Spika Ndugai kakosea lakini pia hajakosea

Spika Ndugai kakosea lakini pia hajakosea

Mozila

Senior Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
174
Reaction score
48
Katika hili suala la Job naona alichokosea ni nadharia ya mambo ya kitaalamu (uchumi na mikopo) ambayo kama mkuu wa mhimili alipaswa apate ushauri wa wataalam kabla hajatoa maoni yake public, lakini hajakosea kupishana na Rais kwa kuwa tu wanavaa wote kijani.

Zile habari za "fikra za mkiti zidumu" ndio leo Mama amezipigilia msumari vizuri. Huko nyuma aliwahi kusema hataki wabunge kudemka wafanye kazi lkn leo amefungulia upyaaaaa watu kudemka.

Huko USA aliwahi kunukuliwa George Bush wa republican kuwa hatompigia kura Trump wa republican na haikuwa kosa wala kuitwa maadali kwa staili hii tutafika huko...
 
Ndugai anakosa gani? Tuanzie hapa
Kwanza alipongeza huo mkopo wa UVIKO 19 siku Mama anauweka hadharani alafu ghafla anauponda, pili kutokuwa na uelewa wa Mambo ya kitaalamu alafu unakwenda kuyazungumza hadharani bila consultation na wataalam
 
Kifupi samia anaona safari yake 2025 inakua ngumu. Kila akiwaza kuachia kiti cha urais wa msaada anaona hapana
 
Kuilaumu serikali ya awamu ya 6, kana kwamba ndio serikali ya kwanza kukopa na deni kufikia hizo trilion 70,
Je ni lawama au Speaker katoa maoni yake?wakati umefika watanzania tuwe honest tulivyo,ni haki yake kama mimi na wewe kutoa maoni yake,Archbishop Desmond Mpilo Tutu (rip)alitangaza hatawapigia kura ANC na maisha yakaendelea maana ilikua ni haki yake,hivi President Mwinyi (rtd)akitangaza hatawapigia kura ccm naona nchi itasimama.
 
Yeye wakati ana waadhibu wabunge waliokuwa wakitoa maoni yao hawakuwa na haki hiyo?!Amewatesa wangapi kipindi cha jiwe?!
 
Yeye wakati ana waadhibu wabunge waliokuwa wakitoa maoni yao hawakuwa na haki hiyo?!Amewatesa wangapi kipindi cha jiwe?!
Hili ndio tatizo kubwa tulilokua nalo,Tanzania ni pithole country maana mtumishi kama huyu(speaker)anawajibika kwa nani au chombo gani?matokeo yake naye alikua ni nusu Mungu
 
Kutoa maoni yake kuhusu mikopo haikua kosa ( japo alifanya kinafiki). Kosa ni kuomba msamaha na kusingizia media.

Hapo ameharibu kote, haaminiki kwa kauli yake wala kwa mwenyekiti wake wa chama.

Sasa hivi anamachaguzi mawili tu, la kwanza kujiuzulu la pili aingie vitani na Mama ( ajipange ipasavyo na mikakati thabiti, kitu ambacho hana uwezo huo).
Hiyo inamfanya abaki na chaguo la kujiuzulu tu.
 
Yeye wakati ana waadhibu wabunge waliokuwa wakitoa maoni yao hawakuwa na haki hiyo?!Amewatesa wangapi kipindi cha jiwe?!
Two wrongs don't makeup a right. Hii ndiyo shida. Watz hatujui tunataka nini. Tunadai katiba izingatiwe pale tu tunapokuwa tunamtetea tunayempenda. Ila kama anayepata cha moto hatumtaki, hata mambo yasipokuwa sawa sisi tunaunga mkono.
 
Hili ndio tatizo kubwa tulilokua nalo,Tanzania ni pithole country maana mtumishi kama huyu(speaker)anawajibika kwa nani au chombo gani?matokeo yake naye alikua ni nusu Mungu
Acha wayaone kwani watu wakipigania katiba mpya na nzuri ili kumlinda kila mtu wao wanapokuwa madarakani, wanaona ni kero, yanapowakuta ndio sasa wanaona umuhimu wake!!harafu leo hii linakuja jitu eti spika ana haki zake kama raia, hao wengine aliokuwa akiwakandamiza walikuwa pimbi?!!
 
Two wrongs don't makeup a right. Hii ndiyo shida. Watz hatujui tunataka nini. Tunadai katiba izingatiwe pale tu tunapokuwa tunamtetea tunayempenda. Ila kama anayepata cha moto hatumtaki, hata mambo yasipokuwa sawa sisi tunaunga mkono.
Wala inshu sio hiyo, katika watu ambao ameumiza wengi kwenye awamu ya 5 baada ya meko ni spika, hakuna kitu kilichowaumiza watu kama sakata la CAG, katiba iko wazi, walilizingatia hilo, hao wabunge 19 walioko bungeni hadi sasa ni katiba gani ina ruhusu hali hiyo?kwa awamu ya 5 hakukuwa na katiba bali ni watawala wanavyoamua iwe!!mimi CCM wote ni wale wale tu, ninakwambia kwa sasa hata hao wakina halima mdee ubunge wao upo rehani ni suala la muda tu!!kwani mzizi uliokuwa unawalinda umeshatikiswa.
 
Hata mimi simpendi ndungai kabisa. Ila ukweli ni kwamba hakuna kosa alilofanya kwa kutofautina na raisi.
Yeye anaongoza mhimili unaojitegemea na unaopaswa kusimamia serikali.
 
Hata mimi simpendi ndungai kabisa. Ila ukweli ni kwamba hakuna kosa alilofanya kwa kutofautina na raisi.
Yeye anaongoza mhimili unaojitegemea na unaopaswa kusimamia serikali.
Unaweza ukawa sahihi kabisa, lakini hoja yako ukaitoa ktk muda usio sahihi!!kwani toka meko amekufa, Ndugai ndio hata bungeni sasa akajifanya kuwa ni mkosoaji wa mambo mengi ya serikali, lazima watu wahoji mbona kipindi kile meko yupo ndio walikuwa wakishirikiana kufanya uzandiki?!
Huo muhimili wa kusimamia serikali ndio uanze awamu ya 6?una kumbuka Generali ulimwengu alipomsema nini kilitokea?!ki ukweli bila kumumunya maneno spika hakubaliani na uongozi wa mama, na hilo liko wazi!!kwani kipindi cha meko alipata favour nyingi sana, kwa kujipendekeza kwake, na ndio maana kila mkutano wa meko spika yupo.Bora hata na BETINA, yeye amejituliza tu, anachungulia kinachomkuta spika!!na kwa hili linaloendelea usishangae akaja pigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Back
Top Bottom