Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka wale wote wanaotaka amfukuze Bungeni, Cecil Mwambe basi wamshauri (Mwambe) amwandikie Spika barua ya kujiuzulu kwake, halafu waone kama ataendelea kukaa Bungeni.
Spika Ndugai amesema hayo Bungeni leo Mei 12, 2020 na kusema kuwa maamuzi hayo yote ya kumrejesha Mwambe Bungeni, yamekuja kutokana na yeye kupata barua ya upande mmoja.
Amehoji, "Nimeeleza Mwambe amewahi kuniandikia barua lini? Hivi wewe ungekuwa Spika ungefanyaje? Huna barua ya mtu aliyejiuzulu ungefanyaje? Unamfukuza tu?"
Ameongeza "Lazima mchunguze na muangalie mzani uko wapi. Mwambe yupo hajafa, mwambieni aandike barua anikabidhi mimi. Akishanikabidhi muone kesho yake itakuwaje"
Aidha, Spika Ndugai amesema leo jioni atatolea ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na CHADEMA, kwamba Wabunge wake waliojiweka karantini kwa sasa hawatorudisha posho kwa sababu wao sio wezi.