Brooklyn
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 1,459
- 286
Katika hali ya kushangaza jana TBC1 ilionyesha mechi live kati ya Cameroon na Japan pamoja na Holland vs Denmark. Wengi tulishtuka kwani ni juzi tu baada ya mechi kati ya German na Australia tulitangaziwa na TBC kwamba wasingeonyesha kupitia TBC1 mechi za mchana na jioni kutokana na wao kurusha matangazo ya Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Wakati naangalia taarifa ya habari ya TBC1 saa 2 usiku, ndipo nikang'amua kwamba Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta alikuwa amewaagiza TBC1 wasikatize matangazo ya Kombe la Dunia kupitia TBC1 na amewashauri warekodi vipindi vya bunge na kurusha baadae baada ya mechi za kila siku kuisha.
Katika maelezo yake Mh. Spika "mzee wa kasi na viwango" alieleza kwa ufasaha umuhimu wa Kombe hili la Dunia na kwa jinsi watanzania wengi wanavyolifuatilia kwa ukaribu ikiwemo "Mh. Rais na wabunge wenyewe" na hivyo kukatiza matangazo hayo ni kuwanyima mamilioni ya watanzania kufuatilia michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika.
Binafsi nakupongeza sana Spika Sitta kwa kuliona hilo.................naamini TBC wameshauza ving'amuzi vya kutosha ku break even katika mradi wao wa TBC 2 na sasa watuachie watanzania tufaidi uhondo wa WOZA 2010.
Naamini Spika Sitta ambaye ni member hapa jamvini alipitia link hiyo hapo chini na kuelewa kilio cha wananchi na hivyo kushauriana na TBC1 kutengua uamuzi wa awali.
https://www.jamiiforums.com/sports-...wa-tbc-bw-tido-mhando-umechemka-big-time.html