Spika Ndugai: Bunge langu limefanya mambo makubwa sana ikiwemo kupeleka wabunge zaidi ya 70 Misri kuishangilia Taifa stars!

Tusimlaumu sana Ndugai kama Spika, wakulaumiwa ni mwenyekiti wake anayependa kupewa heshima na kusifiwa muda wote

Rudini nyuma mwanzo mwanzo wakati awamu hii inaanza, ilifikia mahali hadi baadhi ya wabunge wakawa wanatamani vikao viongozwe na Ndugai maana yule bi mdada ni kama alikuja na maelekezo maalumu ya ku deel na wapinzani ki ubabe ubabe tu

Hakuna asiyependa kula. Huyu mgogo mambo yalibadilika alipousoma mchezo wa kupinduliwa na bi mdada ndio akili zikahama na mafaili yakapotea kabisa

Sasa siku zote jambo la kuiga na kufuata maelekezo lazima litakuumbua tu, ndiomaana anaonekana kituko sasa hivi

Tumuhurumia, Rais ni cheo cha mwisho kabisa, hakuna mkuu mwingine wa muhimili mwenye nguvu ya kupingana nae kama bado ana njaa.

Kina Prof Assad wako wachache nchi hii.

Mimi kuna wakati huwa najiuliza, hivi Ndugai ana mke na watoto kweli? Haoni aibu kutizamana nao usoni kwa anayoyafanya?
 
Asisahau amekuwa spika wa kwanza, kushurutishwa kulazimisha adhabu kwa wabunge wake ili wakashughulikiwe nje ya Bunge.

Na pia tofauti na waliopita hawakuwahi kutuhumiwa isipokuwa Ndugai (matibabu ya Apollo)
Ni Spika dhaifu sana tena mwoga sana. Huwa hawezi kuvumilia kusikiliza hoja mbadala. Bunge chini yake limekuwa dhaifu sana na lenye mipasho tu badala ya hoja. Nimemis Spika Sita. Bunge hili limemaliza muda wake kwa kupitisha sheria za kumkinga ili asishitakiwe kwa kuwa anajua madhaifu aliyopitisha yanayoweza kumfikisha kotini. Ana chukibinafsi. Kwa mfano alikuwa anamchulia sana Halima Mdee na Mbowe kiasi kisichisitirika. Wakati wa kampeni kule Kongwa alimchapa fimbo mpinzani wake. Huyu alifaa kuwa spika wa familia yake lakini kwa udhaifu alio nao nadhani hata familia haimudu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…