Spika Tulia Ackson alivyofungua Mkutano wa uwasilishaji wa maazimio ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Your browser is not able to display this video.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, tarehe 14 Februari 2025, amefungua Mkutano wa uwasilishaji wa maazimio ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kuhusu taarifa za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na hatua zilizopigwa na Mabunge Wanachama.

Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Trusteeship, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), Jijini New York, Marekani.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za IPU kwa kushirikiana na UN kuhakikisha Mabunge yanatekeleza kikamilifu ajenda za maendeleo endelevu kupitia mijadala yenye tija, tathmini ya mafanikio na kushirikishana mbinu bora za utekelezaji.



Pia soma ~ Shigongo katika Mkutano wa Mabunge ya Dunia, aelezea umuhimu wa Afrika kutumia maliasili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…