Spika Ndugai: Nimechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25, mara mbili nimepita bila kupingwa, unaniita ZUZU?

Spika Ndugai: Nimechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25, mara mbili nimepita bila kupingwa, unaniita ZUZU?

Ndio maana mirembe iliwekwa Dodoma kwa ajili ya kusogeza huduma kwa Wananchi kwenye hali hizo,nasema uongo ndugu zangu!.
 
Amwache Mzee wetu Asad kwani alimanisha hilo jina kwani hakutendewa haki
 
Kweli kila zama na kitabu chake. Leo hii Ndugai anapiga yowe bila kuchukua hatua zidi ya Assad,ingekuwa kipindi cha Kayafa sasa hivi Assad angekuwa mikononi mwa Polisi kwa amri ya Ndugai. Haya ni maneno ya Ndugai.

"Kuna Mzee anatukosea sana Wabunge,anatuita mazuzu,nina miaka 25 pale Kongwa na vipindi viwili nimepita bila kupingwa,na hata kesho nikienda nitapita bila kupingwa,kwanini uniite zuzu? Wananchi wa Kongwa ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?"

Credit: Dar Mpya.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani zuzu hana haki ya kuchaguliwa au kupita bila kupingwa😜!? Afu Asad mwenyewe naye ni mazuzu walewale, sasa anakelwa nini chizi akikuita chizi, mtu timamu si atapuuzia tu!?
 
Ile pesa ya Matibabu yake tungeweza kujenga hata madarasa 200 na nchi ikafaidika.
 
Aya majina ya JUMA ni bure kabisa.

Ona hapa:-
[emoji117]Juma jux
[emoji117]Juma lokole

Kweli kabisa, ukiitwa Juma ni sawa na senge hivi.. Jina la hovyo sana na la kimaskini kabisa.

CAG Jafar Musa Assad njoo huku, umezidi kutoa maneno machafu, mzee mzima jina lenyewe feki, kumbe sio Musa ni Jafar.

Ila Prof wengine kichwani akili hakuna kabisa, kama Juma tu
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaita wabunge mazuzu na kuwataka wajenge utamaduni wa kuheshimiana.

Akifungua wiki ya AZAKI jijini Dodoma Jumamosi Oktoba 23, Ndugai amesema, “Sio unaitwa Azaki basi unawasema wenzako maneno unayotaka ya hovyo. Tumewahi kugombana na baadhi ya wazee, mzee unatuita jina sisi hatulipendi…Hivi tumekosea wapi kama unamuita mtu jina la Juma anasema mimi jina hilo silitaki.

“Tatizo lako nini? Unang’anga’ania kuita hilo jina, we ni nani? Haiwezekani kama mwanadamu akikwambia hiki sina raha nacho kiache na wewe hukiachi, kama kweli wewe ni muungwana mtu wa Mungu utakiacha.”

Amesema matokeo ya kutoheshimiana ni wazee (ambao hakuwataja) wanawasema wabunge ni mazuzu wakati wana akili.

Amesema wao hawana muda wa kubishana bishana na watu wana namna hiyo.

Amesema yeye amechaguliwa na watu 400,000 kuwa mbunge kwa miaka 25 katika chaguzi mbalimbali na tena mara mbili amepita bila kupingwa.

“Hata kesho nikienda kusimama (kugombea) tafuta wa kusimama na mimi hutampata. Akisimama ni mpambe wa kusindikiza. Halafu wewe unaniita zuzu yaani wale watu una maanisha ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?”amehoji.

Ndugai alipongeza Azaki kwa kazi nzuri wanazofanya lakini akasema wachache wao wamekuwa wakitumika na wana ajenda zisizokuwa za kwao na kwamba Azaki chache zimekuwa na ajenda za kupata fedha kutoka mahali fulani (hakukutaja).

“Sasa kama we njaa yako ni hela ndio maana lazima zitungwe sheria sasa zinazokufuata kwenye hela. Eeeeh utatuambia nani amekupa, kiasi gani, ziko wapi, utazitumiaje na utaleta taarifa kwa kila shilingi zamani haikuwa hivyo tuliaminiana lakini baada ya kuona mwenendo usio ridhisha ndio tukatunga sheria,”amesema.

Ndugai amesema kama wasipoweka sera ya kuambiana na kurekebishana (wao kwa wao mashirika) basi hata sheria zitakazotungwa siku za usoni zitakuwa kali zaidi.
Huyu si alikuwa anapiga fimbo kichwani wengine? Ndo maana anapita bila kupingwa maana wenye akili wakija anawapiga fimbo vichwani anataka abakili yeye na mazuzu wenzake!
 
Mwerevu mmoja katika kundi la wendawazimu elfu moja, yeye ndiye ataonekana mwendawazimu
 
Prof. Jafar ( Musa) Assad atapigwa rungu moja kwishaaa, Ndugai anapiga, mpeni tahadhari plz

Prof Jafar Musa naye zuzu kubwa sanaa kazi kuiba majina ya watu tu, alafu huyu Prof afanyiwe vetting upya. Kafoji jina kachukua jina la mtu mwingine, kumbe yeye sio Musa ni Jafar, kasema mwenyewe, hapa kuna case ya kujibu kubwaa
 
Kweli kila zama na kitabu chake. Leo hii Ndugai anapiga yowe bila kuchukua hatua zidi ya Assad,ingekuwa kipindi cha Kayafa sasa hivi Assad angekuwa mikononi mwa Polisi kwa amri ya Ndugai. Haya ni maneno ya Ndugai.

"Kuna Mzee anatukosea sana Wabunge,anatuita mazuzu,nina miaka 25 pale Kongwa na vipindi viwili nimepita bila kupingwa,na hata kesho nikienda nitapita bila kupingwa,kwanini uniite zuzu? Wananchi wa Kongwa ni mazuzu wamechagua zuzu mwenzao?"

Credit: Dar Mpya.



Sent using Jamii Forums mobile app
inawezekana ata anaowaongoza pia ni mazuzu labda 🤣🤣
 
Ni kweli Mtu atavuna alichopanda hivi familia ya Ndugai inajisikiaje pale anavyochukiwa na kila Mtu.
Kwa kweli Ndugai awaombe Watanzania msamaha kwani haiwezekani ukachukiwa hivi ukakaa kimya ukajiona uko salama.
Unawaachia watoto na wajukuu shida ya kunyoshewa vidole
 
Back
Top Bottom