Spika Tulia kila kitu hujui ni bora ujiuzulu

Spika Tulia kila kitu hujui ni bora ujiuzulu

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Mara kadhaa nimekuwa nikifuatilia Bunge hasa akiongoza Spika, Dk. Tulia kila jambo analosema Mbunge yeye anasema halijui afundishwe au aeleweshwe, mtakumbuka sakata la TRAB na TRAT aliuliza ndio kituo gani hicho? Sasa unawezaje kuwa Spika hujui hata maana ya TRAB na TRAT.

Mara ya pili niliyomuona Spika ni kutojua Bwawa la Mwalimu Nyerere linagusa mikoa mingapi.. inawezekana vipi Mradi mkubwa kama huu unatekelezwa nchini alafu Spika wa Bunge la nchi hajui Bwawa hilo linapatikana mikoa gani.

Kituko kingine nimeona jana akibishana kuhusu matumizi ya neno LAKI kwenye upitishaji wa vifungu vya Bajeti hajui kama LAKI halimo kwenye namba za kuhesabu.

Tulia anakuwa anapoteza muda kubishana mambo ambayo hayana tija badala ya kusimama imara kuhakikisha Serikali inatimiza wajibu kwa wananchi.

Sasa kila kitu Spika hajui anawezeshaje kukaa kwenye kiti kikubwa namna hiyo kwanini Zungu yeye haborongi anapoongoza Bunge au wale wenyeviti.. Kwanini yeye tu ndio hajui kila kitu.
 
YULE MDADA HATA MIE SIELEWI ANAFANYA NINI PALE MJENGON, ET WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE KWA SHERIA IPI?
 
Kimbaumbau hana uchungu na Tozo zetu na kodi zinavyoliwa.
 
Hawa wakoloni weusi Naona wameungana wamalize wanyonge kabisa.
 
Wewe ndio umeboronga. Hakuna kiongozi anayejua mambo yote ya kitaalamu na kujifanya mjuaji ni ujinga zaidi.

Mara zote anapoomba ufafanuzi ni kwa faida yake na wabunge wengine wote ili waweze kujadili hoja wakiwa na uelewa wa pamoja. Watanzania mbona mnakuwa hivi?
 
Sasa spika atajua kila kitu jamani mambo mengine muangalie mnapolaumu jamani, yeye ni professional kwenye sheria sasa hizo concept za kichumi anaweza kujua kila kitu kweli jamani, wewe sio mfamasia wala sio daktari utaweza kujua terminology zote za kifamasia au kidaktari mbona kwenye kusimamia kanuni yupo vizuri lakini ni kwanin kwasababu ni mwanasheria by professional huko kwingine akiwa na idea sio vibaya Tusipende laumu mambo madogo madogo kama haya jamani

lazima aulize jambo vizuri ajirizishe bunge ni chombo muhimu chenye kutazamwa na wengi na lenye maamuzi ya mustakabali wa taifa hapa nchini na hata nyanja za kimataifa

SPIKA ANAJITAHIDI SANA.
 
Ujuaji mwingi huharibu mambo naamimi watanzania kibao hawaelewi yanayozungumzwa pale hivyo anasaidia uma kuelewa nn kinaongelewa
 
Huyo mwanamke hana akili na ni wa hovyo sana na hakuchaguliwa kuwa naibu spika kipindi cha dikteta Magufuli kwa sababu ya weledi bali kuna mambo mengine yanayohusiana na jinsia yake ndiyo yaliyo mbeba.

Kwenye katiba mpya tunataka spika awe ni mtu ambaye hajawahi kabisa kujihusisha na siasa za vyama kama huyu mwanamke. Bunge la sasa ni kama klabu ya pombe tu halina maana kabisa.
 
Huyo mwanamke hana akili na ni wa hovyo sana na hakuchaguliwa kuwa naibu spika kipindi cha dikteta Magufuli kwa sababu ya weledi bali kuna mambo mengine yanayohusiana na jinsia yake ndiyo yaliyo mbeba.

Kwenye katiba mpya tunataka spika awe ni mtu ambaye hajawahi kabisa kujihusisha na siasa za vyama kama huyu mwanamke. Bunge la sasa ni kama klabu ya pombe tu halina maana kabisa.
Mkuuu taratibu,mods wanaupitia uzi huu...maana hawatak spika asemwe[emoji23]
 
Back
Top Bottom