Spika Ndugai atoa neno kwa Mbunge atakaye kataa bajeti ya serikali

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
1574488214608.png

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema mbunge anayekataa bajeti ya Serikali bungeni ni mpuuzi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiahirisha Bunge la sita la Vijana la mwaka 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma.

"Kuna mambo matatu katika bajeti, kusema ndio, hapana au kukaa kimya ambako ni ishara ya kuwa hujakataa au kukubali lakini unasema hapana kwa sauti kubwa hivi unamwelewa mtu huyo kweli," amesema Ndugai.

Spika amesema bajeti zinazokataliwa na wapinzani huwa zimebeba mishahara yao na watumishi wengine, fedha za miradi ya maendeleo na kwamba kusema hapana ni sawa na kutaka kila kitu kisipelekwe.
 
Hapana, si kweli kuwa kusema hapana maana yake ni kukataa kila kitu kisipelekwe. Kusema hapa maana yake ni kusema kuwe na mpango tofauti ambapo mambo mengine au yatapunguziwa akisi na mengine kuongezwa au yaliyopo kuongezewa akisi.

Ni bahati mbaya sana tunashindwa kukubaliana kwamba kiasili tunafikiri kwa viwango tofauti! So sad, kuwa hata pale mtu anapouliza kama bajeti imepitishwa - anakuwa ametoa haki ya mtu kusema ndio au hapana au kukaa kimya. Halafu bado anakuwa na machungu anapoambiwa hapana!!

Ikiwa hataki mawazo mbadala - waondoe habari za bajeti na wabaki na kutunga sheria tu.
 
Kama ni hivyo kwanini zikawekwa options tatu za kusema ndiyo, hapana au kukaa kimya??
Basi wangeondoa option ya hapana na ile ya kukaa kimya wabaki na ndiyooo tu ili bajeti isipate vikwazo
 
Kupewa tu jina la Soko kapagawa, na hilo jina la Soko hata sikia likiitwa na wachuuzi wa hilo soko. Ukiacha kariakoo masoko yote makuu nchini yanaitwa Soko kuu.
 
View attachment 1269789

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema mbunge anayekataa bajeti ya Serikali bungeni ni mpuuzi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiahirisha Bunge la sita la Vijana la mwaka 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma.

"Kuna mambo matatu katika bajeti, kusema ndio, hapana au kukaa kimya ambako ni ishara ya kuwa hujakataa au kukubali lakini unasema hapana kwa sauti kubwa hivi unamwelewa mtu huyo kweli," amesema Ndugai.

Spika amesema bajeti zinazokataliwa na wapinzani huwa zimebeba mishahara yao na watumishi wengine, fedha za miradi ya maendeleo na kwamba kusema hapana ni sawa na kutaka kila kitu kisipelekwe.

Babu kifimbo cheza Dozi ya Kisukari na ARV itakua hajanywa Leo
 
Kazi ya bunge ni kupitisha bajeti iliyoandaliwa na " Wataalamu" wa serikali.

Ndugai yuko sahihi hakuna mbunge mwenye taaluma ya kuweza kuikataa bajeti kisomi........wabunge wenyewe ndio hawa akina Kibajaji, Musukuma na Jaa Pipo!
 
Duh!! Kila anayekataa bajeti ni mpuuzi hata kama ana hoja ya msingi kufanya hivyo? Tunayo kazi!!!
 
Huyu hata hajui nini maana ya kuwa spika hana tofauti na waziri wa serikali. Ndugai bure kabisa. Tunataka aturejeshee ile Tsh. 27 bilioni aliyofanyia ufisadi kule India.
He is the worst speaker ever.
 
Back
Top Bottom