Dodoma,Jumanne 29/08/2023.
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezuia mjadala wa makata wa bandari kujadiliwa ikiwa tayari Bunge limeishamaliza majukumu yake ya awali, huku akisema linaweza kujadiliwa endapo litaletwa katika utaratibu mwingine wa kibunge.Spika Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 29, 2023, muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya wabunge ambapo amesema kuwa Bunge lilishamaliza mjadala huo hivyo wabunge wanatakiwa kuendelea kuwasikiliza wananchi.
Katika mkutano wa 11 wabunge walipitisha makubaliano ya mpango wa Serikali katika kuingia makubaliano na DP World katika kuendesha bandari, ambapo kumekuwa na mjadala mrefu ukihusisha wanasiasa, wanasheria, wanaharakati, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla.
SOURCE.
Mwananchi online Newspapers.29/08/2023.