Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 7,755
- 11,737
Mimi sio mwanasiasa,kama wangepita wao kwenye majimbo hawa viongozi wa Chadema yasingetokea haya!Katiba mpya ndo mwarobaini.TLS na mzee Warioba na Jenerali Ulimwengu nyie ni wabobezi wa sheria inakuwaje mnakaa kimya kuona chombo muhimu kama bunge linachezewa na mtu mmoja tu. Hili sakata la kufukuzwa uanachama wabunge 19 wa Ndugai ndani ya CHADEMA linapoteza kbs umuhimu wa kufuata sheria na katiba...
Naomba nikukosoe. Ndugai hakuonekana mwenye wasiwasi bali mwenye kujiamini na aliongea kimamlaka.Leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika wa Bunge Job Ndugai amesimama na kumkemea Nape Nauye, Mbunge wa Mtama ambaye hivi karibuni alitoa maoni yake binafsi kuwa wale wabunge 19 waliotimuliwa na CHADEMA sio wabunge halali.
Ndugai, akonekana mwenge wasiwasi na aliyepoteza mwelekeo akaanza kwa kujisifu kuwa yeye ni mzoefu, hivyo asipangiwe cha kufanya.
Ameenda mbali zaidi kwa kutaka kuonesha kuwa akina mama hao 19 wanaonewa na mfumo dume uliopo CHADEMA. Ndugai anasahau yeye na Profesa Lipumba walichowafanyia akina mama wa CUF walipovuliwa ubunge kwa kimemo cha Lipumba.
Mzee Ndugai atabaki katika historia kama SPIKA DHAIFU kuwahi kutokea. Tunazitaka Mamlaka za kulinda Katiba kuhakikisha KATIBA inalindwa.
Ikiwezekana kila NDUGAI atakapoonekana hadharani azomewe kwa aibu anayoiletea Taifa.
Spika ndio mtetezi wao
Hiyo ni hata kwa faida ya Chadema wenyewe,mkiwaondoa wale mtaua chama chenu pasipo kujijua.Kwani kabla Nusrat Henje hajazawadiwa ubunge bunge lilikuwa linakosa hoja?
Kwani Mbowe yeye anatumiaje kichwa chake?Mkuu acha basi kutumia kichwa kama kabati la kutunzia meno. kichwa kina kazi nyingi mkuu
Wapo kwa ajili ya wananchi ,hawapo kwa ajili ya Chadema .Hata hao wabunge 19 hawajihoji kwamba wapo bungeni kwa ajili ya nani.
Kwani wewe ni mzima hapo ulipo?!Hiyo ni hata kwa faida ya Chadema wenyewe,mkiwaondoa wale mtaua chama chenu pasipo kujijua.
Sheria yenyewe inasemaje?nani anayeisimamia?Wewe umetumia hisia zako binafsi ku judge hili jambo. Lakini umesahau kuwa kuna utawala wa sheria.
Sheria haitaki prejudices mkuu lazima ifuate mkondo wake hata kama unaona tofauti lakini as long as sheria inasimamia usawa wewe utajua mwenyewe.
Wewe hujielewi naona. Unakurupuka kuleta mada bila kujua chochote.Sheria yenyewe inasemaje?nani anayeisimamia?
Very interesting...lakini hao wabunge wa upinzani,si ndo kila leo walikuwa wanafukuzwa bungeni wakitoa hoja...leo ndo wanang'ang'aniwa na kulindwa wasiguswe... hahahahaaaa siasa za bongo pasua kichwa.Kwani kabla Nusrat Henje hajazawadiwa ubunge bunge lilikuwa linakosa hoja?