Spika Tulia Ackson anapingana na Rais Samia? Kati yao nani tumsikilize na kumuamini?

Spika Tulia Ackson anapingana na Rais Samia? Kati yao nani tumsikilize na kumuamini?

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Hawa ni viongozi wawili ambao wote ni wakuu wa mihimili 2 katika nchi, wote ni wa chama kimoja, wote walikuwepo tangu enzi za Hayati JPM, wote walikuwa ni "Makamu" kipindi cha Hayati JPM, na wote kwa sasa ndiyo wakuu wa mihimili hiyo baada ya watangulizi wao mmoja kufariki na mmoja kujiuzulu msawazia.

Baada ya JPM kufariki, Mama Samia aliposhika hatamu aliamua kubadili upepo wa aina ya uongozi wake, hakutaka kufuata mrengo aliokuwa nao JPM wa siasa za ubabe ubabe.

Lakini hali ni tofauti kwa huyu Mama Tulia, kauli yake ya jana akiwa huko Mbeya inaonesha bado ana element za u-JPM pure.

Kwenye "Mkutano wa Wadau wa Demokrasia" uliofanyika mwaka huu, Mama Samia alisema yafuatayo:

"Ni mazungumzo, siyo nguvu wala ugomvi wala matusi au kutishana, hivyo niwaombe wenzangu wenyeviti wa vyama vya siasa, tusitazame yaliyopita, tutazame mbele kwa matumaini. Tuweke nguvu zetu pamoja kujenga Tanzania mpya yenye kusameheana, yenye kuheshimiana, na kufungua kurasa mpya ya kwenda na demokrasia yetu Tanzania."



Jana Spika Tulia amekuja na hii kauli ambayo inaendana kinyume kabisa na kauli ya Rais Samia ya hapo juu:

"Isitokee kijana yeyote akaungana na mtu yeyote, anayemsema vibaya Rais wa JMT. Rais Samia ni Rais wa Nchi, lakini pia ni Mwenyekiti wa chama chetu. Asitokee mtu yeyotee, wa nje ya chama, wa ndani ya chama akawa anamsema vibaya Rais Samia halafu wewe unamtazama, shughulika naye na nyooka naye."



Maswali ya kujiuliza:

1. Nani anaongea ukweli wake wa moyoni, Rais ama Spika?

2. Je, Spika bado ana element za utawala uliyopita?

3. Je, Spika kwa kupingana hadharani na Rais anakuwa hajavunja ile "Collective Responsibility" aliyoizungumzia Rais alipomtumbua Mulamula?

4. Ni kwa nini pamoja na Rais kuruhusu vyama vifanye shughuli zake lakini bado wanazuiwa kuendesha mikutano ya kisiasa, katika mazingira haya tumuamini Spika ndiyo yuko "Real?".
 
Kama hata kemea hadharani hayo maneno aliyo ongea Zena basi ni wazi ame furahishwa nayo.
 
Acha kupotosha hii video haijafika mwisho alichikimanisha kama ukisikia mapungufu ya serikali nenda katoe taarifa sehemu husika ili yafanyiwe kazi na si vinginevyo.
 
Nini maana ya malizana nae, nyooka nae? Ukomo wa kumalizana nae na kunyooka nae ni upi? anamalizana na kunyooka nae mpaka wapi?

Haiwezekani hii itokee hivi. Kauli kama hii ni hatari sana kwa taifa. Kauli kama hii ikitoka kwa kiongozi mkubwa kama Spika ni agizo. Kama Rais asipoitolea ufafanusi itamchafulia sana kitaifa na kimataifa. Hata Rais Biden anakosolewa pia.

 
Ndugai alisema tofauti mkamfukuza, mkamshikiza, akatoka huyo unasema anahujumiwa aka mchamba sana tu, leo amesemwa hivi anahujumiwa!
 
Back
Top Bottom