Spika Ndugai: Tusimuachie Mama (Rais Samia) peke yake

Spika Ndugai: Tusimuachie Mama (Rais Samia) peke yake

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
"Tusimuache Mama Peke yake"

Kauli hii imetolewa na Spika wa Bunge Mhe. Ndugai leo hii Bungeni wakati akithibitisha adhabu ya Mbuge wa Kawe na Ukonga.

kauli hiyo ameitoa kwa hisia kali huku akimnyooshea kidole Waziri wa Mambo ya ndani kuchelea au kusita kuchukua hatua ama kukemea viashiria vya uvunjifu wa amani ya nchi.

Kauli hii ya Mhe. Spika imepenya masikioni na imenitafakarisha sana na kwa maoni yangu nadhani kuna baadhi ya Mawaziri na manaibu waziri hawamsaidii Rais ipasavyo ni kama vile "wame pararize".

kuna mambo yanajitokeza ambayo yanatakiwa either kukemewa au kutolewa maelezo na waziri husika lkn wapo kama hawapo.

Kwakweli Mawaziri amabao hawataki au hawataki au wameamua kugomea basi ni bora waachie ngazi mara moja maana hatuwaelewi kabisaa.

Mawaziri, Manaibu waziri, watendaji wa taasisi mbalimbali badilikeni.

Tunawajua na tunawaona mawaziri wote ambao "wanazuga" badala ya kushughulikia mambo ya msingi yanayo wagusa watanzania wao wanazungumzia mambo yasiyo ya msingi kabisaa kama vile hawajui lolote vile

Kumbe wanaumua kuzuga kwa maksudi, either kwa kutokutaka lawama au kwa kutaka kujipendezesha!! wanapaswa waelewe kuwa Ukiwa kiongozi lazima utalaumiwa tu, lazima utachafuliwa tu, jambo la msingi ni kuchapa kazi kwa masilahi ya Watanzania bila kujali makelele ya wahuni wachache.

Baadhi ya Mawaziri wana yumbishwa na kelele za wahuni wachache.
 
Spika aache ubabe. Waziri anayehusika anajua anachokifanya. Spika amempeleka Gwajima kwa sababu za kusema maneno yanayoonyesha kumpinga Rais. Hakuna jinai hapo, labda kwa ubabe tu.

Weledi ikitumika sio kupararize.

Kesha adhibiwa. Hawezi kuadhibiwa mara ya pili labda arudie matamshi hayo hayo.

Simtetei kabisa Gwajima, kutumishia mamlaka ndio kumemponza. Amegeuza kanisa lake kuwa talk show. Nawashangaa wanaoenda pale wanaenda kusali nini.
 
kuna baadhi ya Mawaziri wanachapa kazi kwa moyo wote bila kujali lawama au kulaumiwa au kuchafuliwa ilimradi tu masilahi ya watanzania wengi yapo, mfano:

1. Amb. Mulamula
2. Mwigulu
3. Awesu
4. Gwajima
5. Mkenda
6.Mashimba
8. Lukuvi
9. Jafo
10.Ummi
11. Kalemani
kwa maoni yangu Mawaziri hao pamoja na manaibu wao sio tu wanamsaidia Rais lkn wanajituma sana kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi.

walio baki wanasuasua sana kama vile hawataki, hawaeleweki ni kama vile wanazuga tu, lkn waelewe kuwa sio tu Rais anawaona bali sisi wananchi tunawaona zaidi, jirekebisheni au la wapishe kistaarabu.
 
12.

Kwa maoni yangu Mawaziri hao pamoja na manaibu wao sio tu wanamsaidia Rais lkn wanajituma sana kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi.

walio baki wanasuasua sana kama vile hawataki, hawaeleweki ni kama vile wanazuga tu, lkn waelewe kuwa sio tu Rais anawaona bali sisi wananchi tunawaona zaidi, jirekebisheni au la wapishe kistaarabu.
 
Kuna mawaziri ni kweli kabisa hawamsaidii Mh Rais na kuna wakati huwa najiuliza mama anafanyaje nao kazi kundi kubwa la mawaziri ni kama limeenda likizo. Hawafanyi kazi kabisa
 
Mkuu, kwani wao wote wamechanjwa? inawezekana wanakubaliana na hoja ya Gwajima kwa siri, ndiyo maana hawakemei 🤣
 
Spika aache ubabe. Waziri anayehusika anajua anachokifanya. Spika amempeleka Gwajima kwa sababu za kusema maneno yanayoonyesha kumpinga Rais. Hakuna jinai hapo, labda kwa ubabe tu.

Weledi ikitumika sio kupararize.

Kesha adhibiwa. Hawezi kuadhibiwa mara ya pili labda arudie matamshi hayo hayo.

Simtetei kabisa Gwajima, kutumishia mamlaka ndio kumemponza. Amegeuza kanisa lake kuwa talk show. Nawashangaa wanaoenda pale wanaenda kusali nini.
Kasema rais kapewa hela ili aruhusu chanjo kuingia nchin hakuna jinai hapo chief?
 
Kuna swali limeulizwa kama Rais Magufuli (R. I.P) angejiridhisha kuwa Chanjo ni salama na haina madhara na akatoa Msimamo kuwasihi Watanzania kuchanja kwa faida yao wenyewe, unaamini kuna juha yoyote angeshupaza shingo kufanya uhuni huu wanaoufanya sasa.

Huku ikifahamika kuwa Chanjo ni hiari ila kuto kuambukiza wenzako siyo hiari, unafikiri huyo unaemtetea ana uhalali gani ku mislead wananchi hata kama anajificha kwenye kichaka cha dini?

Yapo mambo ya kuyachekea ila siyo mambo ya hivyo kama hayo. Kama hutaki chanjo hulazimishwi lakini siyo kwa njia ya kuweka ligi na Serikali. Hakuna kitu kama hicho popote pale.
 
Kuhusu chanjo hata mawaziri wengi tu hawajachanjwa na wanaipinga, we uliona wapi chawene na budi wakichanjwa hau wakipigia chapuo chanjo

Umewasikia wakiongea chochote? Ukweli ni kwamba msimamo wa Serikali ni kuwa chanj ni hiari lakini kuleta propaganda huku ukiwa part ya Chama au Serikali, ni insurbodination, ambapo adhabu ni kufukuzwa kazi. Kwa muktadha wa wanasiasa sijui wanafanyaje, lakini kwa mfanyakazi wa Umma unafutwa kazi.
 
Kuna swali limeulizwa kama Rais Magufuli (R. I.P) angejiridhisha kuwa Chanjo ni salama na haina madhara na akatoa Msimamo kuwasihi Watanzania kuchanja kwa faida yao wenyewe, unaamini kuna juha yoyote angeshupaza shingo kufanya uhuni huu wanaoufanya sasa.

Huku ikifahamika kuwa Chanjo ni hiari ila kuto kuambukiza wenzako siyo hiari, unafikiri huyo unaemtetea ana uhalali gani ku mislead wananchi hata kama anajificha kwenye kichaka cha dini?

Yapo mambo ya kuyachekea ila siyo mambo ya hivyo kama hayo. Kama hutaki chanjo hulazimishwi lakini siyo kwa njia ya kuweka ligi na Serikali. Hakuna kitu kama hicho popote pale.
Ficha upumbavu wako ndugu suala sio nani Rais suala ni usalama wa wananchi. Usifananishe Magufuli na wajinga wajinga wenzako.
 
Mkuu unaonekana unaungamkono ukandamizaji wa haki za raia.
 
Mkuu unaonekana unaungamkono ukandamizaji wa haki za raia
Siungi mkono hata kidogo ukandamizwaji wa haki za raia, isipokuwa unapaswa ujue kuwa;

inapobidi haki ya mtu au ya wachache inaweza IKAVUNJWA AMA KUKIUKWA kwa MASILAHI YA WENGI/TAIFA.

Kiongozi yeyote yule aliyepewa dhamana ya kuwatumikia watanzania hawezi kuwa na kigugumizi ktk utendaji wake.

Kiongozi makini huwezi kuogopa ama kukwepa LAWAMA vinginevyo hufai kuwa kiongozi.

Hata ufanyaje huwezi kuwaridhisha watu wote lazima wapo ambao watalaumu tu.
 
kuna baadhi ya Mawaziri wanachapa kazi kwa moyo wote bila kujali lawama au kulaumiwa au kuchafuliwa ilimradi tu masilahi ya watanzania wengi yapo, mfano;
1. Amb. Mulamula
2. Mwigulu
3. Awesu
4. Gwajima
5. Mkenda
6.Mashimba
8. Lukuvi
9. Jafo
10.Ummi
kwa maoni yangu Mawaziri hao pamoja na manaibu wao sio tu wanamsaidia Rais lkn wanajituma sana kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi.
walio baki wanasuasua sana kama vile hawataki, hawaeleweki ni kama vile wanazuga tu, lkn waelewe kuwa sio tu Rais anawaona bali sisi wananchi tunawaona zaidi, jirekebisheni au la wapishe kistaarabu.
Huu ni uchonganishi, mawaziri na wateule wote walivurugwa tangu enzi za magufuli, lakini kulitaja kundi fulani kuwa lina nafuu si sawa. Ni bunge ambalo kwa muda mrefu lipo lipo tu. Ni bunge ambalo limeshindwa kuishauri serikali kwa kuvizia teuzi. Bunge linajitutumua kuiweka hadhi yake juu lakini linashindwa. Si bungeni tu, hata mitaani wabunge wengi mbele za jamii hawafai. Tuhuma za madawa ya kulevya dhidi yao zimezoeleka.
 
kasema rais kapewa hela ili aruhusu chanjo kuingia nchin hakuna jinai hapo chief?
Chanjo zimetolewa msaada na Marekani. Wamarekani wameigomea hiyo chanjo licha ya kuahidiwa kulipwa dola 100 kwa atakae kubali kuchanjwa. Viongozi wa Tanzania wamegawana kanda, kutwa wanazunguka kuhubiri ubora wa chanjo.

Nguvu hii ya kuhubiri wanaitoa wapi? Ni hawa viongozi kila sheria mbovu waipitishayo eg tozo, bei za mafuta etc ikilalamikiwa wanadai imewekwa kwa nia njema, ghafla wanawahurumia watanzania kwa kuwachanja, huruma hii imetoka wapi? Hisia za kuwepo na kupewa kitu, hazitakosekana.
 
Suala hapa sio chanjo.

Suala hapa ni upotoshaji wa maksudi ulio fanywa na Askofu Gwajima.

Mbaya zaidi anenda mbali zaidi kudiriki kutoa tuhuma kali dhidi ya viongozi kuwa wamehongwa.

Gwajima alifika mbali sana!

Huko sio kujiamini bali ni upuuzi!
 
Jibu upotoshaji wa Gwajima kwa hoja, si kwa mihemko. Chanjo ndio chimbuko la yote. Chanjo hatujaitengeneza, tumeletewa. Viongozi walio majukwaani kuhimiza wananchi kuchanjwa hawana ushahidi wa ubora wa chanjo. Gwajima ana maswali ya 'ya mtu mjinga', nayo yameshindwa kujibiwa, zaidi ya kuwa anapotosha watu. Waliotuzawadia chanjo wananchi wao walikataa, ikapelekwa Africa kusini wa wakaikataa, ikatua Tz, tunaambiwa ni nzuri funua bega.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom