Spika Ndugai: Jimbo la Hai limepata Mbunge, aliyekuwepo kabla alikuwa anazurura, haulizi maswali Bungeni

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Jimbo la Hai limepata Mbunge hivi sasa, akiongeza aliyekuwepo kabla ya hapo alikuwa anazurura kila mahali.

Akiwa Bungeni Dodoma leo, Ndugai amesema, "Alikuwa haulizi maswali Bungeni, haeleweki. Lakini sasa Mbunge mnaye kabisa".

Kauli yake imekuja baada ya Mbunge Saasisha Mafuwe kuhoji ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KIA).

Mbunge huyo amesema mgogoro umekuwepo muda mrefu, na jambo hilo limesababisha wananchi kukosa maeneo ya malisho na kuishi kwa wasiwasi kwenye maeneo yao.

Pia soma > Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG
 
Mbowe usirudi tena bungeni uliturostisha sana wana hai. Mbowe hastahili kupewa heshima anayopewa.
 
Ndungai ana chuki binafsi na Mbowe, hilo liko wazi,ukichanganya na tuhuma anazopewa sasa na wanaccm za kumsaliti JPM amechanganyikiwa naona kile kiuvumbe kichwani kinaweza pasuka muda wowote tu.
 
CHADEMA wanapenda kujadili wenzao lakini wao kujadiliwa huwa wanakata moto haraka sana wanahamia kwenye matusi na ugomvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…