Leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika wa Bunge Job Ndugai amesimama na kumkemea Nape Nauye, Mbunge wa Mtama ambaye hivi karibuni alitoa maoni yake binafsi kuwa wale wabunge 19 waliotimuliwa na CHADEMA sio wabunge halali.
Ndugai, akonekana mwenge wasiwasi na aliyepoteza mwelekeo akaanza kwa kujisifu kuwa yeye ni mzoefu, hivyo asipangiwe cha kufanya.
Ameenda mbali zaidi kwa kutaka kuonesha kuwa akina mama hao 19 wanaonewa na mfumo dume uliopo CHADEMA. Ndugai anasahau yeye na Profesa Lipumba walichowafanyia akina mama wa CUF walipovuliwa ubunge kwa kimemo cha Lipumba.
Mzee Ndugai atabaki katika historia kama SPIKA DHAIFU kuwahi kutokea. Tunazitaka Mamlaka za kulinda Katiba kuhakikisha KATIBA inalindwa.
Ikiwezekana kila NDUGAI atakapoonekana hadharani azomewe kwa aibu anayoiletea Taifa.