Spika Ndugai: PhD zina manufaa kwenye kufundisha na kutafiti lakini siyo bungeni, Dkt. Ndugulile aliwahi kumuita Waziri Profesa Ziro

Spika Ndugai: PhD zina manufaa kwenye kufundisha na kutafiti lakini siyo bungeni, Dkt. Ndugulile aliwahi kumuita Waziri Profesa Ziro

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akimpongeza mbunge wa Mtera mh Lusinde kwa uchambuzi mzuri wa hotuba ya Waziri Mkuu uliotumia dakika 15 Spika Ndugai amesema Kibajaj anawazidi wasomi wengi mle bungeni.

Spika amesema bungeni yanahitajika maarifa huo uprofesa ni kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti hivyo katika siasa uprofesa hauna maana yoyote.

Ndio maana wabunge watatu wamewaponda maprofesa tukianza na Kishimba, Kibajaji na kuna wakati Dr Ndugulile aliwahi kumuita waziri fulani Profesa Ziro nikamtoa nje haa haaa amecheka Ndugai.

Ndugai amewataka maprofesa kuwa makini wanapohutubia bungeni kwani darasa la 7 akina Kibajaji, Msukuma Tabasamu, Jah people, Kiinanasi, Babu Tale nk nk wako makini kweli.

Chanzo: TBC

My take; Mbona wabunge wa darasa la 7 ni wanaume watupu!
 
Pumbavu, mawazo ya darasa la saba! Kwanza ukiwafuatilia ni tabia za kujipendekeza, pili kwa kuwa muda wote utetea mihimili lazima wapongezwe, ila bila kujali matakwa ya baadhi ya waliodhulumika leo kumsema jiwe kwa matendo yake maovu haitajiki elimu yeyote.

Mtu ametenda mabaya asemwe faida wengine wasirudie maovu, wawekezaji wamekimbia, biashara zimeuwawa, uchaguzi umearibiwa, watu waliishi kwa hofu, uhuru finyu, ndio tupongeze? Watapongeza hao hao kina kibajaji!
 
Halafu eti ndio bunge hilo tunategemea liishauri serikali ili tupate maendeleo!

by the way Ndu guy anasikitisha sana, hao la 7B wanaongea pumba tu hakuna substance yoyote ile...ni mafundi wa kuongea kwa kutiririka tu kama pipa lililoachiwa juu ya kilima na kukosa uelekeo!
 
CCM mlitaka bunge liwe la kijani mkajipa ushindi wa mezani!

Aliyeusimamia ushindi bandia huo hayupo tena!

Tifuaneni vizuri! Siku nyingine mkumbuke ushirika wa wachawi haudumu..
 
Akimpongeza mbunge wa Mtera mh Lusinde kwa uchambuzi mzuri wa hotuba ya waziri mkuu uliotumia dakika 15 Spika Ndugai amesema Kibajaj anawazidi wasomi wengi mle bungeni.

Spika amesema bungeni yanahitajika maarifa huo uprofesa ni kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti hivyo katika siasa uprofesa hauna maana yoyote.
Ndio maana wabunge watatu wamewaponda maprofesa tukianza na Kishimba, Kibajaji na kuna wakati Dr Ndugulile aliwahi kumuita waziri fulani Profesa Ziro nikamtoa nje haa haaa amecheka Ndugai

Ndugai amewataka maprofesa kuwa makini wanapohutubia bungeni kwani darasa la 7 akina Kibajaji, Msukuma Tabasamu, Jah people, Kiinanasi, Babu Tale nk nk wako makini kweli

Source TBC

My take; Mbona wabunge wa darasa la 7 ni wanaume watupu!
Tatizo hicho kinundu kichwani
FB_IMG_1618336478528.jpg
 
Shida ya mjinga zinaanzia hapo; anadumu akijiamisha kujua, na kumbe anaendelea kutojua kwamba hajui.
 
Back
Top Bottom