Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,271
- 1,052
RAIA MWEMA
Februari 18, 2009
Johnson Mbwambo
NILIPATA kuandika huko nyuma kwamba nchi yetu hivi sasa inapitia kipindi kigumu mno chenye majaribu ya kila aina. Nilisema kwamba ili kuweza kukivuka kipindi hiki ambacho pandora box limefunguka, tunahitaji kuwa na viongozi wenye hekima, ujasiri na uvumilivu.
Nilisema kwamba bila hekima, ujasiri na uvumilivu kutoka kwa viongozi wetu, taifa litapoteza dira kabisa na kuwa sawa na ndege ya abiria inayopita anga lenye mawingu mazito; huku ikiwa kwenye auto-pilot.
Tumefika mahali ambapo Watanzania wengi wamekatishwa tamaa na watawala. Tumefika mahali wafanyabiashara na wanasiasa maarufu wanaanzisha magazeti ya kushambuliana kuhusu masuala yao ya ndoa, ngono na uchafu mwingine!
Tumefika mahali DC mzima wa wilaya ya Bukoba Vijijini anakiri (tena bila woga) kwamba aliamrisha walimu wacharazwe viboko na koplo kwa sababu ya kuchelewa kazini!
Tumefika mahali ambapo hata watawala wenyewe kwa wenyewe hawaelewani; huku baadhi wakijenga ujasiri wa kuwanyooshea wenzao vidole kwamba wao ndiyo chanzo cha wananchi kupoteza imani kwa watawala wote. Na kwa sababu hiyo, malumbano ya wakubwa si haba. Hakika pandora box limefunguka!
Katika mazingira kama hayo, haishangazi atokeapo kiongozi mmoja kuishiwa uvumilivu na kutoa kauli ambazo wakati mwingine hazipendezi sana kutolewa na mtu wa wadhifa wake. Na hivyo ndivyo nilivyoziona kauli zilizotolewa wiki iliyopita na Spika wetu, Samwel Sitta kwenye kikao cha Bunge kilichomalizika, Jumatano iliyopita, mjini Dodoma.
Namfahamu Sitta si tu kama spika wa bunge letu, lakini pia kama mzee wa kanisa wa usharika ambao mimi pia nasali KKKT Kinondoni. Namjua kwamba ni mzee mwenye busara, hekima na uvumilivu.
Hata hivyo, kwa kauli zake za wiki iliyopita alizozitoa bungeni, Dodoma, napata hofu kwamba yaelekea naye anaishiwa na uvumilivu au labda niseme naye ameanza kukata tamaa kama sisi.
Nazungumzia kauli zake mbili alizozitoa, lakini labda nianze na maneno mawili potelea mbali, aliyoyatamka ndani ya bunge wakati akitoa kauli yake ya kujibu malalamiko ya Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan kwamba Bunge limekuwa likiingilia uhuru wa Mahakama.
Nakubaliana na Spika Sitta kwamba malalamiko yaliyotolewa na Jaji Mkuu hayawezi kunyamaziwa na Bunge kwa kuwa suala hilo ni la kikatiba. Lakini pia nakubaliana na haki ya Jaji Mkuu kulalamika mbele ya Rais kwamba Bunge linaingilia kazi za mahakama.
Nisichokubaliana nacho, au labda nisema kilichonishangaza, ni matumizi ya Spika ya maneno potelea mbali. Alisema hivi: Hapa, watasema pia naingilia Mahakama, lakini potelea mbali.
Maneno potelea mbali, kama alivyoyatumia yeye, yanaashiria mtu aliyeishiwa uvumilivu wa kurekebishwa tatizo lililopo kwa utaratibu wa kawaida; na hivyo anaamua kutoa dukuduku lake bila kujali yatakayofuata! Potelea mbali, kwa namna alivyoyatumia yeye, yanafanana na maneno ya Kiingereza come what may!
Sasa kwa kuchagua kutumia maneno hayo, Spika Sitta ametia doa hoja yake nzuri kwamba Bunge haliwezi kukaa kimya likikosolewa na mhimili mwingine wa utawala, na wala haliwezi kukaa kimya likiona mhimili mwingine hauheshimu maslahi ya umma (ya walio wengi).
Kwa kutumia maneno hayo ya liwalo naliwe, Spika Sitta ameweka taswira ya mpambano confrontational (dhidi ya Jaji Mkuu Augustino Ramadhan?) , na nahisi ni kwa sababu ya kuishiwa uvumilivu.
Sasa sidhani kwamba katika kipindi hiki kigumu, baada ya pandora box kufunguka, tunahitaji spika ambaye anaishiwa uvumilivu haraka kiasi cha kusema potelea mbali (liwalo naliwe). Nadhani tunahitaji spika mtulivu, asiye na jazba, anayepima hoja na anayetumia busara kutafuta maslahi ya umma yanaangukia wapi katika pande mbili zinazokinzana.
Lakini zaidi ya yote tunahitaji spika mvumilivu; maana spika akiishiwa haraka uvumilivu, iweje kwa sie raia wa kawaida? Kwa ufupi, lugha ya potelea mbali (come what may) si lugha tunayoitarajia itumiwe na spika.
Tukiyaweka maneno yake hayo mawili pembeni, bado pia kuna mengine yasiyopendeza aliyoyatamka ndani ya bunge siku ya pili yake wakati akieleza kukerwa kwake na uandishi wa baadhi ya magazeti nchini.
Alisema hivi:Nafikiri sheria ya magazeti haiwezi kushindwa kushughulikia hili. Kama kawaida yangu nafyatuka tu. Sasa kama hii ndiyo hulka yangu utafanyaje? Hii ndiyo kawaida yangu, na wakati mwingine ni vizuri katika taifa kuwepo na watu kama mimi wanaofyatuka ili mambo yaende mbele.
Sitaki kuzungumzia hoja kwamba kushambulia magazeti hayo bungeni kunaweza nako kutafsiriwa kuwa ni kuuingilia mhimili wa nne (fourth estate); lakini niseme tu kwamba maneno aliyoyachagua Spika Sitta kuwasilisha malalamiko yake hayo, nayo yameniacha hoi.
Spika Sitta anasema: kama kawaida yangu nafyatuka tu. Hivi kweli katika kipindi hiki kigumu ambapo nchi inatikisika kutokana na kukithiri kwa ufisadi na kutelekezwa kwa maadili ya uongozi, tunahitaji Spika anayefyatuka tu?
Ninavyojua mimi, mtu anayefyatuka tu si mtu mwenye busara wala hekima. Hivi kweli katika kipindi hiki kigumu tunahitaji spika ambaye anafyatuka tu? Mimi naamini tunahitaji spika mtulivu, spika mwenye hekima zaidi, ujasiri zaidi na mvumilivu zaidi!
Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba pamoja na kuwa maudhui ya alichozungumza ni mazuri, lakini halikuwa jambo zuri kwa yeye kuwatangazia Watanzania wote (na kuingia katika hansard za Bunge) kwamba ni kawaida yake kufyatuka. Sidhani kwamba ufyatukaji ni moja ya sifa za kiongozi bora.
Hata hivyo, nisisitize tena hapa kwamba tuna spika jasiri na anayekerwa kweli kweli na umasikini wa Watanzania. Tuna spika anayekerwa na kukithiri kwa ufisadi nchini.Tuna spika anayekerwa kweli kweli na kukwama kwa nchi yetu ki-maendeleo.
Tuna spika ambaye amesimama kidete kuibana serikali kuhusu utekelezaji wa maamuzi ya Bunge juu ya masuala yanayougusa umma kuliko spika mwingine yeyote tuliyewahi kuwa naye katika historia ya nchi yetu.
Na ndiyo maana ninataka kuamini kwamba kwa kutumia maneno aliyoyatumia wakati alipotaka kuonyesha hisia zake hizo bungeni, wiki iliyopita, ni kughafilika tu, na si dalili za kukata tamaa na kuishiwa uvumilivu. Spika Sitta ni mtu wa mwisho tunayetarajia kukata tamaa na kuishiwa na uvumilivu!
Nimalizie tafakuri yangu kama nilivyoianza. Pandora box limefunguka. Tunapitia kipindi kigumu. Ufisadi umetamalaki nchini. Kuna kukata tamaa, na kwenye kukata tamaa kuna kuishiwa na uvumilivu. Tuombe tu Mungu kwamba wanaotuongoza wasiwe ndiyo wa kwanza kuishiwa uvumilivu na kuanza kuwa confrontational.
Tafakari.

Last edited: