Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

Spika Sitta amtimua nje Cheyo (UDP) Bungeni kwa kubishana naye!

mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture518-cheyo-walking-outside-parliament-buldg-after-removal-speaker.jpg


Cheyo akitoka Bungeni baada ya kuamuriwa kufanya hivyo na Spika Sitta (Picha na Mroki Mroki)

Haipo!!
 
Jamani ilikuwa hivi;

Cheyo ameuliza swali kwenye kamati za kupitia mahesabu ya wizara ya mazingira. Alipouliza Sita hakuelewa ikabidi amuulize tena. wakati anauliza Sita akaingilia kuwa je wewe ni chemisty? jamaa akamwambia. baada ya kuuliza sita akamwambia hayo yalishasemwa na waziri.

cheyo akasema ndo umejibu? sita akasema ameshatolea maelezo sio majibu. cheyo akasema hajaridhika.

sita kamwaga radhi eti wapinzani wanapenda sana kila kitu wadikteti tu maana waklishasema lazima wasikilizwe tuu. akasema eti cheyo akishakalia kiti basi huku UDP hakuna mtu kuzungumza. Sita akasema eti cheyo anasema chemical haiunguzi mara moja. cheyo uvumilivu ukamshinda. basi akasimama, sita akamwambia kaa chini yaani kama polisi. nakwambia kaa chini. cheyo akaamua kuondoka na sita akasema sajini mtoeni nje. akatoka nje.

ukiona story ina eti nyingi ujue ni story ya uongo!...."ETI"....NI tungo tata!...huna uhakika na kitu....
 
Alisema Mrisho Mpoto kwenye ule utenzi wake wa "Mjomba"..... Kwa kweli Tanzania tumefikia mahali amabpo inaonekana kwamba watendaji wetu (top to bottom) hawana uhakika (nadhani hawajui kabisa) majukumu yao, mipaka ya madaraka yao (vikomo).... Kwa kweli nimeangalia ile ya PM kwa Zitto, na hili la Spika kwa kweli yanatia aibu sana sana saaanaaa.....
Wahenga walisema "yana mwisho haya", lakini bahati mbaya hawakusema mwisho utakuwaje??
 
The continuing grotesque caricaturing of that august office of the Speaker of the parliament of the URT would irk even the most austere mannered observers.

That a speaker would not only ineloquently disgrace his chair, but do so in repeated shameful frenzies, within the space of a few days, and apparently with all the proud pomposity of an unchecked sadist rural headmaster berserkly drunk with power, begs the question on whether true democracy is served in our parliament.

Moreover, his unfortunate, if not downright partisan remarks about the opposition MPs, not only exposes his ignorance of his arbitrating role, but sheds light on his lack of grace, character, impartiality, integrity, knowledge and a knack for compromise.

In a parliament that is so one sided by the sheer number of CCM members, the Speaker being from CCM, only a fool like Speaker Sitta would feel threatened and overreact in this way. I have never witnessed a Speaker so hellbent on dictating -without as much as providing the statutory stipulation guiding him - as Samuel Sitta. Compared to Pius Msekwa, Msekwa seems like a gentleman and a scholar.

But the greater tragedy tham Sitta is the status quo -including if not led by CCM members- allowing this hegemony of Draconian heavyhandedness, the uncalled for stigmatization and unfounded stereotyping, as long as it is directed towards the opposition.Parliamentary business is now conducted in the most shoddy way, one would be excused to envy the grace displayed in the conducts of football rivarlies -Simba vs Yanga, and wish our parliament could at least rise to that level.

One need not a degree in law or PR to note that Speaker Siatta does not set an example of abiding by the very same stipulation he is so quick to decree. I believe in the right of expression, and an MP as a representative of the people should have protection from Orwellian orangutangs and Ottomanlike ombudsmen like Sitta.

One of these days we may even witness what went down in the South Korean parliament, a pure parliament fist fight.Then maybe some people will learn not to play "Keeper of The Gate" too much when it comes to the people's interest.

Another sad day for the almost lost cause of Tanzanian democracy.

Du Bluray kwa mabomba.....
 
Du Bluray kwa mabomba.....

Sitta anatakiwa ashutumiwe kwa lugha kali kabisa, tena hata zaidi ya hii, halafu afanyiwe kampeni ya kung'olewa. That seat is too important to allow frivolous fraternizations.
 
Last edited:
Hili jambo tunatakiwa tulitazame kwa makini zaidi - Wakati Serikali inakiri Barrick ilisema uwongo ilipokana sumu toka mgodi North Mara:-

1. Wananchi wanaoishi karibu na mgodi wa North Mara wazidi kuathirika
2. Diwani aliyetoa taarifa hii yuko ndani, kashikiliwa na polisi kwa kusema uwongo.
3. Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, katolewa mkuku bungeni na Spika.
Kulikoni ?
Ni matumaini yangu kuwa yanayoandikwa humu yatabakia kuwa kumbu kumbu na kamwe hatatokea mtu wa kuya'edit" kwa manufaa yake. Huko mbele ya safari labda
kila moja wetu itabidi asimame ahesabiwe kutokana na mchango wake
kwenye mustakabhali wa taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni mimi tu au kiburi cha wabunge wa CCM kinazidi? Maana kaanza Pinda na kauli zisizo eleweka na sasa ni huyu spika. The only way to bring these people down to earth is through the ballot box. I think loosing their seats next year will humble them.
 
Taratibu watu wanaanza kutoa picha halisi za wao ni kina nani. Mambo mengine haya bwana yatakuja watoa jasho waheshimiwa siku zijazo kama wanafanya bila kufikiria athari zake
 
Siamini kuwa Spika aliuliza kama jamaa ni CHEMISTRY! Anasingiziwa.

Amandla......
 
..........kwa spika huyu wa bunge lenye wabunge wengi wa SISIEMU,hatuna sehemu ya kulalamikia!NI KAMA KESI YA NGEDERE UNAPOMPELEKEA NYANI!

tuamke wananchi tuingie barabarani kieleweke!AU TUKUBALI KUBURUZWA
 
Hili jambo tunatakiwa tulitazame kwa makini zaidi - Wakati Serikali inakiri Barrick ilisema uwongo ilipokana sumu toka mgodi North Mara:-

1. Wananchi wanaoishi karibu na mgodi wa North Mara wazidi kuathirika
2. Diwani aliyetoa taarifa hii yuko ndani, kashikiliwa na polisi kwa kusema uwongo.
3. Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, katolewa mkuku bungeni na Spika.
Kulikoni ?
Ni matumaini yangu kuwa yanayoandikwa humu yatabakia kuwa kumbu kumbu na kamwe hatatokea mtu wa kuya'edit" kwa manufaa yake. Huko mbele ya safari labda
kila moja wetu itabidi asimame ahesabiwe kutokana na mchango wake
kwenye mustakabhali wa taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania.​

Mkuu, Barriki lazima itoe mkwanja wa kuhakikisha ushindi wa kishindo, kwahiyo lazima itetewe kwa nguvu zote. Hata huyu Kagasheki aliye kiri kwamba wamedadanganya nadhani kapotoka (according to them)! Itabidi akafundwe haraka sana kujua kwamba kemikali ikiwepo inaleta madhara mara moja siyo ya muda mrefu. lol!
 
Mheshimiwa sitta hakumtendea haki mheshimiwa Cheyo.mimi binafsi nilikuwa naangalia tbc1.nilishangaa sana jinsi sitta alivyokuwa na jazba.nilikuwa nikiangalia kipindi hicho na mtoto wangu mwenye miaka sita hivi alishangaa jinsi amri ilivyotolewa na mkuu 'mbona anamfukuza yule mzee?aliuliza mtoto, nilitingisha kichwa kwa masikitiko.Saa mbili usiku tbc1 wakaongelea ile ile habari ya North Mara,niliona picha za watu walioathirika hizo kemikali,inatisha sana.Kisha nikaona jinsi kemikali hizo zinavyotiririka kwenye maji kiasi cha kubadilisha hata sura ya maji,halafu walioyapima maji wanadai ni ya kawaida.sihitaji hata mashine kuona yale maji kama yanafaa au la. ee Mungu tusaidie. KAGASHEKI nilivyokuona tbc1 najua hutaishia hapo,nashukuru hujapuuza sauti iliyokunong'oneza kwamba umedanganywa.Aibu juu ya vichwa vyenu mnaodanganya uma tanzania kwa masilahi yenu.MUNGU IPONYE TANZANIA.
 
Nimeangalia hili tukio, nilibaki mdomo wazi nisiweze kuamini kinachoendelea. Tena mzee Cheyo alikuwa anaongea kwa heshima sana. Spika alijaribu kumdhalilisha kwa kumuonyesha kwamba Cheyo hajui anachokiongea, lakini yule mzee akajikakamua na akaweka lile swali vizuri na kwa heshima kabisa. Cha ajabu badala Spika ampe nafasi waziri husika ajibu swali la Cheyo, anageuka mbogo na kuanza kushambulia upinzani, yaani akatoka nje kabisa! Hivi kumbe uspika ni mgumu kiasi hiki? The whole presentation and what was being said by this man was completely unprofessional and uncivil; never did I expect he could go that low!
I couln't believe what I was seeing on TV. It was so low. So disgusting. Six was the Minister, Six was the Scientist. He completely lost it, all of a sudden. He further panicked when Cheyo maintained a poised composure and repeated slowly, eloquently his question.

I wish I never tuned at that time. It was a shameful moment. Whatever respect I had left for this Man, has turned to hate.
 
Sitta alishatishwa kuwa jimbo lake liko mbioni kunyang'anywa na Fisadiz, hivyo inabidi atumie ubabe ili jina lake liweze kurudishwa. Nothing more than dictatorship.
 
Hapa hatuna Bunge kuna uhuni tu wa watu wazima ,yaani ukiangalia utaona hata mle ndani heshima hamna ,wengine wanauliza na kutoa hoja na wengine wanazungumza hata habari hawana ,na wengine wanachekelea na wengine na wengine yaani utaona kama watu wapo kwenye mkutano wa maskani.
Wabunge wanaonekana hawapo makini au siriaz katika mazungumzo yanayotolewa bungeni tofauti na mabunge ya nchi zingine ambapo unaona wabunge wanasikiliza kwa makini sana ,neno kwa neno mstari kwa mstari na hata kuzuka vurumai panapotokea ufedhuli wa kudharauliana.
 
kila ninapomsoma Bluray.......namkumbuka Pundit........
 
Siamini kuwa Spika aliuliza kama jamaa ni CHEMISTRY! Anasingiziwa.

Amandla......

Unafikiri kwa nini wengine huwa tunadai rekodi za yaliyotamkwa neno kwa neno?

Watu wanaweza kutumia kurasa mia wanajadili na kulaani utata wa kauli huku hakuna mwenye rekodi ya kilichosemwa. Eti mmoja kamuuliza mwenzake "wewe ni chemistry," Cheyo akajajibu yeye kasomea "Textile Chemistry," Sitta akamwambia umesahau chemistry, nyamaza, Cheyo akaendelea kuuliza, akaambiwa kaa chini, wao wapinzani ni madikteta, "sajenti mtoeni nje"! Mazungumzo ya nusu dakika wakafukuzani bungeni!
 
halafu afanyiwe kampeni ya kung'olewa. That seat is too important to allow frivolous fraternizations.

Itakuwa vizuri sana kama utafanya uchunguzi wa kina wa siasa za bunge hili kabla ya kufikia suluhu hili. Usije ukaruka mkojo ukagaragara katika kinyesi....

omarilyas
 
Back
Top Bottom