Ziko taarifa kuwa Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu katika mikoa yote wanapanga kusoma Albadir usiku leo kama sehemu ya kumshitakia mwenyezi Mungu kwa tukio la kuuza bandari kwa Waarabu linalofanywa na wabunge kesho.
Wanazuoni hao wamefikia hatua hiyo baada ya kuona njia zote walizotumia kuwashauri wabunge wakatae jambo hilo kushindikana baada ya kuwepo taarifa za kuwepo mashinikizo makubwa ya fedha walizopewa wabunge hao ili waone hilo ni jambo jema kwa nchi.