Spika Ndugai: Wanaotaka nimfukuze Cecil Mwambe Bungeni, wamwambie aniandikie barua ya kujiuzulu

Spika Ndugai: Wanaotaka nimfukuze Cecil Mwambe Bungeni, wamwambie aniandikie barua ya kujiuzulu

Ivi wanasheria emu tupeni dondoo kidogo, mtu aliyetamka hadharani mchana kweupe na ushahidi wa ile clip bado ipo huwa haitoshi? mpaka aandike barua?

Natamani Mbowe kesho aende kwenye Media aseme nimejiuzulu ubunge Spika kweli ataendelea kumwambia wewe bado ni mbunge mpaka ulete barua?
Mbaya zaidi Mwambe alivyotangaza kuwa amejiuzulu ubunge na kuhama chama aliacha kabisa kuhudhuria vikao vya bunge lakini Spika Ndugai ndiyo akamuomba aje kuendelea na bunge 🤣🤣🤣
 
Chadema imekabwa koo,! Na hapo hata oktoba bado haijafika mbona maji mtaita mma!

Na hivi hamna hela hata za kampeni maana mabwana zenu wapo wanapambana na corona, hahahaha...

Sent using Jamii Forums mobile app

CCM Ilishapoteza dira kitambo sn ndio maana kuna goli la mkono, ndio maana dunia imetangaziwa kwamba CCM itaendelea kutumia dola kubaki madarakani ndio maana rais amewakataza wakurugenzi aliowateua na kuwalipa mshahara yeye wamtangaze mpinzani aliyeshinda na ndio maana ccm wanaogopa uchaguzi (rejea chaguzi za marudio rejea uchaguzi serikali za mitaa etc)

ccm NI CHAMA CHA KISHETANI
 
zaidi ya hapa anataka nini tena ?
 

Attachments

  • Isaya 10_12 Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya m ( 266 X 480 ).mp4
    652.6 KB
Matumizi mabaya ya madaraka. Kuna siku watatokea wenye nguvu za kufukua makaburi, ni vizuri tuheshimu katiba yetu kwa vitu ambavyo viko dhahiri na ceremony za kupeana kadi zipo na ukizingatia pia ni yeye aliyemwita aende bungeni na Mwambe naye akasema ameitwa na Spika aende kwani alielewa kuwa ubunge wake umekoma mara baada ya kujiunga chama kingine.

Ni bora Spika afanye masahihisho ya kosa kwa namna hiyo ya kuamuru Mwambe aandike barua kwani hakuna maana yoyote ya kutumia hoja ya nguvu ambayo baadaye itakuwa na madhara/consequences kwake.
 
mbaya zaidi Mwambe alivyotangaza kuwa amejiuzulu ubunge na kuhama chama aliacha kabisa kuhudhuria vikao vya bunge lakini Spika Ndugai ndiyo akamuomba aje kuendelea na bunge [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sabwoofer akili hana,kwanini hakutilia sheria ile ile aliyotumia kumfukuza Nasari bungeni??

Tukisema hana akili tutakuwa tumetimiza???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda unesahau hata zito alipovuliwa uanachama wa chadema aliendelea na bunge hadi lilipovunjwa bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Zito alienda Mahakama Kuu na kufanikiwa kuweka zuio la muda kwa Kamati Kuu Chadema kumjadili yeye na uanachama wake Chadema, wakati kesi yao ya msingi ilipokuwa yaendelea. Na hata hivyo Zito hakufika mpaka mwisho wa Bunge.
 
Ili CCM ianguke,ni lazima mambo na matukio kama haya yapete nafasi/yatokee kama ambavyo ilimbidi Yesu kusulubiwa ili sisi wanadamu tuokolewe.

Subirini yako mengi yanakuja na yatakayowashangaza zaidi.

Wamenyimwa maarifa ili utawala wao ufike mwisho na hivyo hawajui walitendalo mithili ya Wayahudi waliomsulubisha Yesu kutimizi maandiko,hivyo na hawa CCM nao wanayatenda haya ili kutimiza anguko lao pasipo kujua.
Ccm hii hii au ile ya Chato?

Wavurugane wao wenyewe ccm watengeneze chama kipya lakini wahusika ni wao wao kama ilivokuwa KANU Kenya then tutakunywa mvinyo wa zamani kwenye kiriba kipya.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Mzee hivi wale wabunge wa CUF uliowatimua Bungeni walikuandikia barua ya kujiuzuru kwao?

Ukawatimua maskini wa Mungu huku ukijua kabisa walikuwa wamefungua kesi mahakamani, ukaamua uliyoyataka juu yao.

Ni ushauri tu kwamba kuchezea KATIBA NA SHERIA za nchi si kitu kizuri. Hivi vyeo huwa ni dhamana tu.
 
Mala moja barua yao ikifika na kusomwa itafanyiwa kazi, kumbukeni tu Spika anakazi nyingi, anaweza isoma barua hiyo siku Bunge limevunjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hii case ya Nyalandu nayo unasemaje?maana Mwambe alipojiuzulu na kujiunga CCM,Chadema walimwandikia barua spika kama walivyofanya CCM hapo sasa leo Spika anasemaje kuwa hawezi kuifanyia kazi barua ya upande mmoja eti mpaka Mwambe amwandikie barua. Huoni haoa kuna double standard kwa malengo fulani?
tapatalk_1589290370146.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom