Spika Ndugai usijilinganishe na Jenerali Ulimwengu

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Naona spika anapenda kijilinganisha na watu waliomzidi sana. Kwanza ilikuwa Prof Assad sasa Mzee Ulimwengu.

1CB5ECD4-3CB4-45E3-BB55-3CB181F618C5.jpeg

6054A938-558A-493A-B489-576634ED361A.jpeg

451799FF-BE74-44E5-B134-9C9E63892B84.jpeg
 
Wewe kipara cha zamani Ujuaji sio tatizo ila kumtisha mwenzako ili akae kimya ni tatizo kubwa.

Pia Kuwa mjuaji kama unajua sio tatizo, tatizo ni kuwa mjuaji wakati hujui. Jenerali anajua.
Haya tiba nini?
 
Naona spika anapenda kijilinganisha na watu waliomzidi sana. Kwanza ilikuwa Prof Assad sasa Mzee Ulimwengu.

View attachment 2008434

View attachment 2008435

View attachment 2008436
Kupiga picha na viongozi mbalimbali haikupi mamlaka ya kuropoka hivyo,ndio maana mkapa alimnyang'anya uraia amshukuru jaji waryoba kumsaidia,na wakati wa magu,alimpigia simu kumuonya asiropoke,jamaa kafikisika kabisa anategemea mkewe kwa kika kitu, sasa ndio anaropoka hovyo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Sina imani na wote wawili, Ndugai na Jenerali Ulimwengu.

Sina imani na Jenerali Ulimwengu hata kidogo tokea gazeti lake la Rai kwenye kampeni ya 2005 limchafue Salim Ahmed Salim na kumpamba JK na wengi walioshiriki walibarikiwa kupewa vyeo!!

BW Mkapa ile kampeni timu yake ya 1995 wale wengi wa karibu aliwatema live na hapo ndo bifu kuubwa mkapa alilopata toka kwa hao akina Jenerali na wenzie.

Kwa hiyo Jenerali hakutegemea kabisa kutoswa kivile mpaka akaanzisha makala kali za kuukosoa sana utawala wa BWM.

JK kuingia mwanzoni akaanza kumpamba, nanukuu ''Kwa mara ya kwanza tumepata kiongozi anayekemea rushwa kwa uwazi kabisa''. (maneno ya Jenerali hayo kwa JK)

Ghafla akagundua jamaa wala sio kama anavyofikiri. Hapo alitambua nguvu za akina Rostam Aziz dhidi ya JK na mtandao kwa ujumla ambao Jenerali hawakumu hitaji yeye, Salva, Shoo wakaparaganyika na RA kiulaini akainunua HCL na kuiweka chini yake huku Salva akielekea Ikulu, Shoo mtaani lakini akipata chapuo za kazi toka kwa RA kupitia Salva.

Wakati wa Mwendazake huyu Jenerali alikuwa baridi kama maji ya kwenye mtungi. Hakuthubutu kumkosoa wala kimsema kwani alijuwa kuwa anaweza kumpoteza kama walivyopotea akina Ben Saanane.

Tunaposhabikia hii vuta nikuvute ya Jenerali tujuwe tuna deal na mtu anayependa kujifanya ana akili sana na ni mjuwaji wa kuweza kumuamrisha hata Rais afanye anavyotaka yeye
 
Unalipwa shingapi inayokufanya uwatukane wazee waandamizi nchini mwako?
 
Kupiga picha na viongozi mbalimbali haikupi mamlaka ya kuropoka hivyo,ndio maana mkapa alimnyang'anya uraia amshukuru jaji waryoba kumsaidia,na wakati wa magu,alimpigia simu kumuonya asiropoke,jamaa kafikisika kabisa anategemea mkewe kwa kika kitu, sasa ndio anaropoka hovyo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Nyie mazuzu ebu semeni ukweli hivi kuna mtu anamzidi uropokaji ndugunjaa?Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana,kuwa speaker anajiona hawez kusemwa imagine awe amiri jeshi mkuu?Ufupi nao shida
 
Sina imani na wote wawili, Ndugai na Jenerali Ulimwengu.

Sina imani na Jenerali Ulimwengu hata kidogo tokea gazeti lake la Rai kwenye kampeni ya 2005 limchafue Salim Ahmed Salim na kumpamba JK na wengi walioshiriki walibarikiwa kupewa vyeo!!

BW Mkapa ile kampeni timu yake ya 1995 wale wengi wa karibu aliwatema live na hapo ndo bifu kuubwa mkapa alilopata toka kwa hao akina Jenerali na wenzie.

Kwa hiyo Jenerali hakutegemea kabisa kutoswa kivile mpaka akaanzisha makala kali za kuukosoa sana utawala wa BWM.

JK kuingia mwanzoni akaanza kumpamba, nanukuu ''Kwa mara ya kwanza tumepata kiongozi anayekemea rushwa kwa uwazi kabisa''. (maneno ya Jenerali hayo kwa JK)

Ghafla akagundua jamaa wala sio kama anavyofikiri. Hapo alitambua nguvu za akina Rostam Aziz dhidi ya JK na mtandao kwa ujumla ambao Jenerali hawakumu hitaji yeye, Salva, Shoo wakaparaganyika na RA kiulaini akainunua HCL na kuiweka chini yake huku Salva akielekea Ikulu, Shoo mtaani lakini akipata chapuo za kazi toka kwa RA kupitia Salva.

Wakati wa Mwendazake huyu Jenerali alikuwa baridi kama maji ya kwenye mtungi. Hakuthubutu kumkosoa wala kimsema kwani alijuwa kuwa anaweza kumpoteza kama walivyopotea akina Ben Saanane.

Tunaposhabikia hii vuta nikuvute ya Jenerali tujuwe tuna deal na mtu anayependa kujifanya ana akili sana na ni mjuwaji wa kuweza kumuamrisha hata Rais afanye anavyotaka yeye
Nililisoma andiko la Salva Rweyemamu siku za kampeni ya kumtafuta mgombea wa CCM kwenye nafasi ya Urais 2005 lililommaliza Salim Ahmed Salim kwa kumuhusisha na Hizb waliomuua Karume Senior huku akimpamba vilivyo JK. Hawa wawili ndio walioonekana kua hot and serious contenders wa hiyo nafasi

Salva Rweyemamu, Dr Gideon Shoo, Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo na Athuman Kanua(huyu hakua muandishi haswa) walikua ni Managing Partners kwenye HCL na kila mtu kama muandishi alikua yuko entitled kutoa mawazo yake sawa na mwingine bila kuingiliwa na wenzake

Sidhani kama ni sahihi kumuhusisha Jenerali Ulimwengu na mawazo binafsi ya Salva. Utakumbuka baada ya uchaguzi Salva akapata uteuzi kuongoza Kurugenzi ya Habari Ikulu huku Jenerali akiendelea na mishe zake mtaani. Kwahiyo kama kuna lolote hapo kati ilikua ni Salva na mipango yake na ile timu maarufu ikijulikana kama "MTANDAO"

Ni kweli pia baada ya JK kukalia kiti Jenerali aliandika barua ya wazi kwenye gazeti lao chini ya anuani "EWE JAKAYA MWEMA" akimtahadharisha na mambo mbalimbali ambayo mtangulizi wake aliyakosea. Naamini Ulimwengu alifanya hivyo akiwa na imani kubwa kama waliokua nayo Watanzania wote (ikiwemo wapinzani) kwamba JK anakuja ku address issues zilizomshinda Mkapa ikiwemo rushwa na ufisadi. Sina hakika kama JK aliishi matarajio hayo

Mwaka 1995 Jenerali Ulimwengu alikua Campaign Manager wa Mkapa. Baada ya uchaguzi kuna vitu walitofautiana. Na issue iliyokuja kuweka wazi ugomvi wao ni ya matibabu ya mke wa aliyekua Waziri wa Afya wa Mkapa Bwana Kitine ambayo inasemekana ilikua ni udanganyifu

Simtetei Jenerali Ulimwengu kwenye tofauti zake na Mkapa za huko nyuma maana undani wake siujui saana ila kwa hili la Ndugai Jenerali yupo sahihi
 
Back
Top Bottom