Spika sikiliza ushauri wa Mpina, iundwe tume kuchunguza kwa nini January Makamba amechelewesha mradi wa JNHP. Pia mizengwe ya bei ya mbolea

Spika sikiliza ushauri wa Mpina, iundwe tume kuchunguza kwa nini January Makamba amechelewesha mradi wa JNHP. Pia mizengwe ya bei ya mbolea

Mtu atuambie

1. Bwawa lilianza lini?
2. Lilipangwa kujengwa kwa muda gani?
3. Mpaka 17 March 2021 lilikuwa limefikia hatua gani?
4. Mpaka 20 June 2022 lilikuwa limefikia hatua gani?

Tukipata hizi data tutajua namna bora ya ku-deal na hili jambo
Hoja zijadiliwe hivi, sio kutanguliza mapenzi.

Kuna mjuvi mmoja alisema bwawa lilianza 2017, Jiwe akiwepo, mkandarasi afanye kazi mchana na usiku, hivyo kama ilikuwa lijengwe kwa miaka 5 kawaida, kwa usiku na mchana, muda ungepungua.

Kuna mtu anakumbuka hilo?.

Tukiweka ubinafsi pembeni, sio Makamba, Mwigulu, Nape, Ridhiwani, Simbachawene, Mulamula na wafananao wanaofiti kwenye nafasi za uongozi wowote ule wa kitaifa. Ni majina, pesa na chama ndo vinavyowabeba.

Ni kama kukaa kumsifia PFunk kuwa wakati ule alikuwa na kipaji na ubunifu, ukiuliza alipatia wapi elimu yake ya muziki, unaambiwa amesoma IST, Majani kasoma sijui nchi gani Ulaya huko, Mika Mwamba naye Ulaya ndo kwao, wakina Langa, Shaa, Witness, AY, Gwamaka, Vanesa, Faraja, Jokate, na wafananao...wote wako shaped na uwezo wa kiuchumi nyumbani na si kwamba wamefanya zaidi.
 
Mnafiki tu huyo Mpina, mbona kipindi cha magu alikaa kimya wakati uhayawani unafanyika?
Sawa ni mnafiki je akisikilizwa hoja zake utapungukiwa na nn unamanisha mambo yaendelee ivoivo punguzeni uchawa uo basi
 
1. Kinyerezi 3 & 4 zingekamilika na kuwa chanzo kikuu cha nishati
Pengine wewe ndo hujui kama hujui.
Unajenga 300MW plants kwa awamu awamu wakati demand ni kubwa!

Kawaulize Pan Africa wanavyonufaika na malipo ya gas wanayowauzia Tanesco, kawaulize TPDC wanawadai Tanesco kiasi gani kwaajili ya gesi wanayotumia!

2,100MW ilikuwa na milestone kwa wenye viwanda na wanyonge.

Kaulize tatizo kubwa viwandani kwa sasa kuhusu umeme ujue ni nini! Kipindi cha nyuma, jamaa walishaanza ku-stabilize outage hasa kwa viwanda, wamejaribu hata kupeleka dedicated lines viwandani, issue inakuwa na quality ya umeme kuwa mbovu! Sasa kama ni mtaalamu wa hayo mambo, utaniambia wanapolalamikia quality wanamaanisha nini na moja ya suluhu kwa hilo tatizo ni nini!
 
January ndiye rais?
January ndiye VP?
January ndiye PM?
January ndiye Baraza la mawaziri?

Hivi mleta mada unadhani waziri January ana nguvu kiasi cha kuchelewesha mradi ambao rais na serikali yake wote wanataka uishe?

Acha utoto.
Uzi ufungwe
 
Ujinga na utoto kama huu ndio umefanya Sendeka kuaibiaka na kufuta kauli baada ya Spika kusema anaweza wataka wote walete ushahidi..

Huyu Mpina nae ni hao hao wapumbavu,anaweza thibitisha madai yake kwamba Makamba JR kachelewesha Bwawa?

Kwamba Mpina hajui.kwamba hadi Kalemani anaondoka kwenye Wizara Bwawa lilikuwa limechelewa?

Watu kama Hawa wapotoshaji haifai hata kuwapa airtime.kwa.sababu mburula wengi wasio na akili z kiudadisi huwa wanaamini tuu.
Jaribu kuwa na akili hajasema makamba ye ameomba tume ichunguze ucheleweshaji wa mradi mbona unatua povu ambalo halina ulazima ndg mbona tume nyingi tu zimeundwa mfano.
1.tume ya covid 19 iliyoleta chanjo na watu mmenufaika na hizo chanjo
2.tume ya mkandala na zitto ambayo hadi sasa imefanya mikutano ya wanasiasa inafanyika kwa uhuru

Nini kinawaogopesha kwa hoja ya mh. Mpina
 
Ichunguze nini hapo?
 
Sawa ni mnafiki je akisikilizwa hoja zake utapungukiwa na nn unamanisha mambo yaendelee ivoivo punguzeni uchawa uo basi

Acha yaendelea hivyo hivyo mkuu, maana hata yeye alipokuwa kwenye ulaji hakuwa na faida yoyote.
 
Luhaga Mpina ametoa ushauri mzuri sana. Na hapa ni dhahiri kuwa kuna kitu chini ya kapeti. January amefanya hujuma zake mwenyewe ili mradi usikamilike. Dalili na harufu za hujuma zipo wazi.

Huyu Bashe ndio hafai kabisa kwa nini nchi za jirani bei za Mbolea zipo chini kuliko hapa Tanzania.?

👇
Mpina aikomalia Wizara ya Nishati
Luhaga Ni mnafiki tu. Makamba ana ubavu gani wa kuzuia mradi wa JNHP? Yeye aseme anampiga Vita Raisi Samia kupitia mgongo wa Makamba!
 
Mnafiki tu huyo Mpina, mbona kipindi cha magu alikaa kimya wakati uhayawani unafanyika?
Halafu na wewe unakoelekea!! Jiangalie sana, umeanza kuwa mweupe sana kichwani, staki kusema uzee unakunyemelea! Ila umeamua kuacha Kwa maksudi kuziona hoja na kuweka michango ile inayolisaidia taifa!

Jitahidi sana kusahau yaliyopita Kwa sababu hayasaidii chochote hata ukaishi nayo Kwa karine na karine
 
Mnafiki tu huyo Mpina, mbona kipindi cha magu alikaa kimya wakati uhayawani unafanyika?
Kwani nini maana ya mnafki?Wakati wa Magufuli alikua kimya coz aliamini Magufuli yupo sahihi, Now anaona yale aliyoamini hayapo ndio maana anapinga. Huu ni UNAFKI au hujui maana ya UNAFKI?
 
Muda mwingine hata kama unakuwa na chuki na mtu, fikiria kabla ya kuandika. January kateuliwa September 2021 na hadi sasa ni miezi 9 tu! Niambie sasa, nani amekaa muda mrefu kati ya January na Medadi?
Hii nchi ivumilie tu, ukweli ni kuwa Viongozi wa dini wamepandikiza chuki mbaya sana za udini kwa waumini.
Akiwekeza Mzungu inasifiwa hata kama fisadi
Akiwekeza Mwarabu inatahadharishwa nchi
Akipewa cheo Jo......, nchi kimyaaaa
Akipewa cheo Mo......, nongwa kibaooo.

NB: Nchi hii hakuna vita ya kidini, endeleeni kukashifu tu! Tufanye kazi tulishe watoto wetu maana unaweza mchukia mtu sanaaaa kisha ukakuta ndio anazidi kukuzidi kimaisha.
 
Halafu na wewe unakoelekea!! Jiangalie sana, umeanza kuwa mweupe sana kichwani, staki kusema uzee unakunyemelea! Ila umeamua kuacha Kwa maksudi kuziona hoja na kuweka michango ile inayolisaidia taifa!

Jitahidi sana kusahau yaliyopita Kwa sababu hayasaidii chochote hata ukaishi nayo Kwa karine na karine

Shetani yoyote hawezi kuungwa mkono fullstop.
 
Kwani nini maana ya mnafki?Wakati wa Magufuli alikua kimya coz aliamini Magufuli yupo sahihi, Now anaona yale aliyoamini hayapo ndio maana anapinga. Huu ni UNAFKI au hujui maana ya UNAFKI?

Alikaa kimya kwasababu alikuwa mezani kwenye mlo na wala sio kwakuwa aliamini yuko sahihi. Kama yeye aliona Magu yuko sahihi sisi tuliona hayuko sahihi, hivyo acha tumkatae shetani na mambo yake yote. Case closed.
 
Hoja zijadiliwe hivi, sio kutanguliza mapenzi.

Kuna mjuvi mmoja alisema bwawa lilianza 2017, Jiwe akiwepo, mkandarasi afanye kazi mchana na usiku, hivyo kama ilikuwa lijengwe kwa miaka 5 kawaida, kwa usiku na mchana, muda ungepungua.

Kuna mtu anakumbuka hilo?.

Tukiweka ubinafsi pembeni, sio Makamba, Mwigulu, Nape, Ridhiwani, Simbachawene, Mulamula na wafananao wanaofiti kwenye nafasi za uongozi wowote ule wa kitaifa. Ni majina, pesa na chama ndo vinavyowabeba.

Ni kama kukaa kumsifia PFunk kuwa wakati ule alikuwa na kipaji na ubunifu, ukiuliza alipatia wapi elimu yake ya muziki, unaambiwa amesoma IST, Majani kasoma sijui nchi gani Ulaya huko, Mika Mwamba naye Ulaya ndo kwao, wakina Langa, Shaa, Witness, AY, Gwamaka, Vanesa, Faraja, Jokate, na wafananao...wote wako shaped na uwezo wa kiuchumi nyumbani na si kwamba wamefanya zaidi.
Kinachonikera ni watu wanakuwa very personal badala ya kujadili issues. Mimi nilivyosikia bwawa litajengwa kwa miaka 3 nikashangaa sana. Zile zilikuwa ni siasa. Inawezekana Makamba akawa hafai hata kidogo, lakini asemwe kwa kuangalia ukweli, sio kumbebesha lawama ambazo sio zake.

Shida ya bwawa ilianza tangu wakati wa Mwendazake, na hiyo timu ikiundwa kama ikiwa ya ukweli itasema hivyo.
 
Halafu na wewe unakoelekea!! Jiangalie sana, umeanza kuwa mweupe sana kichwani, staki kusema uzee unakunyemelea! Ila umeamua kuacha Kwa maksudi kuziona hoja na kuweka michango ile inayolisaidia taifa!

Jitahidi sana kusahau yaliyopita Kwa sababu hayasaidii chochote hata ukaishi nayo Kwa karine na karine
Alijenga darasa huko kijijini kwao akidhania atapata ubunge bahati mbaya akaliwa kichwa amebakiza chuki kwa hayati JPM
 
No more funds are available for the project. I see it as a failing elephant.
Jiwe alikurupuka kuanza ujenzi wa mradi mkubwa kiasi kile bila ya kuwa na fedha na wakati huo huo mradi unapingwa na nchi wahisani..

Jiwe hafai
 
Back
Top Bottom