VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Suala la Mpina halipuuziki. Sema nasi tusikie. Mbunge Luhaga J. Mpina alidai bungeni kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amelidanganya Bunge kuhusu sakata la uingizwaji wa sukari nchini. Alidai, pamoja na mambo mangine kuwa Bashe alisema uongo zaidi ya mara kumi.
Kwa mujibu wa Mpina, Waziri Bashe alidanganya kuhusu utaratibu na takwimu muhimu kuhusu uagizwaji, uzalishwaji na usambazaji wa sukariu hapa nchini. Alidanganya ili kuficha ufisadi uliopo kwenye sukari [ambao Bashe anahusishwa nao pamoja na Waziri wa Fedha-Mwigulu].
Mpina alitakiwa nawe Spika awasilishe ushahidi wa kuthibitisha madai yake ya Waziri Bashe kusema uongo. Alipewa siku za kufanya hivyo. Akafanya hivyo. Mpina aliwasilisha ushahidi jadidi kuhusu uongo wa Bashe bungeni na sakata zima la sukari hapa nchini.
Katika namna ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, Bunge lako likaibuka na hoja ya kwamba Mpina amekiuka utaratibu wa kibunge: kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ushahidi wake huo kabla ya kufanyiwa kazi na Spika. Mpina akaitwa Kamati ya Maadili. Akajadiliwa Bungeni. Akapewa adhabu ya kutohudhuria vikao 15 vya Bunge.
Ukweli kuhusu kukiuka au kutokiuka utaratibu kwa Mpina na uhalali wa adhabu yake mnaujua wenyewe. Sisi wananchi ambao huguswa na kuumizwa na upatikanaji na bei ya sukari tunataka kuujua ukweli. Je, ni kweli kuwa Bashe alisema uongo na anahusika (pamoja na Mwigulu na wengineo) na ufisadi kwenye suala la sukari?
Je, ushahidi wa Mpina, ambao tayari ulishapokelewa na Spika, umethibitisha madai yake au la? Spika Tulia, jitokeze hima utuambie wananchi. Muda ni huu.
Mhe. Rais Mama Samia, jitokeze umalizane na wafanyabiashara!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)