 2, mwaka huu.


 

Attachments

Huwa sioni maana ya sheria kusema wenteviti wa kamati za PAC na LAAC kuongozwa na wapinzani wakati kiuhalisia wabunge wa CCM ndio wenye influence kubwa ya kumuweka huyo mpinzani wamtakae kwa kumpigia kura kwa wingi.

Ningeshauri wakati wa upigaji kura kwa wenyeviti wa hizo kamati mbili ( PAC na LAAC), wabunge wa CCM wawe excluded, hilo zoezi waachiwe wapinzani peke yao kwasababu ndio linawahusu.

Hata kama chama kimoja cha upinzani kitakuwa na wabunge wengi zaidi ya vyama vingine, kwangu ni bora chama hicho kitoe hao wenyeviti kuliko CCM kuwapigia kura wanaowataka wao ndio wawe wenyeviti wa hizo kamati, hii inapoteza maana ya hizo kamati kuongozwa na wabunge wa upinzani, wanakuwa wapinzani vivuli tu.
 
Huwa sioni maana ya sheria kusema wenteviti wa kamati za PAC na LAAC kuongozwa na wapinzani wakati kiuhalisia wabunge wa CCM ndio wenye influence kubwa ya kumuweka huyo mpinzani wamtakae kwa kumpigia kura kwa wingi....
Siasa ni maigizo, tuseme comedy show!

Everyday is Saturday........... 😎
 
Yupo Halima na Ester wanafanya hizo kazi . . . . . . .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…