CHIEF PRIEST
JF-Expert Member
- Dec 13, 2021
- 11,635
- 21,347
Rango kama RangoTulia ni muhuni kama wahuni wengine sema yeye anapulizia chooni!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rango kama RangoTulia ni muhuni kama wahuni wengine sema yeye anapulizia chooni!
..Hawezi kusema kitu, jua tu kina RANGO ni maadui wa taifa, wako pale kuona taifa linaamgamia, walichokifanya ni ushahidi tosha.
Kama ulisikiliza vizuri mpina hana hoja ya msingiTulia anazidi kuonesha udhaifu wake.Mpina akimaliza adhabu feki ndiyo ataanza kusikilizwa hoja zake?
Vipi hoja za Mpina? Ni za uongo?Mpina
anatetea tumbo lake wewe bwege kwa kuwakilisha wanaomlipa. Mbona akiwa kwenye Serikali ya DHALIMU Magufuli aliwatia hasara wafanyabiashara wengi wa uvuvi kule kanda ya ziwa kwa kuwachomea nyavu?
Kwa taarifa yako huyu Mpina anamiliki ekari za ardhi zaidi ya 1,000 huko Morogoro. Je kazipataje?
Jiulize angekuwa leo ni Waziri kwenye Serikali ya Samia angeweza kuja na hoja hiyo?
Sipendi utumike kuwaneemesha wanasiasa walio kwenye mashindano ya ufisadi. Waache waparurane wenyewe
Acha mkuu kuzushia watu uongo....sio poa kabisa.Siyo tu Bashe amelidanganya Bunge. Za ndani kabisa ni kuwa Bashe ana malipo haramu kutoka kwa waagizaji, kiasi cha sh bilioni 36. Malipo yake ni sh 100 kwa kila kilo.
Rais awaambie wananchi, anasimama na fisadi kama alivyofanya kwenye report ya CAG, au anasimama na wananchi, ili wananchi wajue kama wana serikali inayowadhulumu au inayowahudumia.
Mpina
anatetea tumbo lake wewe bwege kwa kuwakilisha wanaomlipa. Mbona akiwa kwenye Serikali ya DHALIMU Magufuli aliwatia hasara wafanyabiashara wengi wa uvuvi kule kanda ya ziwa kwa kuwachomea nyavu?
Kwa taarifa yako huyu Mpina anamiliki ekari za ardhi zaidi ya 1,000 huko Morogoro. Je kazipataje?
Jiulize angekuwa leo ni Waziri kwenye Serikali ya Samia angeweza kuja na hoja hiyo?
Sipendi utumike kuwaneemesha wanasiasa walio kwenye mashindano ya ufisadi. Waache waparurane wenyewe
Ungekuwa una akili ungetoa point. Ila kwa vile huna uwezo wa kuchanganua unatoa sweeping statement. Kima wewe kaa kimya
Wacha wivu kenge wewe. Nyie mlipokuwa mnaiba awamu ya Magufuli unadhani tulikuwa hatuumii? Tena mlikuwa mnaiba, mnaua, mnateka watu na kutubana hata uhuru wa maoniUnamawazo ya kitoto sana.
Watu wanaiba. na huku maisha yakiendelea kuwa duni.
Watu wanapeana deal, tunalipa 1000 zaidi ya bei harisi. Ubora wa sukali uko duni.
Changamka ili nchi ipige hatua.
Tunahitaji majibu.
Wewe una haki ya kumpeleka Bashe kwenye vyombo vya dola na siyo kulialia hapa. Sisi tunataka sukari yenye ubora kwa bei ya Tsh 1,800/= kwa kilo.Wewe ndiyo bwege halisi. Malipo haramu aliyoyapokea Bashe kutoka kwa waagizaji, yanatetea tumbo lako wewe, siyo watanzania.
Fisadi Bashe, anastahili adhabu kali, na Rais kama hatamchukulia hatua basi wananchi watakuwa wametangaziwa rasmi kuwa tuna Serikali ambayo ni ya mafisadi kwaajili ya kulinda mafisadi na ufisadi.
Ilete hapa hiyo sheria.Sheria ya uvuvi inasemaje kuhusu nyavu aina hiyo (makokolo)?
Mpina alikua wa kwanza kuchoma nyavu nchi hii?
Hoja iliyopo mezani ni Mpina kutumika na Tajiri wa Superdoll ambaye ni mmiliki wa Mtubwa Sugar na Kagera Sugar, periodPamoja na yote haimaanishi kwamba hawezi kuongelea ufisadi wa sukari eti kwa kuwa tu alikosea (kwa hukumu yako) huko nyuma. Hoja iliyopo mezani inajibiwa kwa hoja mezani sio historia
Aisee...Ukiona CCM hawaelewani ujue dili ni la mkuu zaidi anahusika ,keep watching
Suala la Mpina halipuuziki. Sema nasi tusikie. Mbunge Luhaga J. Mpina alidai bungeni kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amelidanganya Bunge kuhusu sakata la uingizwaji wa sukari nchini. Alidai, pamoja na mambo mangine kuwa Bashe alisema uongo zaidi ya mara kumi.
Kwa mujibu wa Mpina, Waziri Bashe alidanganya kuhusu utaratibu na takwimu muhimu kuhusu uagizwaji, uzalishwaji na usambazaji wa sukariu hapa nchini. Alidanganya ili kuficha ufisadi uliopo kwenye sukari [ambao Bashe anahusishwa nao pamoja na Waziri wa Fedha-Mwigulu].
Mpina alitakiwa nawe Spika awasilishe ushahidi wa kuthibitisha madai yake ya Waziri Bashe kusema uongo. Alipewa siku za kufanya hivyo. Akafanya hivyo. Mpina aliwasilisha ushahidi jadidi kuhusu uongo wa Bashe bungeni na sakata zima la sukari hapa nchini.
Katika namna ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, Bunge lako likaibuka na hoja ya kwamba Mpina amekiuka utaratibu wa kibunge: kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ushahidi wake huo kabla ya kufanyiwa kazi na Spika. Mpina akaitwa Kamati ya Maadili. Akajadiliwa Bungeni. Akapewa adhabu ya kutohudhuria vikao 15 vya Bunge.
Ukweli kuhusu kukiuka au kutokiuka utaratibu kwa Mpina na uhalali wa adhabu yake mnaujua wenyewe. Sisi wananchi ambao huguswa na kuumizwa na upatikanaji na bei ya sukari tunataka kuujua ukweli. Je, ni kweli kuwa Bashe alisema uongo na anahusika (pamoja na Mwigulu na wengineo) na ufisadi kwenye suala la sukari?
Je, ushahidi wa Mpina, ambao tayari ulishapokelewa na Spika, umethibitisha madai yake au la? Spika Tulia, jitokeze hima utuambie wananchi. Muda ni huu.
Mhe. Rais Mama Samia, jitokeze umalizane na wafanyabiashara!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)