Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Kwa nini Mbowe aitolee uchambuzi wakati kisheria na anajua kabisa kwamba ni kamati za bunge PAC na LAAC ndio wanamamlaka ya kuichambua na kuiwakilisha kwetu kupitia bunge... Kama sio kutumwa ni nini?
 
Hatushangai kwa maelezo yake. Hebu fikiria mwizi wa kuku mwenye thamani ya shilingi 10,000 anafungwa miaka 10. Hawa Waheshimiwa wanakwiba shilingi 1,000,000 wanafungwa miezi sita na kifungo kuahirishwa hivyo wanatumikia jamii kwa kufagia hospitalini kwa wiki nne! "For Justice we better go to the Godfather" ...in Mario Bonasera's voice.
 
Hao mazuzu ni pamoja na wale waliobobea katika kufufua misukule.
 
Ulikuwa wapi wakati wa msiba mkuu ?! Poleni sana [emoji120]

Odhis *
 
Hivi wafikiri Mbowe ni mbumbumbu? hajui,,ana mda gani katika hilo bunge mpaka ashindwe kujua ,,na kumwambia amejiropokea huko ulaya.Hivi wewe bado una kichwa mgando?Au una fikiri Jiwe atarudi kwahiyo atakuona wa maana kukanusha?,,ukweli utabaki kuwa ukweli,juu ya Ripoti hiyo,,kama kuna madudu yataonekana,,kama hayapo pia tutayaona.Wacha tusubiri akina Babu Tale na Mwanaafuei waichambue,,,wakisaidiwa na Msukuma.
 
Mm nafikiri kuna tatizo hapa, aliyewakilisha ripoti ya wizi ni Mbowe au CAG? Kama ripoti ni ya uongo au tafsiri yake ina lengo la kuichafua serkali huyu si ndiye mwajiriwa wa serkali hiyo hiyo anayoitolea taarifa za wizi? Sasa hapa Mbowe anahusikaje? Namalizia kusema haya kwa hili analotueleza spika tunatakiwa tuwe na taaluma ya kihasibu kujua taarifa imepotoshwa.Si aitwe CAG awaeleze alikuwa na maana gani kuzungumzia upotevu na hasara nyingi za fedha alizozibainisha mle?Watanzania mbona tunageuzwa mazuzu na hawa wanaodhulumu kodi zetu kwa mabavu kupitia kwenye uchaguzi za kibabe?Mungu atoe uelekeo wa busara kwa Rais wetu.Mama nina imani naye anayo mwezi wa kuchambua wapiga dili hawa wanaopindisha pindisha sentensi ili tuendelee kupigwa.
 
Mzee Ndungai pengine hutumia msuba kabla ya kuingia Bungeni
 
Ndungai hupiga msuba kabla ya kuingia Bungeni
 
Je! Katika kipindi cha miaka mitano 2016 hadi 2020 bunge liliweza kuchambua na kujadili kwa kina taarifa za CAG? Je! Bunge liliweza kuisimamia serikali au lilikuwa linaiunga mkono? Je! Kunapokuwa matumizi ya fedha nje ya bajeti maana yake ni nini? Tuangalie tulipojikwaa na kuanguka ili kesho tusirudie tena. Tanzania ni ya Watanzania wote ambao ni wazawa. Hakuna mzawa anaeitakia nchi mabaya. Yeyote anaesema mwenzake ni kibaraka wa mabeberu anastahili kuangaliwa kwa jicho la tahadhari. Tena ni wa kuogopwa kama ukoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…