Hujaelewa kitu gani hapo? Spika lazima ajiridhishe kuwa kufutiwa uanachama wa wabunge umefuata taratibu na katiba ya chama husika. Spika aliridhika CUF ilifuata kanuni na taratibu za katiba yake kuwafukuza uanachama wabunge wake. Chadema haikufuata kanuni na taratibu za katiba yake. Chadema haikutaka hata kusikiliza utetezi wa wahusika kabla ya kuwaadhibu, hivyo ilikiuka misingi ya natural justice. Kwa mjibu wa katiba ya chadema, baraza kuu la chama ndilo lenye mamlaka ya mwisho kwenye maamuzi ya kufukuzwa uanachama. Kwa sababu ya ukwasi baraza hilo limeshindwa kukutana. Taarifa kwa spika ya kufukuzwa uanachama wa wabunge hiyo aliipata kwa njia ya kipeperushi cha katibu mkuu, hivyo kushindwa kuridhika nacho kama kanuni na taratibu zote za katiba ya chadema zilifuatwa kuwafukuza wabunge hao.
Fuateni taratibu na kanuni za katiba yenu. Baraza la chama likae kutoa maamuzi yake. Wahusika kama hawataridhika wanaweza kukata rufaa mahakama kuu. Uamuzi wa mwisho kwenye suala hilo ni mahakama. Hivyo wahusika wataendelea kuwa wabunge hadi pale mahakama itakapoamua vinginevyo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe alipotimuliwa chadema, kwa nini iwe tofauti kwa hawa akina mama?